Tahadhari tusiyoizingatia

Tahadhari tusiyoizingatia

Ni alfajiri nyingine tena kunapambazuka....
Kwanza kwa huzuni kubwa naomba nitoe pole nyingi kwa ndugu na jamaa wa mama aliyeuliwa kikatili usiku wa kuamkia jana kwenye uwanja wa transforma chalinze! Mpaka juzi saa tano usiku alikuwa hai nyumbani kwake (si mbali sana na eneo alipouliwa) lakini asubuhi ya jana alikutwa uwanjani hapo akiwa kafa kifo cha kikatili na mateso makubwa. .mwili unaonyesha alibakwa na watu zaidi ya wawili kuvunjwa mikono kunyongwa na hatimaye kutobolewa macho RIP [emoji144] [emoji24] [emoji25]
===============================
Tumejifunza katika masomo yaliyotangulia kuhusu mlango wa sita/mlango wa machale, mara nyingi ikija kama sauti ya kutoa tahadhari au moyo kupasua au kukosa pumzi kila ukikumbuka jambo husika! Ukiwa na fikra yakinifu lazima ubadili mawazo

Sasa huu mlango wa sita hutokea ukaunganisha familia kwa namna ya ajabu kabisa kupitia kwa mama watoto na hata baba mwenyewe
Ninapoandika haya muda huu kuna watu wako kwenye vituo mbalimbali vya usafiri wa majini angani na nchi kavu na wengine wanajiandaa kwenda huko
Ni katika ya watu hao kuna ambao kati yao

= usiku mzima alikuwa akiiwaza hii safari moyo unapiga paa/una shikamooo na kukosa amani
= mke au mume anakosa amani na kukushauri uahirishe safari na ukimuuliza kwanini anakwambia hajui
= mtoto/watoto wanaota ndoto za ajabu na kukusihi usisafiri au kama ni wadogo kulia bila sababu kila unapokaribia kutoka (kuna kule kumlilia mzazi lakini siku hiyo inakuwa tofauti )

Haya ni matukio ambayo kwa namna fulani yanakunyima amani moyoni..unajaribu kujiuliza bila jibu kuna kuna nini leo
Kuna kitu kinaitwa willpower, nguvu ya kutenda bila kujifahamu (ipo willpower ya kuamua kutenda pia, njia zote na ishara zote za kukutahadharisha kuwa uendako sio salama, na kama hiyo nguvu imeamua kukuepusha na janga linalokunyemelea yatatokea haya

= utasahau kufungasha kitu muhimu kitakachokulazimu urudi nyumbani kukichukua
= utaachwa na gari au itatokea dharura yoyote ya kukuchelewesha kufika kituo husika
= kwa sababu nyingine zozote zile utakosa kusafiri kwa kuachwa na chombo husika iwe ndege boat/meli au gari
Utakasirika sana na hata kugombana na aliyesababisha hiyo hali kama si mtu wa kutafakari. ..... ni mpaka pale utakapokuja kupata taarifa za kutisha kuhusu ajali ya chombo ulichotaka kusafiri nacho ndio litakupambazukia kuwa kwanini kulikuwa na mikwamo kiasi kile
9648c0451a37950a2bbe89da171d3ecd.jpg

Usipoisikiliza ile sauti! Usipotafakari ile mikwamo na ukalazimisha kwa kupingana na ile nguvu ya ndani basi unaenda kukutana na mustakabali wako
Haya mambo yapo na shuhuda ni nyingi mno...sikiliza waliokoka kusafiri na Mv Bukoba nk . utapata ushuhuda wa ajabu kabisa

Na hii si lazima iwe safari ya mbali kuna baadhi yetu mwisho wao waliuona kabisa . siku moja kabla unakuwa ni mtu wa mawazo na kukosa furaha bila kujua sababu ninini...ni mpaka litimie la kutimia ndio watu wataanza kusimulia

Ni muhimu sana kusikiliza sauti zinenazo ndani yetu zina ujumbe gani ...sauti ya ndani ni jicho la kiroho linaona mbele ya muda mavune yaliyokuzonga ndio yanazuia tu kukupa clear msg ya kile kinachotaka kukutokea... .. kabla ya kuchukua uamuzi wowote sikiliza sauti yako ya ndani..utaokoka na mengi
Ni kweli mkuu hunitokea hata mimi lakini baadhi ya ishara zangu zinapotokea mwilini mwangu na nikajua jambo linakuja gumu ni vipi naweza zuia hyo hali au hatari ijayo isinitokee?
 
Ni kweli mkuu hunitokea hata mimi lakini baadhi ya ishara zangu zinapotokea mwilini mwangu na nikajua jambo linakuja gumu ni vipi naweza zuia hyo hali au hatari ijayo isinitokee?
Mara nyingi kuna sauti mbili zinaongea nawe kuhusu jambo hilo hilo moja...mazingira uliyonayo kwa wakati husika hukulazimisha kutii sauti mojawapo
 
Siyo kila kitu ni siasa mkuu. Siamini kama CCM ni waovu kiasi hiki mpaka wachome bweni la wasichana kisa eti wasingiziwe wapinzani. Kuna conspiracy theories zingine huwa nakubaliana nazo lakini hii ya kwako hapana.

Kuna makala ndefu ilitoka kwenye gazeti ikihusisha tukio hili na mambo ya mauzauza na kwamba eti mabinti wale waliendelea kuonekana wakiwa wanalia. Shule ilibidi ifungwe tena hata baada ya kufunguliwa kutokana na mauzauza hayo.

Ukifunikwa sana na chuki za kisiasa kila kitu kwako kinakuwa ni siasa. Hata ukijamba utasingizia chama kingine kimekutega. Tuache urazini ujipambanue!
Inawezekana chama sio katili lakini wanachama wake ni katili na waovu rejea yaliyotokea zanzibar wakati wa mkapa halafu urudi tena!
 
Lakini hili swala nadhani liko na sura mbili zenye kuchanganya.

Embu chukulia mfano-huu wa hili tukio hapa wahanga wanaonekana kuifuata hatari kwa nguvu zote.wanaowazuia wanazidiwa nguvu.wahanga wanaondoka wakiwa hawana hisia zozote, hii tunaita siku ya kufa nyani,,*.

Nyingine hii sasa ni wewe mhanga kukubariana na matakwa ya wengi wanaokuzuia, unaahirisha safari, kesho yake ukiwa unaondoka kama walivyotaka unakutwa na ya kukukuta.

Wahenga wanena kifo kina sumaku.
 
Hiyo sasa ni fate...! Kwamba imepangwa iwe hivyo na hakuna namna lazima itokee
 
Mshana nmefuatilia ile journey to the west anagalau nmeona mashart ya meditation nyama pombe havitakiwi kwa wale monks so meditation moja kwa moja ina link na Buddha? Je mbona monkey alieekti kule yy anaonekana kurelax Zaidi na ndio alikua akipambana na wale maadui yaan alikua na nguvu zaidi na kuelewa zile evil spirit pia kwel kuna mungu wa mvua n.k walivyoonesha kule? Au vingine ni fiction tu
 
Pia embu nielezee power of light and sound inavyofanya kazi ukishafika stage ya juu katika meditation
 
Mshana nmefuatilia ile journey to the west anagalau nmeona mashart ya meditation nyama pombe havitakiwi kwa wale monks so meditation moja kwa moja ina link na Buddha? Je mbona monkey alieekti kule yy anaonekana kurelax Zaidi na ndio alikua akipambana na wale maadui yaan alikua na nguvu zaidi na kuelewa zile evil spirit pia kwel kuna mungu wa mvua n.k walivyoonesha kule? Au vingine ni fiction tu
Ile sinema imekuwa exaggerated mno kuna mengi ya ukweli lakini pia kuna mengi zaidi ya uongo na kufikirika
 
Kitalaam wanasema mtu ukiwa na msongo wa mawazo ama kuufikirisha sana ubongo basi huchoka na hupelekea macho kucheza, na dawa yake ni kupumzika tu.
Sasa mbona mimi likicheza jicho kwa chini itatokea kugombana na mtu kwa kupigizana makelele?au ndo kujiaminisha hatimae inakua?
 
Huwa nikikaa nimetulia kuna matukio yanapita kama flash of lights, baada ya muda labda siku kadhaa tukio lile lile nililoliona linatokea kwa uhalisia na mazingira yale yale niliyoyaona before.

mshana jr hii inakuwa ni nini?
 
The concept of sixth sense seeing through time into future.... nafsi kupitia roho huweza kuona yajayo kupitia mlango wa sita japo nguvu yake ni ndogo kutokana na taratibu za maisha yetu lakini kuna wachache wana vipawa vya kuupa nguvu huo mlango
 
Inauma sana hasa issue ya wanafunzi. Imetimia miaka 22 sasa. Hao wanafunzi kwasasa wangekuwa na around miaka 36 - 40 hivi ambapo ingekuwa faida kubwa kwa familia zao na taifa kwa ujumla.

Hao wazazi wawili imeniuma pia nikakumbuka 2007 nilikuwa nasafiri kutoka Dar kwenda dom sasa hiyo safari dada yangu hakuitaka kabisa kwa siku hiyo tulichukua takriban saa 3 tukiongea yeye hataki niende na mimi nataka kwenda mpaka akashindwa nikaondoka.

Ile kufika Kibamba tu ikatokea ajali pale darajani ambapo tulinusurika wote hakuna safari iliyoendelea maana gari iluyokuwa mbele yetu ndio ilipata ajali na kuziba njia na sisi kwenda karibu na ile gari ambambo tungekuwa na speed walao 70 ingekuwa balaa zaidi. Narudi kwa sister anakwambia unapoondoka kwa kinyongo hutokea haya.

Sasa navuta hisia kwa hawa mabinti ambao waliondoka kwa kinyongo huku Mungu akiwakataza wasiende lakini bila kujua wazazi wakalazimisha kwa nia nzuri tu. Kiukweli kujinyonga kwao waliona hakuna namna ya kuishi tena bila wanao wawili tena their only.

R.I.P All
Jamani inasikitisha sana, mmoja kati ya walionusurika tulisomanaye Tabora Girls A level mwaka 1997-1999. sasa hivi ni mke na mama wa watoto
 
Siyo kila kitu ni siasa mkuu. Siamini kama CCM ni waovu kiasi hiki mpaka wachome bweni la wasichana kisa eti wasingiziwe wapinzani. Kuna conspiracy theories zingine huwa nakubaliana nazo lakini hii ya kwako hapana.

Kuna makala ndefu ilitoka kwenye gazeti ikihusisha tukio hili na mambo ya mauzauza na kwamba eti mabinti wale waliendelea kuonekana wakiwa wanalia. Shule ilibidi ifungwe tena hata baada ya kufunguliwa kutokana na mauzauza hayo.

Ukifunikwa sana na chuki za kisiasa kila kitu kwako kinakuwa ni siasa. Hata ukijamba utasingizia chama kingine kimekutega. Tuache urazini ujipambanue!

HAPO KWENYE RED ninakuja na maswali haya hapa chini
Vipi tukio la Soweto kwenye mkutano wa CHADEMA? ni chama gani kilihusika na tukio lile? vipi juu ya kesi ya Ugaidi ya Lwakatale ni chama gani kilihusika na kesi ile? vipi juu ya kuchinjwa kwa yule Mwenyekiti wa CDM Usarivar ni chama gani kilihusika?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom