Tamko Rasmi la Wanafunzi wa Vyuo vya Dodoma

Tamko Rasmi la Wanafunzi wa Vyuo vya Dodoma

TAMKO LA UONGOZI WA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU DODOMA KULAANI KUHUSISHWA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA DODOMA NA KUMUOMBA MH. LOWASA KUGOMBEA URAIS.

Ndugu Waandishi wa habari, Tunapenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu kwa kufika katika eneo hili kutusikiliza.Mbele yenu ni viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka Vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo mkoani Dodoma.Ndugu waandishi wa habari,si kawaida na wala mazoea kwa marais na viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo tofauti kukutana kwa pamoja na kuzungumza na nyie wanahabari kama inavyotokea hii leo.

Ndugu wanahabari,siku ya Jumapili ya tarehe 22 mwezi huu wa 3,kundi la watu waliojitambulisha kama ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma walijikusanya nyumbani kwa mh; Lowasa na kutoa matamko mbalimbali ikiwa pamoja na kuutangazia uma wa watanzania kuwa sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma tunamuunga mkono na tunahitaji Lowasa awe rais wetu sambamba kumchangia pesa.

Ndugu wanahabari,Tunapenda kukanusha kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma kwa ujumla wetu hatukuhusika na jambo lile na kama viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya mkoa huu wa Dodoma,Tunapinga na kulaani kitendo cha watu wachache kwenda kutuingiza sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma katika jambo ambalo halituhusu na wala si lililotuleta hapa Dodoma.

Sisi kama wasomi ambao jamii inatutegemea kama kioo hatuwezi kuandamana na kujikusanya kwenye nyumba ya kiongozi na kumuomba agambee urais, wakati tunajua fika sisi hatuhusiki na uteuzi wa wagombea ndani ya taasisi yao.Kilichofanyika ni kuudanganya uma wa watanzania na taasiasi yake kupitia kivuli cha vijana wachache kutoka vyuo vya hapa Dodoma,waliolipwa pesa ili waweze kuwa kava la tukio lile.

Ndugu wanahabari,Mkoa wa Dodoma unavyuo vikuu visivyopungua 8,Na jumla ya wanafunzi wote tunaosoma katika vyuo vya Dodoma ni zaidi ya wanafunzi 35,000.Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) pekee yake kinawanafunzi wasiopungua 22,000.Idadi ya watu waliojikusanya nyumbani kwa Mh: Lowasa siku ya tarehe 22-03-2015 haizidi watu 230 wakiwemo Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi, kama vyombo vya habari vilivyoripoti.

Ukiwatoa Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi waliotoka mikoa mbalimbali,idadi ya wanafunzi waliokuwepo kwenye tukio lile hawazidi 150.Idadi hii ni sawa na asilimia 0.4 ya wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma.Ndugu wanahabari,kwa akili ya kawaida kabisa asilimia 0.4 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ndio waliokuwa pale.Tunashangazwa na dhambi tusiyoitenda tunayobebeshwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao kwa sasa tupo bize na msimu mpya ya masomo wenye changamoto mbalimbali.

Ndugu wanahabari,sisi kama vijana wasomi na watu tunaotegemewa na jamii zetu tutakusanyika katika kujadili na kuchambua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii yetu na sio kukusanyika kwa ajili ya mwanasiasa ambaye sifa zake na uhadilifu wake unatiliwa shaka katika jamii.Tunaomba mlijulishe Taifa, kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma hatujahusika na tukio lile isipokuwa wanafunzi wachache walitumika kwa kupewa pesa na wahusika wa tukio lile.Tunataka Taifa lijue hatupo tayari kutumia elimu zetu kulitia upofu taifa letu.

Waambieni mama zetu na baba zetu huku vijijini kwetu kuwa tumekuja kutafuta elimu ili ituwezeshe kuwakomboa wao na sio kutumika na Wanasiasa kwa malengo yao.Tunatambua haki ya mwanafunzi kuamua na kufanya shughuli za kisiasa nje ya maeneo ya vyuo, lakini hatukubaliani na wanafunzi wachache kuchafua na kuwapaka matope maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao hawajahusika na tukio lile.Hii sio haki na haikubaliki.

Vilevile tungependa kutumia fursa hii kuwaasa wanafunzi wenzetu popote pale nchini, makundi mbalimbali ya kijamii (wakulima, wafugaji, wavuvi, wamachinga, wasanii, n.k), zikiwemo taasisi za dini kwamba watu wachache kuzungumza kwa niaba ya makundi juu ya mambo yanayogusa maamuzi ya mtu binafsi.

Mwisho tunatoa wito kwa wanafunzi wenzetu wote kujitambua na kutumie muda wetu kwa mambo ya msingi na muhimu kwa ustawi wa Nchi yetu. Na kuonesha jinsi wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma walivyokasilishwa na jambo hili, Tamko hili limesainiwa na wanafunzi 7821 toka vyuo mbali mbali vya Dodoma.Majina ya sahihi za wanafunzi zimeambatanishwa. Tusikubali kutumika na wanasiasa wa aina hii.

Asanteni

Mungu ibariki Tanzania,Mungu vibariki vyuo vikuu vya Dodoma.

Kwa niaba ya wawakilishi wa serikali za Wanafunzi Chuo cha Mipango,Chuo cha Madini, Chuo cha Hombolo,Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) na CBE.

DANIEL DANIEL -Rais wa Saint Jonh’s University

26/03/2015

Yetu macho, time will tell where serious people we'll make HISTORY & HARD DECISION.
Siko Tayari KABURI LANGU LIJE KUCHAPWA NA WANANGU,WAJUKUU,VITUKUU,VILEMBWE,JAMII n.k.
 
Umesahau waendesha bodaboda sijui miangapi kutoka Mbeya Mbarali. Leo uongozi wa Mbarali umekanusha na kuseam huo nimpango wamtu mmoja aliwashawishi waendesha bodaboda 7 kutoka kule. Waliofika dodoma ni 50 na haijulikani wengine aliwapata wapi. Na isitoshe WANAOSEMWA ETI NI WAENDESHA bodaboda, kunawengine hata kuendesha hizo pikipiki hawajui.

Kama vile mashehe n.k.

Ndugu zangu, Watanzania, Tusirudie makosa yakurubuniwa na makeke ya kisanii kama ya kikwete. Lowasa na kikwete ni mtu mmoja.

Ninaomba Ccm wamchukulie hatua za kinidhamu Lowasa kwa sababu anadhalilisha Utanzania. Ni dhalilil kwa taifa kuwa na mtu wa umri ule, aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa kabisa serikalini ingawa alifukuzwa kwa wizi na udanganyifu, halafu anatumia udanganyifu huu kuvunja sheria ili kulipotosha taifa.

Lowasa ni adui mkubwa sana wa maendeleo na haki za watanzania.

KWA SASA WATANZANIA TUNA LENGO MOJA TU. KUKOMBOA TAIFA. HATUTAKI KUMWONA WALA KUSIKIA FISADI, MWONGO NA MHUNI KAMA LOWASA AKITUPOTEZEA MUDA. Ccm mchagueni kusimamia chama chenu lakini serikali ya Tanzania haiwezi kuwa chini ya Lowasa.


Team Lowasa, ninawaomba ushauri wenu uishie ccm, na si kutuvuruga hapa na uhuni wenu wa kijinga hapa. Kwa taarifa, CCM HAINA NAFASI YA KUONGOZA NCHI HII TENA. NA MBINU MNAZOTUMIA KAMA ZA KUKODISHA WAHUNI NA KUWAVALISHA MABANGO KWENDA KUSHAWISHI WATU WENYE UCHU NA UONGOZI TAYARI, NDILO KABURI LA CHAMA CHENU.

NIMESEMA NA IMEKUWA.

hafai kabisa huyu mtu kuwa rais wa tano wa JMT
 
Nyie ndio mnaotumiwa na Nepi mje kuupotosha umma wa watz sio,kw hilo mmechelewa sana mnakumbuka shuka tyr kumekucha,watz ujumbe umeshafika kwao kwamba Makundi mbalmbali yana muunga mkono ktk mbio zake za kuwani urais tofauti na mtu yyte kwa sasa na El ndio tumaini la watz wengi,hizo propaganda zenu zimechelewa mno yan labda mngeanza kabla makundi kufika kwa EL huenda mngefanikiwa kuturubun huo ujingA wenu,Lowassa ndo habar ya mjin aisee bnafsi cjaona mbadala wake labda ww mleta mada nan unaona anacfa za kutuongoza zaidi ya EL

Labda unamuunga mkono wewe na wapumbavu wenzio mnaoendekeza njaa,pumbavu zenu nyie
 
Palipo masilahi usiogope kuharibu utatubu dhambi taaratibu! Kiujumla mi ata siwezi walaumu sana wanafunzi na viongozi wa vyuo vya Dodoma kwa kile kilichofanywa na wanafunzi njaa makada wa ccm wakitumia mwamvuli wa kuvivika vyuo vya dodoma kumuunga mkono Lowasa, bali tuwatazameni wahusika wakuu tusihukumu kwa misemo ya zamadi ambayo haina mashiko kwa sasa
Binafsi sio muumini sana wa msemo wa "together we stand" bali "alone a strong person has to stand" hivyo mzigo huu uwaangukikie mashushu waliotumika bila kuangalia ubovu wa hotuba ilotolewa na jumuiya ya viongozi wa vyuo vya dodoma
 
Wewe ni mwanafunzi wa vyooo vikuuu vya stand za mabasi kwani wale walionyeshwa kwenye tv zote ni wakimbizi acha ujinga nenda kandike nsha unajaza ushudu ndani ya blogs eti rais nyambafu kwenda mwende halafu mkatae au na nape kaleta fungu mkane. Hamkwenda nenda kakane itv
 
Nyie ndio mnaotumiwa na Nepi mje kuupotosha umma wa watz sio,kw hilo mmechelewa sana mnakumbuka shuka tyr kumekucha,watz ujumbe umeshafika kwao kwamba Makundi mbalmbali yana muunga mkono ktk mbio zake za kuwani urais tofauti na mtu yyte kwa sasa na El ndio tumaini la watz wengi,hizo propaganda zenu zimechelewa mno yan labda mngeanza kabla makundi kufika kwa EL huenda mngefanikiwa kuturubun huo ujingA wenu,Lowassa ndo habar ya mjin aisee bnafsi cjaona mbadala wake labda ww mleta mada nan unaona anacfa za kutuongoza zaidi ya EL

Mi nakuona wewe unaweza kuliko hata lowassa na wewe ndo tegemeo la watanzania wote sijaona mtanzania wenye weledi kama wewe
Yani mimi nakukubali sana kuliko hata lowassa kwasababu hauna kashfa yoyote
Wewe ndo tegemeo la watanzania wala sio lowassa
 
Siku chache baada ya mbunge wa monduli kudai kuwa amechangiwa fedha na wanafunzi wa vyuo vikuu vya dodoma na kumshawishi agombee urais wanafunzi wa vyuo hivyo wa mkoa wa dodoma kikiwemo UDOM wameibuka na kupinga madai hayo.

wanafunzi hao wamedai kuwa hawajawahi kukaa hata siku moja na kuchanga fedha hatimaye kwenda kwa Lowasa kumuomba agombee urais wakizungumza kwa uchungu wanafunzi hao wamesema Lowasa ni muongo anayetumia pesa kuhadaa jamii.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    545.7 KB · Views: 313
Ukizoea ulagahi kila kitu utafanya kilaghai tu Lowasa amezidi kwa ulaghai usiokuwa na na maana.
 
Soma kwanza magazeti ya leo ndiyo ubishe.
 
Magazeti ya siku hizi ni kama toilet paper tu..
 
Na hilo Gazeti nina uhakika kama siyo Raia Tanzania basi Jambo leo au Uhuru
 
Back
Top Bottom