Tamko Rasmi la Wanafunzi wa Vyuo vya Dodoma

Tamko Rasmi la Wanafunzi wa Vyuo vya Dodoma

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
TAMKO LA UONGOZI WA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU DODOMA KULAANI KUHUSISHWA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA DODOMA NA KUMUOMBA MH. LOWASA KUGOMBEA URAIS.

Ndugu Waandishi wa habari, Tunapenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu kwa kufika katika eneo hili kutusikiliza.Mbele yenu ni viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka Vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo mkoani Dodoma.Ndugu waandishi wa habari,si kawaida na wala mazoea kwa marais na viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo tofauti kukutana kwa pamoja na kuzungumza na nyie wanahabari kama inavyotokea hii leo.

Ndugu wanahabari,siku ya Jumapili ya tarehe 22 mwezi huu wa 3,kundi la watu waliojitambulisha kama ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma walijikusanya nyumbani kwa mh; Lowasa na kutoa matamko mbalimbali ikiwa pamoja na kuutangazia uma wa watanzania kuwa sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma tunamuunga mkono na tunahitaji Lowasa awe rais wetu sambamba kumchangia pesa.

Ndugu wanahabari,Tunapenda kukanusha kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma kwa ujumla wetu hatukuhusika na jambo lile na kama viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya mkoa huu wa Dodoma,Tunapinga na kulaani kitendo cha watu wachache kwenda kutuingiza sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma katika jambo ambalo halituhusu na wala si lililotuleta hapa Dodoma.

Sisi kama wasomi ambao jamii inatutegemea kama kioo hatuwezi kuandamana na kujikusanya kwenye nyumba ya kiongozi na kumuomba agambee urais, wakati tunajua fika sisi hatuhusiki na uteuzi wa wagombea ndani ya taasisi yao.Kilichofanyika ni kuudanganya uma wa watanzania na taasiasi yake kupitia kivuli cha vijana wachache kutoka vyuo vya hapa Dodoma,waliolipwa pesa ili waweze kuwa kava la tukio lile.

Ndugu wanahabari,Mkoa wa Dodoma unavyuo vikuu visivyopungua 8,Na jumla ya wanafunzi wote tunaosoma katika vyuo vya Dodoma ni zaidi ya wanafunzi 35,000.Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) pekee yake kinawanafunzi wasiopungua 22,000.Idadi ya watu waliojikusanya nyumbani kwa Mh: Lowasa siku ya tarehe 22-03-2015 haizidi watu 230 wakiwemo Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi, kama vyombo vya habari vilivyoripoti.

Ukiwatoa Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi waliotoka mikoa mbalimbali,idadi ya wanafunzi waliokuwepo kwenye tukio lile hawazidi 150.Idadi hii ni sawa na asilimia 0.4 ya wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma.Ndugu wanahabari,kwa akili ya kawaida kabisa asilimia 0.4 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ndio waliokuwa pale.Tunashangazwa na dhambi tusiyoitenda tunayobebeshwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao kwa sasa tupo bize na msimu mpya ya masomo wenye changamoto mbalimbali.

Ndugu wanahabari,sisi kama vijana wasomi na watu tunaotegemewa na jamii zetu tutakusanyika katika kujadili na kuchambua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii yetu na sio kukusanyika kwa ajili ya mwanasiasa ambaye sifa zake na uhadilifu wake unatiliwa shaka katika jamii.Tunaomba mlijulishe Taifa, kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma hatujahusika na tukio lile isipokuwa wanafunzi wachache walitumika kwa kupewa pesa na wahusika wa tukio lile.Tunataka Taifa lijue hatupo tayari kutumia elimu zetu kulitia upofu taifa letu.

Waambieni mama zetu na baba zetu huku vijijini kwetu kuwa tumekuja kutafuta elimu ili ituwezeshe kuwakomboa wao na sio kutumika na Wanasiasa kwa malengo yao.Tunatambua haki ya mwanafunzi kuamua na kufanya shughuli za kisiasa nje ya maeneo ya vyuo, lakini hatukubaliani na wanafunzi wachache kuchafua na kuwapaka matope maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao hawajahusika na tukio lile.Hii sio haki na haikubaliki.

Vilevile tungependa kutumia fursa hii kuwaasa wanafunzi wenzetu popote pale nchini, makundi mbalimbali ya kijamii (wakulima, wafugaji, wavuvi, wamachinga, wasanii, n.k), zikiwemo taasisi za dini kwamba watu wachache kuzungumza kwa niaba ya makundi juu ya mambo yanayogusa maamuzi ya mtu binafsi.

Mwisho tunatoa wito kwa wanafunzi wenzetu wote kujitambua na kutumie muda wetu kwa mambo ya msingi na muhimu kwa ustawi wa Nchi yetu. Na kuonesha jinsi wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma walivyokasilishwa na jambo hili, Tamko hili limesainiwa na wanafunzi 7821 toka vyuo mbali mbali vya Dodoma.Majina ya sahihi za wanafunzi zimeambatanishwa. Tusikubali kutumika na wanasiasa wa aina hii.

Asanteni

Mungu ibariki Tanzania,Mungu vibariki vyuo vikuu vya Dodoma.

Kwa niaba ya wawakilishi wa serikali za Wanafunzi Chuo cha Mipango,Chuo cha Madini, Chuo cha Hombolo,Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) na CBE.

DANIEL DANIEL -Rais wa Saint Jonh’s University

26/03/2015
 
Hawa hamna kitu halafu ndio wasomi watarajiwa mimi kuna kautafiti nilishakafanya siku nyingi kuna jambo la kushangaza na la kufurahisa analoweza kufanya mtu ambae hana elimu na likamshangaza hata profesa manake hii jamii huwq inajitahidi kutumia akili ya kuzaliwa na kuchanganya na maarifa lakini kuna msomi hawa wanaojiita wasomi wanaweza kufanya kitu chenye kb 1mpaka ukajiuliza huyu ni msomi kweliii ama alifoji? Ukweli una baki kuwa ukweli samaki mmoja akioza ni wote wameoza.
 
kumbe wanafunzi wa vyuo vya Dodoma ni vilaza namna hii. Tamko gani hili utadhani limeandikwa na mtoto wa darsa la tatu? ndio maana wanasiasa uchwara wanayatumia sana haya madent ya Dodoma
 
Hawa hamna kitu halafu ndio wasomi watarajiwa mimi kuna kautafiti nilishakafanya siku nyingi kuna jambo la kushangaza na la kufurahisa analoweza kufanya mtu ambae hana elimu na likamshangaza hata profesa manake hii jamii huwq inajitahidi kutumia akili ya kuzaliwa na kuchanganya na maarifa lakini kuna msomi hawa wanaojiita wasomi wanaweza kufanya kitu chenye kb 1mpaka ukajiuliza huyu ni msomi kweliii ama alifoji? Ukweli una baki kuwa ukweli samaki mmoja akioza ni wote wameoza.

Where s your point?? Au umekuja kukejeli tu??!!
 
Hivi St john ni chuo au kikundi cha wanafunzi??
 
Inasikitisha pale wasomi wanapokubali kununulika kama juice ya miwa. Zamani wakulima walilaumiwa kupewa kofia chumvi.du!
 
Hakika Mafuriko hayawezi kuzuiwa kwa Mikono ila pesa tu.
 
CC
l.OWASSA NA BASHE WAKE
2.NAPE Nnawiye hongera sana11
3. Rostam Aziz na Karamage upumbafu wenu utaiponza nchi yetu nyie mtasepa Pakistani sisi tutakimbilia wapi?
4.Philip Mangula mshauri mwenyeiti wako mchezo wake ndio mauti yetu
 
mimi kwakweli napata wakati mgumu kiasi fulani kuhusu watu wanaoenda kumshawishi Lowassa agombee urais, maana kila kundi likienda kesho yake wanaibuka wengine kupinga. walianza Masheikh wa Bagamoyo, kesho yake akaibuka sheikh mkuu wa bagamoyo akawakana na kudai hawatambui hao masheikh. Wakaja wanafunzi wa vyuo vya Dodoma, leo hii marais wa hivyo vyuo wameibuka na tamko kupinga. Pia ilikuwa hivyo hivyo kwa wachungaji wa makanisa ya kipentecoste. Swali hapa hao wanaojitokeza kumshawishi Lowassa huwa hawawasiliana na viongozi wao wa juu?
 
Mmefanya vizuri kuliweka wazi suala hili japo mmechelewa kidogo. Pengine mlikuwa mnajipanga kutoa jibu muafaka. Haingii akilini kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu wanafanya upuuzi kama huo.

Ya Masheikh tayari lipo bayana. Ni utapeli mtupu. La watu wa bodaboda wala halihitaji kuumiza kichwa sana. Kila timamu anajua usanii usiojificha. Tunasubiri majibu toka kwenye baraza la makanisa ya wapentekoste.

Ifike mahali Mheshimiwa Lowassa atambue kuwa watu wake wanamtumia kama kitega uchumi. Bila shaka anawawezesha lakini wanamfanyia kiini macho watafune hela zake.

Kama kweli lile suala la Masheikh wa Bagamoyo lililatibiwa na Prof. Kapuya, wasomi wenye hadhi hiyo watoe tamko kuhusu huyo mwenzao anayewadhalilisha. Heshima ya mtu kuitwa profesa inatoweka taratibu.
 
Where s your point?? Au umekuja kukejeli tu??!!

Ukweli utawaweka huru wanafunzi wa udom walikwenda full stop hicho ndicho mlichokifuata huko chuo dhambi mliyoifanya inawatafuna wewe kama kweli unajiita msomi hembu jiulize waliandamana wanafunzi wangapi? Na iweje mnapandamana kudai haki yenu ya msingi huwa hamfiki hatau kilomita moja mnapigwa mabomu na wengine wanapoteza hata uhai je mliandamanaje na mkapewa ulinzi bila mabomu mpaka mkamfikia huyo lowasa kama hapo hakuna mchezo mchafu mnaojua msituone sisi wananchi wa kawaida na mazuzu sana mmelikoroga na mlinywe.
 
wasomi wazima mnakubali kutumika na mtu anayeutafuta urais kwa nguvu,mbona hatuwaon mkiandamana kudai haki ya kupatiwa mikopo ya elimu ya juu?
 
Lowasa bhana kweli wamasai wana vituko ndio maana unamkuta anauza dawa ukimuuliza dawa ya ukimwi atakuambia anayo mpaka ya kukuza ume kwahiyo lowasa kaiga uongo wa wamasai wezake
 
Nyie ndio mnaotumiwa na Nepi mje kuupotosha umma wa watz sio,kw hilo mmechelewa sana mnakumbuka shuka tyr kumekucha,watz ujumbe umeshafika kwao kwamba Makundi mbalmbali yana muunga mkono ktk mbio zake za kuwani urais tofauti na mtu yyte kwa sasa na El ndio tumaini la watz wengi,hizo propaganda zenu zimechelewa mno yan labda mngeanza kabla makundi kufika kwa EL huenda mngefanikiwa kuturubun huo ujingA wenu,Lowassa ndo habar ya mjin aisee bnafsi cjaona mbadala wake labda ww mleta mada nan unaona anacfa za kutuongoza zaidi ya EL
 
Back
Top Bottom