A
Anonymous
Guest
Kuna jambo limetokea linahusu rushwa, sijajua kwa sababu zipi halitangaziwi au halitajwi hadharani, inawezekana kuna bado mamlaka zipo kazini au inawezekana pia kuna vitu havipo sawa.
Hapa kwetu Mkoani Songwe kuna jambo limetokea likimhusisha Kaimu Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe ambaye anajulikana kwa Eng. Suleiman Bishanga.
Inasemekana wiki moja au mbili zilizopita maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walizikamata gari ambazo zilikwepa kupita kwenye Mzani (Mzani wa Mpemba) kwa ruhusa ya Eng. Bishanga.
Baada ya TAKUKURU kuingilia ‘Mchongo’ huo, wamezikamata gari nne, mbili nyeupe na mbili za njano ambazo mpaka leo tarehe 16 mwezi wa nane, 2023 zimepaki kwenye yard yao.
Inadaiwa kampuni inayomiliki magari hayo (mali ya Mchina) ilikuwa inatoa fungu (zaidi ya shilingi milioni 4) kwa Meneja ili aruhusu malori yake yapite bila kupimwa kila wanapopitisha magari hayo ambayo huwa yanabeba lami.
Hata hivyo, TAKUKURU walivyokamata magari, yakapimwa na kukutwa na uzito mkubwa sana kiasi kwamba kwa gari zote nne jumla ya faini iliyotozwa ni zaidi ya Shilingi milioni 90.
Hoja yangu ni kuwa mbona kuna ukimya kuhusu hiki kilichotokea, si TAKUKURU wala Serikali ya Mkoa ambayo imejitokeza kueleza micheo michafu iliyokuwa inaendelea.