Jinsi mwizi anaweza kuiba pesa kwenye simu yako ambayo haina passwords kwenye line

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweka zile password/pin ambazo ukizima simu na kuwasha inadai uingize kwanza password kwenye hiyo line kabla ya kuendelea kutumia hiyo line.

Hebu fikiri, mtu aliibiwa simu na siku moja baadae ikafanyika miamala ya kuhamisha fedha kutoka kwenye account yake ya M-Pesa kiasi cha zaidi ya TZS. 3,000,000/= kwenda kwenye namba tofauti za simu. Swali ambalo wengi wangependa kujua ni kwamba, mwizi huyo aliwezaje kujua namba ya siri ya aliyeibiwa simu hadi kuweza ku- access account yake ya M-pesa na kutoa fedha??!!

Wengi wetu wanaweza kusema watu wa kampuni za simu wanahusika katika hili. Hebu fuatilia ujue mbinu iliyotumika au inayotumiwa na wezi wa aina hii:

1. Simu ikishaibiwa, kama simu yenyewe ina password, wanatoa line na kuweka kwenye simu nyingine.

2. Hatua ya pili, mwizi atataka kujua line hiyo ya simu imesajiliwa kwa jina gani? Hivyo atapiga *106# na baada ya hapo atabonyeza No 1. Kama line imesajiliwa, atakuwa amepata kujua jina kamili la mmiliki wa line hiyo.

3. Hatua ya tatu, atataka kufahamu account ya mwenye simu, mfano: m-pesa, ina kiasi gani cha fedha? Hapo mwizi atatumia simu yake au simu ya mtu mwingine anayefahamiana naye kutuma kiasi fulani cha fedha, mfano atatuma TZS. 2,000/= kwenda kwenye namba ya simu ya aliyeibiwa. Pesa hiyo ikishaingia, automatically line ya simu iliyoibiwa italetewa sms inayoonyesha kutumiwa kiasi cha fedha, na salio lake jipya la wakati huo baada ya kutumiwa fedha.

4. Baada ya mwizi kujua salio, sasa anaweza kuweka mikakati ya kuiba kama account ya aliyeibiwa simu ina kiasi cha fedha zinazoweza kuibika.

•Hatua ya kwanza anapiga simu Customer Care na kujitambulisha kuwa yeye ndiye mwenye line ya simu iliyobiwa. Kumbuka jina analo tayari.

•Hatua ya pili akishapiga simu, atawaambia kuwa amesahau password ya account yake, Customer Care watakachotaka kujua kutoka kwake ni lini alifanya muamala wa mwisho, na ilikuwa ni kiasi gani, na salio lake kwenye account yake ni kiasi gani. Kumbuka taarifa zote hizo jamaa anazo tayari, hivyo anawaelezea watu wa Customer Care na wanamuelewa vizuri tu.

•Kutokana na usahihi wa taarifa za mwizi alizotoa kwa Customer Care, watamuamini na kumtumia code namba ambazo atatumia kubadilisha namba ya siri, na hivyo anafanikiwa ku-access account ya victim na kufanya miamala vile atakavyo.

MUHIMU
Ni vyema ikitokea mtu kaibiwa simu yake, immediately apige simu kampuni husika na kutoa taarifa ili line yake iwe blocked. Asitumie muda mrefu kutoa taarifa polisi na kufuatilia Loss Report pasipo kwanza kuwasiliana na Service Provider. Hii inaweza kusaidia kuzuia madhara yanayoweza kutokea mara baada ya mtu kuibiwa simu. Asanteni

USHAURI PIA KWA MITANDAO YA SIMU.
Mtu akipiga simu kuomba msaada wa kubadilisha namba ya siri waongeze pia idadi ya maswali ya udadisi kama namba ya kitambulisho alichosajili sajilia line, mwaka wa kuzaliwa, nk
 
Nikitaka kukuibia PIN haitakusaidia chochote nitakachofanya naingiza wrong PIN mara 3 naambiwa PIN blocked enter PUK kisha nachukua cm nyingine napiga customer service naomba PUK naingiza line inafunguka naambiwa enter new PIN (hii imeenda).
 
Labda niulize, line ikiwa pined, mwizi hawezi kutumia utaratibu huo huo wa kuomba msaada huduma kwa wateja kwa service provider ili afunguliwe password?
Line ikiwa pinned kila ukizima simu inadai pin , ukikosea mara tatu itadai puk. Puk unaweza omba kutoka kwa service provider ila mlolongo ni mrefu na siku hizi ni lazima ufike ofisini
Halotel line zao mpya zote zina pin by default na hakuna option ya kuondoa, japo unaweza kubadilisha .
 
Ukishapoteza simu, piga huduma kwa Wateja waiblock kwa muda mpaka utakapoenda kuihusisha upya.

Namba za NIDA? Vijana wanaosajili wana access ya kuipata bila jasho. Anaingiza tu namba ya simu inamletea namba ya NIDA ya Mhusika.

Ukitaka kuomba PUK, ukipiga huduma kwa wateja wanakuuliza tu maswali wanakufungulia. Taarifa zote zinakuwa very accessible.

Kama umesahau namba ya siri huwa wanauliza maswali yafuatayo;
1. Majina sahihi
2. Aina ya kitambulisho
3. Namba za kitambulisho
4. Salio
5. Muamala wa mwisho na aina

Sasa ukishakuwa na namba ya NIDA ya mhusika, kazi kwisha.

Ninachopenda TIGO, kuna kiwango ukikifikia hawawezi kukufungulia. Mfano una laki tano kwenye akaunti yako, Tigo hawafungui. Watakuambia fika duka lao lililo karibu yako.

PIN hazitakusaidia. Ukipoteza, piga ifungwe.
 
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweka zile password/pin ambazo ukizima simu na kuwasha inadai uingize kwanza password kwenye hiyo line kabla ya kuendelea kutumia hiyo line.

Hebu fikiri, mtu aliibiwa simu na siku moja baadae ikafanyika miamala ya kuhamisha fedha kutoka kwenye account yake ya M-Pesa kiasi cha zaidi ya TZS. 3,000,000/= kwenda kwenye namba tofauti za simu. Swali ambalo wengi wangependa kujua ni kwamba, mwizi huyo aliwezaje kujua namba ya siri ya aliyeibiwa simu hadi kuweza ku- access account yake ya M-pesa na kutoa fedha??!!

Wengi wetu wanaweza kusema watu wa kampuni za simu wanahusika katika hili. Hebu fuatilia ujue mbinu iliyotumika au inayotumiwa na wezi wa aina hii:

1. Simu ikishaibiwa, kama simu yenyewe ina password, wanatoa line na kuweka kwenye simu nyingine.

2. Hatua ya pili, mwizi atataka kujua line hiyo ya simu imesajiliwa kwa jina gani? Hivyo atapiga *106# na baada ya hapo atabonyeza No 1. Kama line imesajiliwa, atakuwa amepata kujua jina kamili la mmiliki wa line hiyo.

3. Hatua ya tatu, atataka kufahamu account ya mwenye simu, mfano: m-pesa, ina kiasi gani cha fedha? Hapo mwizi atatumia simu yake au simu ya mtu mwingine anayefahamiana naye kutuma kiasi fulani cha fedha, mfano atatuma TZS. 2,000/= kwenda kwenye namba ya simu ya aliyeibiwa. Pesa hiyo ikishaingia, automatically line ya simu iliyoibiwa italetewa sms inayoonyesha kutumiwa kiasi cha fedha, na salio lake jipya la wakati huo baada ya kutumiwa fedha.

4. Baada ya mwizi kujua salio, sasa anaweza kuweka mikakati ya kuiba kama account ya aliyeibiwa simu ina kiasi cha fedha zinazoweza kuibika.

•Hatua ya kwanza anapiga simu Customer Care na kujitambulisha kuwa yeye ndiye mwenye line ya simu iliyobiwa. Kumbuka jina analo tayari.

•Hatua ya pili akishapiga simu, atawaambia kuwa amesahau password ya account yake, Customer Care watakachotaka kujua kutoka kwake ni lini alifanya muamala wa mwisho, na ilikuwa ni kiasi gani, na salio lake kwenye account yake ni kiasi gani. Kumbuka taarifa zote hizo jamaa anazo tayari, hivyo anawaelezea watu wa Customer Care na wanamuelewa vizuri tu.

•Kutokana na usahihi wa taarifa za mwizi alizotoa kwa Customer Care, watamuamini na kumtumia code namba ambazo atatumia kubadilisha namba ya siri, na hivyo anafanikiwa ku-access account ya victim na kufanya miamala vile atakavyo.

MUHIMU
Ni vyema ikitokea mtu kaibiwa simu yake, immediately apige simu kampuni husika na kutoa taarifa ili line yake iwe blocked. Asitumie muda mrefu kutoa taarifa polisi na kufuatilia Loss Report pasipo kwanza kuwasiliana na Service Provider. Hii inaweza kusaidia kuzuia madhara yanayoweza kutokea mara baada ya mtu kuibiwa simu. Asanteni

USHAURI PIA KWA MITANDAO YA SIMU.
Mtu akipiga simu kuomba msaada wa kubadilisha namba ya siri waongeze pia idadi ya maswali ya udadisi kama namba ya kitambulisho alichosajili sajilia line, mwaka wa kuzaliwa, nk
Una pount ila kuna mambo siku hizi kwenye mitandao ya simu ni kama hayawezekani.
 
Back
Top Bottom