Tahadhari: Catalunya Mwenge si salama

Tahadhari: Catalunya Mwenge si salama

Jamaa inaonekana kwanza walichungulia kwenye kioo cha gari wakaona kibegi, wakajua kitakuwa na milungula... Hii ndio Bongo Dar es Salaam.
 
Mali ya mtu kaitafuta kwa jasho halafu jitu jingine tena mbaya zaidi la jinsia ya kiume linalopenda maisha ya shortcut na mteremko linaivizia na kuiba.

Ndio maana hawa jamaa wakikamatwa wanapigwa kama si kuchomwa mpaka kufa.
 
Ulipomsisitiza mlizi achunge gari yako ndipo ulipo haribu,weka alarm na usiwe unaacha vitu kwenye gari,weka kwenye buti mapema sio ukishafika ndio unahamisha wakikuona
 
Wakuu jana baada ya pilika za kazi nilikuwa na ratiba ya kukutana na rafiki zangu hapo Catalunya opposite na Calabash kwa mazungumzo maalum.Nilipofika Mlinzi wa pale (Masai) akanieleza sehemu ya kupaki. Ndani ya gari nikaacha begi lenye laptop na vitu vingine lakini kwa taadhari nilishaliweka chini ya siti ya nyuma.
Baada ya kushuka nikiwa na mwenzangu nikamuuliza yule Mlinzi kama ndio muhusika wa usalama akakubali nikamuomba aniangalizie usalama wa gari langu. Tukaenda kukaa sehemu ya nje tunapoweza kuona pia gari vizuri. Muda wote tulikuwa makini lakini maongezi yalivyozidi na kidogo kupoteza umakini ule kwa kama dakika 10 ghafla yule Masai akanifata kuwa brother twende gari yako inashida. Tulipogeuka kuangalia gari taa ilikuwa inawaka na mlango upo wazi! Tulipoenda tukakuta kioo cha mlango kilichokuwa upande wa pili kimevunjwa mlango umefunguliwa na begi limebebwa. Kwa muda mrefu eneo nililopaki zilikuwepo gari mbili tu tena zilizo mbali kidogo kiasi ambacho huwezi kutarajia mtu apate ujasiri wa kuchungulia hadi aone begi kubomoa, kufungua mlango na kuvuta begi upande wa pili.Mlinzi akatupa Maelezo ya kujichanganya ikiwemo kutaka kuruka baadhi ya vitu. Muhusika wa hapo Catalunya anasema hata yeye ameshaibiwa Catalunya ya mlimani city siku si nyingi. Mlinzi yupo polisi mabatini. Chukueni tahadhari wananchi wenzangu maana ni dhahiri walinzi wanashirikiana na wahalifu. Nimeamua kulifatilia kwa ukaribu tukio hili na nitawajulisha kila hatua muhimu.


WA TZ KWA WIVU

HIZO NI BLA BLA ZA KIUSHINDANI KIBIASHARA.

JAMAA KAJITAHIDI KUWEKEZA SEHEMU NZURI SANA ILE.

UNAONGOZANA NAWADADA WA KUOKOTWA SINZA UNATAKA MASAI ALINDE MALI YAKO. UPUUZI
 
Sehemu yoyote Dar haina muamana wa kuacha chochote ndani ya gari.

Kuna shoga'ngu alishachapwa nyanya na vitunguu aliviacha ndani ya gari lake.
Teh teh..Kweli mwizi hakosi cha kuiba
 
Ile bar kila mtu mwizi, wahudumu mpaka na shoe shiner
 
Asante kwa taarifa Mkuu!

Weka ndani hao wapuuzi, anza na Mlinzi. Hakikisha hatoki ndani mpaka PC ipatikane.

Mtu unatafuta mali kwa jasho lako harafu anakuja mjinga mjinga anaiba kizembezembe tuu. Eboooo!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom