TAKUKURU isiongozwe na Askari. Inahitaji katiba ya Dkt. Hosea kuifufua

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imekabidhiwa mikononi mwa wanajeshi na Askari. Kazi hii aliifanya Magufuli kwa lengo la kumwezesha kutoa amri ya kutimiza malengo yake .

Baada ya JPM bado aliteuliwa Afisa wa Polisi kuongoza taasisi hii. Madhara ya uteuzi ule ni kwamba taasisi imeacha misingi yake na sasa inasikiliza amri kutekeleza majukumu yao. Ni taasisi inayosubiri mwanasiasa aseme kamata na siyo taasisi yakujieneza kwa jamii kubaini wizi na kuchukua hatua.

TAKUKURU inapaswa kuwa na mifumo mizuri ya kubaini viashiria vya rushwa kwenye taasisi na kisha kukutana na mkuu wa taasisi husika kumwelekeza visharia na risks zilizopo anazopaswa kuzifanyia kazi.

TAKUKURU haipaswi kukamata inapaswa kuita mtuhumiwa kwa mahojiano. Haipaswi taasisi yakisubiri wizi utokee bali iwe taasisi yakuona wizi kabla hakutendeka na kudhibiti isitokee.

Kwa ufupi TAKUKURU ilipaswa kuangaika na mapapa siyo dagaa.....dagaa walipaswa kudhibitiwa kwa kuwabaini kabla ya kuiba ili wasifanikiwe kuiba.

Nashauri mamlaka za uteuzi ziondoe TAKUKURU polisi na kuirudisha kwa RAIA wenye integrity. Haiwezekani watumishi wa TAKUKURU wafanye kazi ndani kwao wanapofikia nafasi ya ukurugenzi mkuu waletewe mtu kutoka nje ya taasisi na anayeletwa akapata uungwaji mkono. Tukubali kwamba hizi taasisi wapo watu wamesota miaka na miaka wakifanya kazi wafikie nafasi ya juu, tuwape nafasi badala ya kuwaletea watu kutoka nje.

Rushwa imekithiri kwa sababu wanaopambana na rushwa leo walikulia kwenye rushwa. Kila wakitaka kuchukua hatua wanakumbuka maovu yao.
 
Ungejua Siasa Imeingilia Utendaji, Hapo Utailaumu PCCB Ila Wenye Maamuzi Ni Hawa Tu
Rais Wa JMT
Makamu Wa Rais Wa JMT
Waziri Mkuu Wa JMT
 
Takukuru sio raia wa kawaida; wana mafunzo ya kijeshi na ndio maana wanaongozwa na Mwanajeshi/askari.

Saivi kozi yao wanapigia Chuo cha Taaluma ya polisi(MOSHI)kwahiyo haiwezekani ikawa taasisi lelemama lazima iongozwe kijeshi.
 
Takukuru sio raia wa kawaida;wana mafunzo ya kijeshi na ndio maana wanaongozwa na Mwanajeshi/askari.

Saivi kozi yao wanapigia Chuo cha Taaluma ya polisi(MOSHI)kwahiyo haiwezekani ikawa taasisi lelemama lazima iongozwe kijeshi.
Mafunzo ni tofauti na utendaji, unaweza ukasoma polisi usiwe polisi. Siyo watu wote waliokuwa askari wanapokwenda kufanya kazi benki wanafanya kiaskari.....TAKUKURU INATAKIWA KUWEKEZA KWENYE KUFICHUA MBINU ZA UBADHIRIFU KABLA YA UBADHIRIFU.

Mfano kwenye halmashauri wanapaswa kuvujisha taarifa za wizi kabla hata watendaji awajaanza kula pesa za miradi.

Wakijikita kukamata wanapoteza focus coz kila watakayetaka kumkamata watakuta ana godfather juu. Wawekeze kufichua mbinu siyo wizi.....
 
Kuzuia siyo kukamata wala rushwa

Kupambana siyo kukamata wala rushwa.

Wakizuia hata CAG atapumua na wakubwa watajirekebisha. T

Narudia tena TAKUKURU ikabidhiwe wataalam wa Risks na Mitigation siyo wakamataji
 
Takukuru sio raia wa kawaida;wana mafunzo ya kijeshi na ndio maana wanaongozwa na Mwanajeshi/askari.

Saivi kozi yao wanapigia Chuo cha Taaluma ya polisi(MOSHI)kwahiyo haiwezekani ikawa taasisi lelemama lazima iongozwe kijeshi.
Uwongo. Tuko nao huku mtaani na CV zao tunazijua. Lini walipata hayo mafunzo ya kijeshi?
 
Kuzuia siyo kukamata wala rushwa

Kupambana siyo kukamata wala rushwa.

Wakizuia hata CAG atapumua na wakubwa watajirekebisha. T

Narudia tena TAKUKURU ikabidhiwe wataalam wa Risks na Mitigation siyo wakamataji
Zamani kitengo chao Cha operesheni kilikua moto sana yaaan ilikua ushangai wanawategeshea wapenda rushwa zile hela zao za moto maofisini, matrafiki walikua waoga maana mda wowote wananaswa na wale jamaa, ilikua mabosi hawana upendeleo ule kisa ngono maana majamaa walikua siriaz. Cjui wamekumbwa na kitu gani!!!! Kuna ofisi Moja pale TRC wao bosi wao anakula ten percent ya per diem ya surbodinate ili akupange safari lkn TAKUKURU wapo kimya nshawai waandika umu lkn kimyaaaa
 
Takukuru sio raia wa kawaida;wana mafunzo ya kijeshi na ndio maana wanaongozwa na Mwanajeshi/askari.

Saivi kozi yao wanapigia Chuo cha Taaluma ya polisi(MOSHI)kwahiyo haiwezekani ikawa taasisi lelemama lazima iongozwe kijeshi.
Mkuu umemuelewa mleta hoja??
 
Zamani kitengo chao Cha operesheni kilikua moto sana yaaan ilikua ushangai wanawategeshea wapenda rushwa zile hela zao za moto maofisini...
Samahani hii zamani ipi? Hicho chombo toka kiundwe sijawahi kuachwa kuombwa rushwa napotaka uhudumu toka ofisi za umma.
 
Samahani hii zamani ipi? Hicho chombo toka kiundwe sijawahi kuachwa kuombwa rushwa napotaka uhudumu toka ofisi za umma.
Hakijawahi kua perfect toka kimeundwa, Yes. But ubutu wa sasa unazidi Kwa mbali ubutu wa zamani. Sasa kimezidi kua butu mno.
 
Rushwa nje nje nje! Hakuna idara isiyolamba rushwa!

Miradi Iko chini ya kiwango lkn wasimamiz wamevuta chao.
 
Back
Top Bottom