Oh yah, kazi kweli kweli. Mwaka huu naona haponi mtu!!!
NI MPASUKO DODOMA; Wapiganaji hawako tayari kupatana!!
NI MPASUKO DODOMA; Wapiganaji hawako tayari kupatana!!
Tatizo moja la siasa za Tanzania yetu, pengine tofauti na nchi zingine hapa Afrika, ni kukosa watu wenye ujasiri wa kisiasa, ambao wapo tayari kuhesabiwa, sio kwa maneno yao bali kwa matendo yao. Pengine hii inachangiwa kwa kiasi fulani na ukweli kwamba ni wanasiasa wachache sana wanaoweza kusurvive bila mkono wa serikali. Wanasiasa wetu wengi wanaishi ama kwa kuitegemea serikali moja kwa moja, kwa kuajiriwa, kwa pensheni wanazopata au kwa kuwa wafanyabishara wakifanya biashara ambazo ufanisi wake kwa kiasi kikubwa unategemea short cut kama vile kukwepa kodi, etc., kiasi kwamba serikali ikiamua kuziba mianya sawasawa hawezi kukatiza siku mbili.
Ni kwa sababu hii wengine hatukashangazwa kwa waanzilishi wa CCJ kujificha wakipima upepo, na ndio maana na leo wanatoa nyaraka kwa kujificha. Kama unaamini unachokiongea kwa nini ufiche jina lako? Woga ni adui mkubwa sana wa maendeleo ya kisiasa katika nchi hii.
NI MPASUKO DODOMA; Wapiganaji hawako tayari kupatana!!
kesho.. kitawiva.. subirini tu!
kaka tatizo watu hawajui ccm kuwa ni wakoloni weusiKitila Mkumbo,
..nakumbuka 1995 kulikuwa na mazingira kama haya ya Richmond. wakati ule kulikuwa na kashfa za Chavda na Loliondo.
..sasa hivi Mwinyi na Kinanan ambao ni watuhumiwa wa kashfa za 1995, wamepewa jukumu la kuchunguza migongano kati ya mafisadi na "wapiganaji" ndani ya CCM.
..Mwinyi ndiye Raisi aliyemfutia kifungo rubani wa ATC aliyekamatwa airport akitorosha dhahabu. Kinana naye alikuwa mstari wa mbele katika ugawaji/ukodishaji wa mbuga ya Loliondo.
..sijui kwanini baadhi yetu wana matumaini na CCM kwa kweli?
NI MPASUKO DODOMA; Wapiganaji hawako tayari kupatana!!
Greetings dear friends; We received this document late last night from very reliable and impeccable sources. M has given the greenlight to release it as it is.