Tahadhari: Catalunya Mwenge si salama

Tahadhari: Catalunya Mwenge si salama

Hao walinzi ndio zao ....wanachunguza gari lina nini wewe unajua ndio wanalinda. Siku hizi wanazo spray za kuvunjia kioo wanaiba na kuwapa wenzao wanasepa then ndio unashtuliwa. Wengine wakishachunguza vizuri wanawastua hao wapigaji then Mlinzi anakuwa anakufatilia kama utatoka awastue. Kuna baa bunju imekufa kabisa kwasababu ya ujinga huu ...
 
Wakuu jana baada ya pilika za kazi nilikuwa na ratiba ya kukutana na rafiki zangu hapo Catalunya opposite na Calabash kwa mazungumzo maalum.Nilipofika Mlinzi wa pale (Masai) akanieleza sehemu ya kupaki. Ndani ya gari nikaacha begi lenye laptop na vitu vingine lakini kwa taadhari nilishaliweka chini ya siti ya nyuma.
Baada ya kushuka nikiwa na mwenzangu nikamuuliza yule Mlinzi kama ndio muhusika wa usalama akakubali nikamuomba aniangalizie usalama wa gari langu. Tukaenda kukaa sehemu ya nje tunapoweza kuona pia gari vizuri. Muda wote tulikuwa makini lakini maongezi yalivyozidi na kidogo kupoteza umakini ule kwa kama dakika 10 ghafla yule Masai akanifata kuwa brother twende gari yako inashida. Tulipogeuka kuangalia gari taa ilikuwa inawaka na mlango upo wazi! Tulipoenda tukakuta kioo cha mlango kilichokuwa upande wa pili kimevunjwa mlango umefunguliwa na begi limebebwa. Kwa muda mrefu eneo nililopaki zilikuwepo gari mbili tu tena zilizo mbali kidogo kiasi ambacho huwezi kutarajia mtu apate ujasiri wa kuchungulia hadi aone begi kubomoa, kufungua mlango na kuvuta begi upande wa pili.Mlinzi akatupa Maelezo ya kujichanganya ikiwemo kutaka kuruka baadhi ya vitu. Muhusika wa hapo Catalunya anasema hata yeye ameshaibiwa Catalunya ya mlimani city siku si nyingi. Mlinzi yupo polisi mabatini. Chukueni tahadhari wananchi wenzangu maana ni dhahiri walinzi wanashirikiana na wahalifu. Nimeamua kulifatilia kwa ukaribu tukio hili na nitawajulisha kila hatua muhimu.
TRY THE FOLLOWING TIPS TO AVOID FORTHCOMING RISKS Watch out for car-jackers / assailants, especially when stopped at junctions, congestion points and red lights.
• Keep vehicle doors and windows securely locked / closed at all times.
• Maintain situational awareness at all times.
• In the hours of darkness when approaching junctions, slow down but avoid stopping if necessary.
• If traffic forces you to come to halt, if possible, leave enough space between you and the vehicle in front to allow you to maneuver away in a forward motion if necessary.
• Be wary of accident scenes/ breakdowns - they may be false. Do not stop.
Do not leave valuables on show in the car. Hide them away.

NOTE
When visiting hotels or Restaurants you should avoid complacency and be sure to adhere to basic security precautions. Note:- taxi drivers and hotel, Restaurant staff and Watchmen can act as informers to criminals, and personnel should be careful not to disclose personal information and avoid displaying valuables, which should be kept hidden in an understated bag or carefully concealed. When visiting beaches and local communities during the day, personnel should avoid carrying valuables.
 
Sehemu yoyote Dar haina muamana wa kuacha chochote ndani ya gari.

Kuna shoga'ngu alishachapwa nyanya na vitunguu aliviacha ndani ya gari lake.
Teh teh ungesema tu ni wewe umechapwa nyanya na vitunguu ,hizo habari za shoga ako umeamua tu kuua bendi
 
Wakuu jana baada ya pilika za kazi nilikuwa na ratiba ya kukutana na rafiki zangu hapo Catalunya opposite na Calabash kwa mazungumzo maalum.Nilipofika Mlinzi wa pale (Masai) akanieleza sehemu ya kupaki. Ndani ya gari nikaacha begi lenye laptop na vitu vingine lakini kwa taadhari nilishaliweka chini ya siti ya nyuma.
Baada ya kushuka nikiwa na mwenzangu nikamuuliza yule Mlinzi kama ndio muhusika wa usalama akakubali nikamuomba aniangalizie usalama wa gari langu. Tukaenda kukaa sehemu ya nje tunapoweza kuona pia gari vizuri. Muda wote tulikuwa makini lakini maongezi yalivyozidi na kidogo kupoteza umakini ule kwa kama dakika 10 ghafla yule Masai akanifata kuwa brother twende gari yako inashida. Tulipogeuka kuangalia gari taa ilikuwa inawaka na mlango upo wazi! Tulipoenda tukakuta kioo cha mlango kilichokuwa upande wa pili kimevunjwa mlango umefunguliwa na begi limebebwa. Kwa muda mrefu eneo nililopaki zilikuwepo gari mbili tu tena zilizo mbali kidogo kiasi ambacho huwezi kutarajia mtu apate ujasiri wa kuchungulia hadi aone begi kubomoa, kufungua mlango na kuvuta begi upande wa pili.Mlinzi akatupa Maelezo ya kujichanganya ikiwemo kutaka kuruka baadhi ya vitu. Muhusika wa hapo Catalunya anasema hata yeye ameshaibiwa Catalunya ya mlimani city siku si nyingi. Mlinzi yupo polisi mabatini. Chukueni tahadhari wananchi wenzangu maana ni dhahiri walinzi wanashirikiana na wahalifu. Nimeamua kulifatilia kwa ukaribu tukio hili na nitawajulisha kila hatua muhimu.
op

Pole mkuu, maana hapo ni hasara mara mbili: laptop na kio kuvunjwa!!!!!!!!!!!
 
Hahaha dada faiza unataka kuniambia kama umeshuka sehemu kama bar au una mizunguko inabidi vitu vilivyoko kwenye gar ushuke navyo hata nyanya,vitunguu,mkaa
hahahaha
Sehemu yoyote Dar haina muamana wa kuacha chochote ndani ya gari.

Kuna shoga'ngu alishachapwa nyanya na vitunguu aliviacha ndani ya gari lake.
 
Kila mara watu wanaibiwa laptop kwenye magari lakini hamkomi kuziacha kwenye magari na kuingia Bar.

Hata mimi sielewi kwanini tunafanya hili kosa. Halafu pia watu mchague sehemu za kwenda kustarehe kama una vitu vya thamani ndani ya gari.

Tatizo ni vigumu sana kupata watu waaminifu hapa kwetu Tanzania sasa hivi. Hata awe mzee, kijana, mwanaume na mwanamke wote sawa tu. Kila mtu anatafuta nafasi ya kuiba. Tuombe Mungu atusaidie.
 
mlinzi anashirikiana nao kwa jinsi tukio lilivyotokea akiminywa atsema mengi
 
Sehemu kama hizo ni viota vizuri vya majambazi wezi na vibaka
 
Siku zote unapopaki hakikisha hakuna vitu vinavyompa mtu ushawishi weka hata katika buti kama gari ina buti.
 
Sitaki hata kupasikia hapo Catalunya,Maasai alikuja kunistua kuwa gari imeibiwa nipo kwenye "chorus" ya kutafuna Makange...Baadae nikatumia "Private investgators" wangu nikaja kujua CATALUNYA ni kijiwe cha majambazi ya Mjini na wachora ramani wa wizi wa magari wa Dsm.Wale walinzi wa kimasai wanachora dili na "vibaka" njaa na kuiba vitu ndani ya gari....Wale kina Baba Yeyoo sio wa kuamini tena,wezi wakubwa na wachora michoro ya wizi.

Kuna siku nilienda kupata chakula na jamaa yangu,tukaacha laptop kwenye gari kwa kuiweka chini ya seat na kufunga milango na vioo,ndani ya Laptop kulikuwa na "Proposal" ya hatari ya Mradi wa REA tumetoka kui-wasilisha kwa wadau Wizara ya Nishati ili tupate mkwanja wa kuwasha umeme kijijini kwetu!Washenzi wale wakaiba Apple ile kumbe walikuwa mabwege tu wa techolojia,tukayakamata maeneo ya Mwenge na baadae ikaja kuonekana mchora mchoro ni Maasai mlinzi tuliomkabishi gari.Ila Maasai wana mbio asikwambie mtu,Maasai alivyoona anaenda kunyea debe alichoropoka tukabaki kuona shuka tu na pu..mbu zinaning'inia.Hapai pale Catalunya kwenda na gari au vitu vya thamani
 
Duh! Wewe utakuwa ni mgeni katika hili jiji la Makonda. Yani bado unaachaga Laptop kwenye gari? Kwa hili sikupi pole.
Tena ilibidi ukamatwe wewe kwa makosa ya uzembe maana watu kibao wameshalizwa laptos hapa mjin lakini nyie bado hamjifunzi tuu!
 
Kwan ukiweka chini ya siti wanajuaje maana barafu pia uliiweka chini ya siti au wana macho kama X-Ray
 
Wakuu jana baada ya pilika za kazi nilikuwa na ratiba ya kukutana na rafiki zangu hapo Catalunya opposite na Calabash kwa mazungumzo maalum.Nilipofika Mlinzi wa pale (Masai) akanieleza sehemu ya kupaki. Ndani ya gari nikaacha begi lenye laptop na vitu vingine lakini kwa taadhari nilishaliweka chini ya siti ya nyuma.
Baada ya kushuka nikiwa na mwenzangu nikamuuliza yule Mlinzi kama ndio muhusika wa usalama akakubali nikamuomba aniangalizie usalama wa gari langu. Tukaenda kukaa sehemu ya nje tunapoweza kuona pia gari vizuri. Muda wote tulikuwa makini lakini maongezi yalivyozidi na kidogo kupoteza umakini ule kwa kama dakika 10 ghafla yule Masai akanifata kuwa brother twende gari yako inashida. Tulipogeuka kuangalia gari taa ilikuwa inawaka na mlango upo wazi! Tulipoenda tukakuta kioo cha mlango kilichokuwa upande wa pili kimevunjwa mlango umefunguliwa na begi limebebwa. Kwa muda mrefu eneo nililopaki zilikuwepo gari mbili tu tena zilizo mbali kidogo kiasi ambacho huwezi kutarajia mtu apate ujasiri wa kuchungulia hadi aone begi kubomoa, kufungua mlango na kuvuta begi upande wa pili.Mlinzi akatupa Maelezo ya kujichanganya ikiwemo kutaka kuruka baadhi ya vitu. Muhusika wa hapo Catalunya anasema hata yeye ameshaibiwa Catalunya ya mlimani city siku si nyingi. Mlinzi yupo polisi mabatini. Chukueni tahadhari wananchi wenzangu maana ni dhahiri walinzi wanashirikiana na wahalifu. Nimeamua kulifatilia kwa ukaribu tukio hili na nitawajulisha kila hatua muhimu.
Lakini kila siku huwa watu wanatoa onyo ,usiache kitu chako cha thamani kwenye gari au hoteli,uliona uzito gani kubeba laptop yako ,kwani ulidhani waoibiwa hivyo vitu vyao huweka kwenye dashboard ,naona kama kuna aina ya kuwachafulia wenye Catalunya ili waonekane wakose wateje,kama ulipaki gari lako na ulikuwa unaangalia wakti wote imekuwaje watu wanavunja kioo nawe upo hapo hapo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom