masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,172
Wizara ya Ardhi imeoza kwa rushwa. Sina uhakika kama Waziri Jerry Slaa ataziweza mbinu za ufisadi ndani ya Wizara ya Ardhi na Idara za Ardhi katika Halmashauri.
Sakata la plots 194 na 195 Rwegasore Mwanza inatufungua macho.
Nampongeza sana Waziri Mkuu Majaliwa kwa kulichunguza kwa undani swala la ufisadi wa viwanja tajwa, ufisadi uliotungwa na watu ndani ya serikali.
Kuna maafisa Ardhi wakishirikiana na viongizi wakubwa serikalini wamekuwa wakiwapora viwanja wananchi wa hali ya chini mchana kweupe.
Mbinu inayotumika sasa hivi ni kushirikisha Mahakama au TAKUKURU.
Mbinu inayotumika iko hivi:
Kama kuna kiongozi au mtu mwenye pesa ndefu anataka kiwanja maeneo fulani, sema Mbezi, Ununio au Bahari Beach, au hata Mapinga na sehemu prime, inaanzishwa kesi au mashitaka yasiyo na mbele wala nyuma juu ya kiwanja husika.
Nia inakuwa kupora kiwanja.
Mtu anasitukia anatakiwa Mahakamani au kwenda TAKUKURU kujieleza.
Hao maafisa Ardhi huwa wamempanga mtu kulianzisha na kuandika malalamiko feki.
Kama una uzembe hukufuatilia kiwanja chako na kulipia Land Rent, wanakusubiri hata mwaka na mwisho unaletewa barua kuondoka kwenye kiwanja hata kama Hati ulikuwa nayo.
Wenyewe wanasema imekuwa revoked.
Mimi binafsi lilinitokea hili, ila nawashukuru TAKUKURU waliushitukia mchezo, baada ya misuguano ya mwaka mzima, kuwa wanatumiwa na hao wajanja kunyang'anya viwanja vya wananchi wa hali ya chini wenye viwanja prime.
Namfahamu mtu Bahari Beach aliyeondolewa mchana kweupe kwa mbinu hiyo na kwa vile wanaonyang'anya ni wenye vyeo na pesa kubwa, mwananchi anabaki kulia.
Waziri Jerry Slaa namshauri awekeke Help Desk ofisi za Ardhi Mkoa ili zishughulikiwe kwa njia inayofaa.