Tahadhari: Baada ya line kuzimwa leo utapeli huu utashamiri kwa kasi ya ajabu

adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
10,952
23,101
Moja kwa moja..

Nimeona tangazo kutoka serikali kuwa leo tarehe 13 line zote zisizo hakikiwa zinaenda kuzimwa. Kwa utafiti wangu mfupi nilioufanya unaonyesha Watanzania wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu zoezi ili kuanzia madhumuni yake ,jinsi ya kuhakiki nk..

UTAPELI UTAKUJA KIVIPI ?

Kuna vijana wanaopita mitaani kusajili lini hawa ndio waasisi wa utapeli huu kwa kujifanya wao wanahakiki kumbe wanachukua taarifa zako muhimu za miamala na namba yako ya siri bila kujijua na kujikuta kila hela itakauyoingia kwako wao wanawahi kupitia na wewe unaambulia kapa.

Hii itawezekana kutokana na Watanzania wengi hatupendi kufuatilia mfano muhimu yanayotuzunguka na uelewa mdogo kuhusu maswla ya utapeli.

USHAHIDI NO 1:

Mimi waliwahi kunijia vijana waopita kusajili line mtaani wakadai wanahakiki na kupandisha 4G line bure nikajifanya mjinga na kuwapa simu yangu .

Basi akaanza kutaka namba ya Nida nikaampa baadae akafika stage ya kuweka namba ya siri nikaweka kisha baada ya muda kidogo akasema tayari na kuondoka ,baada ya kuondoka mimi nikahisi lazima kunakitu litakuwa hakiko sawa nikawasha application yangu ya TigoPesa nikaangalia vifaa vilivyokuwa na access na akuanti yangu nikafuta simu yangu hii na simu nyingine ya kijana wa hovyo hapo nikaiondoa chap nikasalimika kwa mtindo huo.

USHAHIDI NO 2:

Kuna ndungu yangu nilimtumia kiasi fulani cha pesa baada zikapita siku mbili kisha akenda kwa wakala akaambiwa hana salio kwenye akaunti yake kuwapigia mtandao wakasema kuna mtu mwingine ana access na akuanti yake wakampa maekezo akamuondoa chap.

Nilipo muhoji akasema wiki moja iliyopita wazee wa kuhakiki walipita wakaihakiki laini yake na leo yamekuta hayo.

HITIMISHO:

Ni muhimu mamlaka husika kutoa tahadhari pamoja na kuzuia utapeli huu maana wabongo wengi wengi vijijini unakuta wazee wengine hawajui hata kuunga bando wanaweza kutapelika kirahisi sana.
 
Hawatazima hivyo ni vitisho kama vile tulivyoanza navyo na kulazimika kujipanga foleni, hata hivyo utapeli waliotudanganya utaisha uliendelea.
 
Back
Top Bottom