Tahadhari: Catalunya Mwenge si salama

Tahadhari: Catalunya Mwenge si salama

Wakuu jana baada ya pilika za kazi nilikuwa na ratiba ya kukutana na rafiki zangu hapo Catalunya opposite na Calabash kwa mazungumzo maalum.Nilipofika Mlinzi wa pale (Masai) akanieleza sehemu ya kupaki. Ndani ya gari nikaacha begi lenye laptop na vitu vingine lakini kwa taadhari nilishaliweka chini ya siti ya nyuma.
Baada ya kushuka nikiwa na mwenzangu nikamuuliza yule Mlinzi kama ndio muhusika wa usalama akakubali nikamuomba aniangalizie usalama wa gari langu. Tukaenda kukaa sehemu ya nje tunapoweza kuona pia gari vizuri. Muda wote tulikuwa makini lakini maongezi yalivyozidi na kidogo kupoteza umakini ule kwa kama dakika 10 ghafla yule Masai akanifata kuwa brother twende gari yako inashida. Tulipogeuka kuangalia gari taa ilikuwa inawaka na mlango upo wazi! Tulipoenda tukakuta kioo cha mlango kilichokuwa upande wa pili kimevunjwa mlango umefunguliwa na begi limebebwa. Kwa muda mrefu eneo nililopaki zilikuwepo gari mbili tu tena zilizo mbali kidogo kiasi ambacho huwezi kutarajia mtu apate ujasiri wa kuchungulia hadi aone begi kubomoa, kufungua mlango na kuvuta begi upande wa pili.Mlinzi akatupa Maelezo ya kujichanganya ikiwemo kutaka kuruka baadhi ya vitu. Muhusika wa hapo Catalunya anasema hata yeye ameshaibiwa Catalunya ya mlimani city siku si nyingi. Mlinzi yupo polisi mabatini. Chukueni tahadhari wananchi wenzangu maana ni dhahiri walinzi wanashirikiana na wahalifu. Nimeamua kulifatilia kwa ukaribu tukio hili na nitawajulisha kila hatua muhimu.
Pole sana Mkuu na asante kwa kututahadhalisha!!!
 
Mm naacha madurisha waz na siachi kitu hata kimoja.....
 
Siku zote unapopaki hakikisha hakuna vitu vinavyompa mtu ushawishi weka hata katika buti kama gari ina buti.
Na ndivyo tunavyoshauriwa kila siku katika sehemu mbalimbali. Na hata hoteli, Lodge na Guest House wanaandika "kama una vitu vya thamani kabidhi reception"
 
Unapofunga mlango wa gari kuna ka uwazi kanabakia ktk mlango haka ka upenyo ni rahis mtu kuingiza kamba au uzi,mfano unachukua uzi mgumu mwembamba una ufunga kitanzi katikati halafu kile kitanzi kina penyezwa kwenye ile sehem ya mlango wa gari ambao wewe unaona umebana yani hata kidole hakipiti.huu uzi unaenda pitishwa mpaka usawa wa kile kitanzi kiingie ndani ya gari halafu wana bana lock ya gari kisha anavuta juu mlango unafunguka bila ubishi.
 
Usirogwe kuacha laptop au any valuable item for that matter ndani ya gari. Tena wengine unakuta amefika eneo husika then anatoa bag la laptop na kulihamishia chini ya seat...huku wataalamu wakiwa wanacheck mkanda mzima. Utapigwa tu.
 
Sasa ndo umetoka nayo job ukaona upitie maali je utaiacha wapi
Mimi huwa naweka chini ya kiti ila napo sio salama kabisa cha muhimu ni kuacha kuweka wazi vitu vitakavomvutia mwizi kuiba
 
Catalunya ina sehemu finyu ya parking.Usalama ni mbovu pale.Si mahali ninapopenda kutokana na matatizo ya parking.Nakushauri uweke alarm katika chombo chako cha moto.Pia vitu kama laptop weka ndani ya buti.
 
Mnaojifanya watoto wa mujini hayo yakiwapata ndo haki yenu. Mimi siiachi wala mfuko wowote kwenye gari. Nilipo navyo vipo. Mtanicheka sana lakini ka ni lazima niingie huko baa au hoteli ntaingia navyo. Anayeniona mshamba yeye ndo mshamba. Wanipige roba sawa lakini wasinipasulie kioo cha gari na mkoba uende. Hasara x 2. Pole sana
 
Kabla mtu hujaenda baa, kama una vitu kama laptop viweke chini ya kiti ama nenda navyo.
 
Asante kwa taarifa Mkuu!

Weka ndani hao wapuuzi, anza na Mlinzi. Hakikisha hatoki ndani mpaka PC ipatikane.

Mtu unatafuta mali kwa jasho lako harafu anakuja mjinga mjinga anaiba kizembezembe tuu. Eboooo!!!

= halafu
 
Ingia kitaa tangaza bingo laptop yako inarudi kabla hawajaiformat
 
Sasa ndo umetoka nayo job ukaona upitie maali je utaiacha wapi
this is 3rd worl country. hatubadiliiki over night, kama kuna wimbi la uhalifu wa design hiyo , inabidi uchukue tahadhari sana....jua ata kama una haraka zako..either kama unasehemu unapita acha pc ofisini uifwate kesho asubuhi, piga simu kwa eife aifwate njiani muonane, pita kwa jamaa ndugu au rafiki ambaye yupo maeneo ya karibu na unapoenda kula bata uiache...ila usipofanya ivyo...mijizi itakurudisha nyuma sana...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom