Tambiko Ofisini. Tutafika kweli??

CtVKiLaZA

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
301
37
Katika hali isiyo ya kawaida leo asubuhi nimefika Ofisini kwangu. Si unajua tena mambo ya kujiajiri. Nina ka salon kangu na mtaani kuna salon mbili nyingine. Lakini kufika mlangoni nikakuta kuna kichwa cha kuku, kitamba chekundu na damu. Pembeni kidogo nikaona kuna shimo limechibwa ndani kukiwa na kuku mweupe. Mi sio mtu ya kuamini Mambo ya kishirikina. Nimefanya usafi na kuendelea na biashara yangu.
Lakini kwa nini tunafanyiana hivi. Tunarudisha nyuma.
 
Na wewe kama unaamini hayo mambo basi ni kweli utarudishwa nyuma.
 
Pole sana mkuu watu kama hao hata kwetu wapo! Dumu kwenye maombi tu. Ila sijakuelewa hapo uliposema kuwa " Mi sio mtu ya kuamini Mambo ya kishirikina. Nimefanya usafi na kuendelea na biashara yangu.
Lakini kwa nini tunafanyiana hivi. Tunarudisha nyuma"
 
sisi ndio waafrica nakupa siku tatu lazima ufunge saluni yako Lol,mkuu huamini ushirikina,je hukustuka ulipoona hivyo vimbwanga? Nalog off
 
Hiyo ni mbinu tu ya kukudhoofisha,umefanya usafi na kuanza kazi hiyo ni hatua nzuri sasa fanya kazi kwa bidii zaidi hata ukikuta ng'ombe kachinjwa mlangoni we fanya usafi na kupiga kazi watachoka wenyewe.
 
asante sana. Maneno yako yamenifariji
 
Katika hali isiyo ya kawaida leo asubuhi nimefika Ofisini kwangu. Si unajua tena mambo ya kujiajiri. Nina ka salon kangu na mtaani kuna salon mbili nyingine. Lakini kufika mlangoni nikakuta kuna kichwa cha kuku, kitamba chekundu na damu. Pembeni kidogo nikaona kuna shimo limechibwa ndani kukiwa na kuku mweupe. Mi sio mtu ya kuamini Mambo ya kishirikina. Nimefanya usafi na kuendelea na biashara yangu.
Lakini kwa nini tunafanyiana hivi. Tunarudisha nyuma.

basi kama umefanya usafi we endelea kula vichwa ama ida..
 
ukiona vipi tafuta tu eneo lingine la biashara
haya mambo wakati mwingine yanaishia pabaya.
 
Pole sana mkuu watu kama hao hata kwetu wapo! Dumu kwenye maombi tu. Ila sijakuelewa hapo uliposema kuwa " Mi sio mtu ya kuamini Mambo ya kishirikina. Nimefanya usafi na kuendelea na biashara yangu.
Lakini kwa nini tunafanyiana hivi. Tunarudisha nyuma"

ya kwa imani yangu siamini haya mambo kabsa. Nilipo sema kwa nini tunarudisha nyuma nilikuwa na maanisha kwa nini tusumbuane. Wakafanyie huko huko. Hapa inawapa hofu mpaka wateja wangu. Binadamu tumetofautiana uwezo wa kutambua.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom