Wakuu jana baada ya pilika za kazi nilikuwa na ratiba ya kukutana na rafiki zangu hapo Catalunya opposite na Calabash kwa mazungumzo maalum.Nilipofika Mlinzi wa pale (Masai) akanieleza sehemu ya kupaki. Ndani ya gari nikaacha begi lenye laptop na vitu vingine lakini kwa taadhari nilishaliweka chini ya siti ya nyuma.
Baada ya kushuka nikiwa na mwenzangu nikamuuliza yule Mlinzi kama ndio muhusika wa usalama akakubali nikamuomba aniangalizie usalama wa gari langu. Tukaenda kukaa sehemu ya nje tunapoweza kuona pia gari vizuri. Muda wote tulikuwa makini lakini maongezi yalivyozidi na kidogo kupoteza umakini ule kwa kama dakika 10 ghafla yule Masai akanifata kuwa brother twende gari yako inashida.
Tulipogeuka kuangalia gari taa ilikuwa inawaka na mlango upo wazi! Tulipoenda tukakuta kioo cha mlango kilichokuwa upande wa pili kimevunjwa mlango umefunguliwa na begi limebebwa. Kwa muda mrefu eneo nililopaki zilikuwepo gari mbili tu tena zilizo mbali kidogo kiasi ambacho huwezi kutarajia mtu apate ujasiri wa kuchungulia hadi aone begi kubomoa, kufungua mlango na kuvuta begi upande wa pili.
Mlinzi akatupa Maelezo ya kujichanganya ikiwemo kutaka kuruka baadhi ya vitu. Muhusika wa hapo Catalunya anasema hata yeye ameshaibiwa Catalunya ya mlimani city siku si nyingi. Mlinzi yupo polisi mabatini.
Chukueni tahadhari wananchi wenzangu maana ni dhahiri walinzi wanashirikiana na wahalifu. Nimeamua kulifatilia kwa ukaribu tukio hili na nitawajulisha kila hatua muhimu.