Tamko Rasmi la Wanafunzi wa Vyuo vya Dodoma

Tamko Rasmi la Wanafunzi wa Vyuo vya Dodoma

TAMKO LA UONGOZI WA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU DODOMA KULAANI KUHUSISHWA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA DODOMA NA KUMUOMBA MH. LOWASA KUGOMBEA URAIS.

Ndugu Waandishi wa habari, Tunapenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu kwa kufika katika eneo hili kutusikiliza.Mbele yenu ni viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka Vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo mkoani Dodoma.Ndugu waandishi wa habari,si kawaida na wala mazoea kwa marais na viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo tofauti kukutana kwa pamoja na kuzungumza na nyie wanahabari kama inavyotokea hii leo.

Ndugu wanahabari,siku ya Jumapili ya tarehe 22 mwezi huu wa 3,kundi la watu waliojitambulisha kama ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma walijikusanya nyumbani kwa mh; Lowasa na kutoa matamko mbalimbali ikiwa pamoja na kuutangazia uma wa watanzania kuwa sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma tunamuunga mkono na tunahitaji Lowasa awe rais wetu sambamba kumchangia pesa.

Ndugu wanahabari,Tunapenda kukanusha kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma kwa ujumla wetu hatukuhusika na jambo lile na kama viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya mkoa huu wa Dodoma,Tunapinga na kulaani kitendo cha watu wachache kwenda kutuingiza sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma katika jambo ambalo halituhusu na wala si lililotuleta hapa Dodoma.

Sisi kama wasomi ambao jamii inatutegemea kama kioo hatuwezi kuandamana na kujikusanya kwenye nyumba ya kiongozi na kumuomba agambee urais, wakati tunajua fika sisi hatuhusiki na uteuzi wa wagombea ndani ya taasisi yao.Kilichofanyika ni kuudanganya uma wa watanzania na taasiasi yake kupitia kivuli cha vijana wachache kutoka vyuo vya hapa Dodoma,waliolipwa pesa ili waweze kuwa kava la tukio lile.

Ndugu wanahabari,Mkoa wa Dodoma unavyuo vikuu visivyopungua 8,Na jumla ya wanafunzi wote tunaosoma katika vyuo vya Dodoma ni zaidi ya wanafunzi 35,000.Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) pekee yake kinawanafunzi wasiopungua 22,000.Idadi ya watu waliojikusanya nyumbani kwa Mh: Lowasa siku ya tarehe 22-03-2015 haizidi watu 230 wakiwemo Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi, kama vyombo vya habari vilivyoripoti.

Ukiwatoa Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi waliotoka mikoa mbalimbali,idadi ya wanafunzi waliokuwepo kwenye tukio lile hawazidi 150.Idadi hii ni sawa na asilimia 0.4 ya wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma.Ndugu wanahabari,kwa akili ya kawaida kabisa asilimia 0.4 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ndio waliokuwa pale.Tunashangazwa na dhambi tusiyoitenda tunayobebeshwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao kwa sasa tupo bize na msimu mpya ya masomo wenye changamoto mbalimbali.

Ndugu wanahabari,sisi kama vijana wasomi na watu tunaotegemewa na jamii zetu tutakusanyika katika kujadili na kuchambua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii yetu na sio kukusanyika kwa ajili ya mwanasiasa ambaye sifa zake na uhadilifu wake unatiliwa shaka katika jamii.Tunaomba mlijulishe Taifa, kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma hatujahusika na tukio lile isipokuwa wanafunzi wachache walitumika kwa kupewa pesa na wahusika wa tukio lile.Tunataka Taifa lijue hatupo tayari kutumia elimu zetu kulitia upofu taifa letu.

Waambieni mama zetu na baba zetu huku vijijini kwetu kuwa tumekuja kutafuta elimu ili ituwezeshe kuwakomboa wao na sio kutumika na Wanasiasa kwa malengo yao.Tunatambua haki ya mwanafunzi kuamua na kufanya shughuli za kisiasa nje ya maeneo ya vyuo, lakini hatukubaliani na wanafunzi wachache kuchafua na kuwapaka matope maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao hawajahusika na tukio lile.Hii sio haki na haikubaliki.

Vilevile tungependa kutumia fursa hii kuwaasa wanafunzi wenzetu popote pale nchini, makundi mbalimbali ya kijamii (wakulima, wafugaji, wavuvi, wamachinga, wasanii, n.k), zikiwemo taasisi za dini kwamba watu wachache kuzungumza kwa niaba ya makundi juu ya mambo yanayogusa maamuzi ya mtu binafsi.

Mwisho tunatoa wito kwa wanafunzi wenzetu wote kujitambua na kutumie muda wetu kwa mambo ya msingi na muhimu kwa ustawi wa Nchi yetu. Na kuonesha jinsi wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma walivyokasilishwa na jambo hili, Tamko hili limesainiwa na wanafunzi 7821 toka vyuo mbali mbali vya Dodoma.Majina ya sahihi za wanafunzi zimeambatanishwa. Tusikubali kutumika na wanasiasa wa aina hii.

Asanteni

Mungu ibariki Tanzania,Mungu vibariki vyuo vikuu vya Dodoma.

Kwa niaba ya wawakilishi wa serikali za Wanafunzi Chuo cha Mipango,Chuo cha Madini, Chuo cha Hombolo,Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) na CBE.

DANIEL DANIEL -Rais wa Saint Jonh’s University

26/03/2015

Asanteni sana mkuu DANIEL,maana mimi binafsi nilistushwa sana na habari hizi heti wanafunzi wa UDOM waandamana kumshawishi mtu FISADI agombee urais wa TZ! hakika ilinipa shida sana maana naamini kuwa watanzania waliowengi ni wepesi wa kusahau na kupoteza kumbukumbu lakini nikajiuliza na wanafunzi pia!wasomi nao wamo! sasa nimeamini njaa ni mbaya sana, yaani hao wenzenu wachache waendekeza njaa wanakubali kudhalilisha taaluma zao kwa kuhongwa Tshs 15,000 ili waandamane na kutengeneza MOVIE ili ionekane LOWASA kaombwa na makundi mbalimbali,this is shame on them!bila shaka hawa wenzenu waliokubali kucheza hii movie hata darasani watakuwa ni zero kabisaa!
 
Umesahau waendesha bodaboda sijui miangapi kutoka Mbeya Mbarali. Leo uongozi wa Mbarali umekanusha na kuseam huo nimpango wamtu mmoja aliwashawishi waendesha bodaboda 7 kutoka kule. Waliofika dodoma ni 50 na haijulikani wengine aliwapata wapi. Na isitoshe WANAOSEMWA ETI NI WAENDESHA bodaboda, kunawengine hata kuendesha hizo pikipiki hawajui.

Kama vile mashehe n.k.

Ndugu zangu, Watanzania, Tusirudie makosa yakurubuniwa na makeke ya kisanii kama ya kikwete. Lowasa na kikwete ni mtu mmoja.

Ninaomba Ccm wamchukulie hatua za kinidhamu Lowasa kwa sababu anadhalilisha Utanzania. Ni dhalilil kwa taifa kuwa na mtu wa umri ule, aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa kabisa serikalini ingawa alifukuzwa kwa wizi na udanganyifu, halafu anatumia udanganyifu huu kuvunja sheria ili kulipotosha taifa.

Lowasa ni adui mkubwa sana wa maendeleo na haki za watanzania.

KWA SASA WATANZANIA TUNA LENGO MOJA TU. KUKOMBOA TAIFA. HATUTAKI KUMWONA WALA KUSIKIA FISADI, MWONGO NA MHUNI KAMA LOWASA AKITUPOTEZEA MUDA. Ccm mchagueni kusimamia chama chenu lakini serikali ya Tanzania haiwezi kuwa chini ya Lowasa.


Team Lowasa, ninawaomba ushauri wenu uishie ccm, na si kutuvuruga hapa na uhuni wenu wa kijinga hapa. Kwa taarifa, CCM HAINA NAFASI YA KUONGOZA NCHI HII TENA. NA MBINU MNAZOTUMIA KAMA ZA KUKODISHA WAHUNI NA KUWAVALISHA MABANGO KWENDA KUSHAWISHI WATU WENYE UCHU NA UONGOZI TAYARI, NDILO KABURI LA CHAMA CHENU.

NIMESEMA NA IMEKUWA.


mimi kwakweli napata wakati mgumu kiasi fulani kuhusu watu wanaoenda kumshawishi Lowassa agombee urais, maana kila kundi likienda kesho yake wanaibuka wengine kupinga. walianza Masheikh wa Bagamoyo, kesho yake akaibuka sheikh mkuu wa bagamoyo akawakana na kudai hawatambui hao masheikh. Wakaja wanafunzi wa vyuo vya Dodoma, leo hii marais wa hivyo vyuo wameibuka na tamko kupinga. Pia ilikuwa hivyo hivyo kwa wachungaji wa makanisa ya kipentecoste. Swali hapa hao wanaojitokeza kumshawishi Lowassa huwa hawawasiliana na viongozi wao wa juu?
 
mimi kwakweli napata wakati mgumu kiasi fulani kuhusu watu wanaoenda kumshawishi Lowassa agombee urais, maana kila kundi likienda kesho yake wanaibuka wengine kupinga. walianza Masheikh wa Bagamoyo, kesho yake akaibuka sheikh mkuu wa bagamoyo akawakana na kudai hawatambui hao masheikh. Wakaja wanafunzi wa vyuo vya Dodoma, leo hii marais wa hivyo vyuo wameibuka na tamko kupinga. Pia ilikuwa hivyo hivyo kwa wachungaji wa makanisa ya kipentecoste. Swali hapa hao wanaojitokeza kumshawishi Lowassa huwa hawawasiliana na viongozi wao wa juu?

watawasliana vipi na viongozi wao wakati wanaenda kutengeneza MOVIE feki?
 
kumbe wanafunzi wa vyuo vya Dodoma ni vilaza namna hii. Tamko gani hili utadhani limeandikwa na mtoto wa darsa la tatu? ndio maana wanasiasa uchwara wanayatumia sana haya madent ya Dodoma

Mpuzi wew unaweza kuandika tamko kama lile au unakurupuka tu km mtt wa chekechea
 
Nilidhani limetolewa na yule Rais wa wanafunzi wa UDOM aliyesoma risala fupi nyumbani kwa Lwaigwaini!... Kumbe la linatoka kwa Rais wa St John!
 
Nyie ndio mnaotumiwa na Nepi mje kuupotosha umma wa watz sio,kw hilo mmechelewa sana mnakumbuka shuka tyr kumekucha,watz ujumbe umeshafika kwao kwamba Makundi mbalmbali yana muunga mkono ktk mbio zake za kuwani urais tofauti na mtu yyte kwa sasa na El ndio tumaini la watz wengi,hizo propaganda zenu zimechelewa mno yan labda mngeanza kabla makundi kufika kwa EL huenda mngefanikiwa kuturubun huo ujingA wenu,Lowassa ndo habar ya mjin aisee bnafsi cjaona mbadala wake labda ww mleta mada nan unaona anacfa za kutuongoza zaidi ya EL

wewe ni kilaza tu!yaani huoni hata aibu heti LOWASA ndio chaguo la watanzania wengi,pole sana!watu wenye akili timamu na kumbukumbu sahihi kamwe hawawezi mkubali LOWASA awe RAIS wa Taifa hili! wewe na upeo wako mdogo ndio utaendelea kumsifia huyo FISADI!Wasalimie SUMBAWANGA! 5/37.
 
Wewe unae jiita raisi wa st john yani ni mjinga unafanana na jina lako. yani bora hata ungekaa kimya maana hakuna unacho taka kuwaambia watazania ulikuwa wapi eti leo ndio unajidai kulaan Baada ya kuwa umepewa vipesa useme hayo uliyo yasema nenda kalaaani kwa mamaako na babaako usituletee ujinga
 
Lowassa ndio Rais mtajiwa watz wengi tunaimani nae,sio hao wagombea wenu ambao hawauzik ktk jamii yetu.
 
wewe ni kilaza tu!yaani huoni hata aibu heti LOWASA ndio chaguo la watanzania wengi,pole sana!watu wenye akili timamu na kumbukumbu sahihi kamwe hawawezi mkubali LOWASA awe RAIS wa Taifa hili! wewe na upeo wako mdogo ndio utaendelea kumsifia huyo FISADI!Wasalimie SUMBAWANGA! 5/37.

Kilaza mamako
 
Halafu eti na wewe unajiita msomi tena eti raisi wa serikali ya wanafunzi pumbavu kabisa hizo laana alizo kufundisha bibiyako ukazilaanie huko kwenu na wewe ulaaniwe, ---- kabisa siku zote hizo, baada ya kupewa pesa eti unatoa tamko, hilo tamko kamtolee mamaako,halafu hivi st john ni chuo au tuition center. maana sidhani kama kweli chuo kitakuwa na raisi tahila kama huyu anejiita Daniel
 
tamko la uongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu dodoma kulaani kuhusishwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma na kumuomba mh. Lowasa kugombea urais.

ndugu waandishi wa habari, tunapenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu kwa kufika katika eneo hili kutusikiliza.mbele yenu ni viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo mkoani dodoma.ndugu waandishi wa habari,si kawaida na wala mazoea kwa marais na viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo tofauti kukutana kwa pamoja na kuzungumza na nyie wanahabari kama inavyotokea hii leo.

Ndugu wanahabari,siku ya jumapili ya tarehe 22 mwezi huu wa 3,kundi la watu waliojitambulisha kama ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma walijikusanya nyumbani kwa mh; lowasa na kutoa matamko mbalimbali ikiwa pamoja na kuutangazia uma wa watanzania kuwa sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma tunamuunga mkono na tunahitaji lowasa awe rais wetu sambamba kumchangia pesa.

Ndugu wanahabari,tunapenda kukanusha kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma kwa ujumla wetu hatukuhusika na jambo lile na kama viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya mkoa huu wa dodoma,tunapinga na kulaani kitendo cha watu wachache kwenda kutuingiza sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma katika jambo ambalo halituhusu na wala si lililotuleta hapa dodoma.

Sisi kama wasomi ambao jamii inatutegemea kama kioo hatuwezi kuandamana na kujikusanya kwenye nyumba ya kiongozi na kumuomba agambee urais, wakati tunajua fika sisi hatuhusiki na uteuzi wa wagombea ndani ya taasisi yao.kilichofanyika ni kuudanganya uma wa watanzania na taasiasi yake kupitia kivuli cha vijana wachache kutoka vyuo vya hapa dodoma,waliolipwa pesa ili waweze kuwa kava la tukio lile.

Ndugu wanahabari,mkoa wa dodoma unavyuo vikuu visivyopungua 8,na jumla ya wanafunzi wote tunaosoma katika vyuo vya dodoma ni zaidi ya wanafunzi 35,000.chuo kikuu cha dodoma (udom) pekee yake kinawanafunzi wasiopungua 22,000.idadi ya watu waliojikusanya nyumbani kwa mh: Lowasa siku ya tarehe 22-03-2015 haizidi watu 230 wakiwemo wamachinga na wenyeviti wa jumuiya za wazazi, kama vyombo vya habari vilivyoripoti.

Ukiwatoa wamachinga na wenyeviti wa jumuiya za wazazi waliotoka mikoa mbalimbali,idadi ya wanafunzi waliokuwepo kwenye tukio lile hawazidi 150.idadi hii ni sawa na asilimia 0.4 ya wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu vya dodoma.ndugu wanahabari,kwa akili ya kawaida kabisa asilimia 0.4 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ndio waliokuwa pale.tunashangazwa na dhambi tusiyoitenda tunayobebeshwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma ambao kwa sasa tupo bize na msimu mpya ya masomo wenye changamoto mbalimbali.

Ndugu wanahabari,sisi kama vijana wasomi na watu tunaotegemewa na jamii zetu tutakusanyika katika kujadili na kuchambua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii yetu na sio kukusanyika kwa ajili ya mwanasiasa ambaye sifa zake na uhadilifu wake unatiliwa shaka katika jamii.tunaomba mlijulishe taifa, kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma hatujahusika na tukio lile isipokuwa wanafunzi wachache walitumika kwa kupewa pesa na wahusika wa tukio lile.tunataka taifa lijue hatupo tayari kutumia elimu zetu kulitia upofu taifa letu.

Waambieni mama zetu na baba zetu huku vijijini kwetu kuwa tumekuja kutafuta elimu ili ituwezeshe kuwakomboa wao na sio kutumika na wanasiasa kwa malengo yao.tunatambua haki ya mwanafunzi kuamua na kufanya shughuli za kisiasa nje ya maeneo ya vyuo, lakini hatukubaliani na wanafunzi wachache kuchafua na kuwapaka matope maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma ambao hawajahusika na tukio lile.hii sio haki na haikubaliki.

Vilevile tungependa kutumia fursa hii kuwaasa wanafunzi wenzetu popote pale nchini, makundi mbalimbali ya kijamii (wakulima, wafugaji, wavuvi, wamachinga, wasanii, n.k), zikiwemo taasisi za dini kwamba watu wachache kuzungumza kwa niaba ya makundi juu ya mambo yanayogusa maamuzi ya mtu binafsi.

Mwisho tunatoa wito kwa wanafunzi wenzetu wote kujitambua na kutumie muda wetu kwa mambo ya msingi na muhimu kwa ustawi wa nchi yetu. Na kuonesha jinsi wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma walivyokasilishwa na jambo hili, tamko hili limesainiwa na wanafunzi 7821 toka vyuo mbali mbali vya dodoma.majina ya sahihi za wanafunzi zimeambatanishwa. Tusikubali kutumika na wanasiasa wa aina hii.

Asanteni

mungu ibariki tanzania,mungu vibariki vyuo vikuu vya dodoma.

Kwa niaba ya wawakilishi wa serikali za wanafunzi chuo cha mipango,chuo cha madini, chuo cha hombolo,chuo kikuu cha dodoma(udom) na cbe.

daniel daniel -rais wa saint jonh’s university

26/03/2015

hakuna mtu atakayewafukuza chuoni mbona mnahanya hanya,waliokuja wote ni wanafunzi wa udom na hilo halina ubishi,angalia sura utawagundua wengi
 
Lowassa ndio Rais mtajiwa watz wengi tunaimani nae,sio hao wagombea wenu ambao hawauzik ktk jamii yetu.

Urais siyo bidhaa. Mkiuchukulia ni bidhaa ndiyo haya mnayofanya ya kununua watu na kujifanya wanakwenda kumshawishi mwizi aingie Ikulu. Kama mnaona urais ni bidhaa tusitumie nguvu nyingi tuone mwezi wa 5 ukifika hiyo bidhaa kama itawekwa hadharani watu waichangamkie. Tunaelewa fika watu wwadilifu na wazuri wapo ila wanawekewa mizengwe lakini kwa mwaka huu jiandaeni kupigwa na butwaa. Mtu wenu ataishia msikotarajia. CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA
 
Hahahhahahaaa ujenzi wa mnara wa Babeli sijui contractor wake ni nani???
 
Katuni Feb 2.jpg
kifo cha nyani miti huteleza ndo ilivyo kwa EL anayetumia pesa zake kuwanunua watu na kutangaza wameenda kumwomba kugombea uraisi mwaka huu tutashuhudia matamko mengi sana ya kupinga huu usanii wa EL bado kesho utasikia wale wachungani walikuwa ni wasanii kwa sababu zile nguo za uchungaji hata waigizaji wa bongo movies huwa wanavaa wanavyoigiza kama mchungaji hii movie itavunja rekodi .
 
hakuna mtu atakayewafukuza chuoni mbona mnahanya hanya,waliokuja wote ni wanafunzi wa udom na hilo halina ubishi,angalia sura utawagundua wengi
walikuonyesha vitambulisho vyao unashabikia tuu ujinga
 
Hawa hamna kitu halafu ndio wasomi watarajiwa mimi kuna kautafiti nilishakafanya siku nyingi kuna jambo la kushangaza na la kufurahisa analoweza kufanya mtu ambae hana elimu na likamshangaza hata profesa manake hii jamii huwq inajitahidi kutumia akili ya kuzaliwa na kuchanganya na maarifa lakini kuna msomi hawa wanaojiita wasomi wanaweza kufanya kitu chenye kb 1mpaka ukajiuliza huyu ni msomi kweliii ama alifoji? Ukweli una baki kuwa ukweli samaki mmoja akioza ni wote wameoza.

Hivo unasema kua kwakua wew ni mbulula hivo kila mtanzania ni mbulula? Acha kuendekeza hisia badala yale ziruhusu akili zako zifikiri na si kukariri. Asante, nimekusamehe usirudie tena.
 
Back
Top Bottom