Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Mkurugenzi wa TAKUKURU na wafanyakazi walio chini yake wanalipwa fedha nyingi kutoka kwenye kodi za wananchi.
Pamoja na malipo mazuri hakuna kazi yoyote ya msaada wanayotoa kwa serikali na jamii kwa ujumla. Kama wangekuwa active hizi taarifa za madhila ya wafanyabiashara wangekuwa wanazo na kuchukua hatua, lakini hakuna kesi yoyote walioripoti kuipokea kuhusu changamoto hizi. Je, kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na hii taasisi?
Lakini pia wanaolalamikiwa ndio waliomlea boss wa sasa wa TAKUKURU; Je, ilikuwa sahihi kwa Mhe. Rais kuteua Mkuu wa TAKUKURU kutoka kwenye taasisi inayoongoza kwa rushwa (polisi)?
Hata kama angekuwa muadilifu kiasi gani, anaendaje kuwakamata watendaji wa bosi wake? IGP ni senior kwa Kamishna wa Polisi anayeongoza TAKUKURU, je, anawezaje kumkwepa IGP na kwenye kukamata vijana wake? Najiuliza maswali haya nikitambua kwamba mfumo wetu wa uteuzi unaweza kumtengua na kumrejesha polisi, atatazamana vipi na ndugu zake?
Muundo huu wa TAKUKURU utaendelea kuwatesa viongozi wakuu nakuwalazimisha wawe maafisa TAKUKURU huku wenye dhamana wakiwa wanalipwa salary bila tija.