Tambiko Ofisini. Tutafika kweli??

Katika hali isiyo ya kawaida leo asubuhi nimefika Ofisini kwangu. Si unajua tena mambo ya kujiajiri. Nina ka salon kangu na mtaani kuna salon mbili nyingine. Lakini kufika mlangoni nikakuta kuna kichwa cha kuku, kitamba chekundu na damu. Pembeni kidogo nikaona kuna shimo limechibwa ndani kukiwa na kuku mweupe. Mi sio mtu ya kuamini Mambo ya kishirikina. Nimefanya usafi na kuendelea na biashara yangu.
Lakini kwa nini tunafanyiana hivi. Tunarudisha nyuma.
Leo wamekuroga hao wachawi au kuna jirani yako anafanya kazi kam ya kwako nini? ndio maana kafanya Tambiko mlangoni kwako uwe muangalifu sana.

wanapima imani yako,
la sivyo kama umemdhulumu mtu jitahidi muyamalize.
huenda amemkopa Mtu sas hataki kulipa huyo jamaa kaamuwa kumroga au ana mpenzi wa kike ndie aliyefanya dawahiyo jihadhari sana mkuu pole kwahayo yaliyokukuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom