Ushauri kwa makampuni ya simu kuhusu matumizi ya line za simu

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,789
2,383
Hongereni kwa majukumu ya kazi wadau wa mawasiliano. Naomba kutoa ushauri kwa makampuni ya simu kuondoa matumizi la line nyingi kwa huduma zinazofanana.

Wazo hili limenijia baada ya kutakiwa kusajili line nyingi kwa matumizi yaleyale kama jina langu. Nilifungua biashara A ambayo nilihitaji kuwa na LIPA NAMBA. Nililazimika kusajili line mbili za mitandao fulani ya simu. Juzi nikafungua biashara B pia nikatakiwa kuwa LIPA NAMBA. Nilvyoenda ofisi za hayo makampuni ya simu nikatakiwa kusajili tena line mbili tena. Niliwaambia kwa kuwa mmiliki ni mimi kwa nini wasitumie line zilezile wakasema haiwezekani.

Kumbuka kwenye hizi biashara nimefunga CCTV kamera. Napo nimesajili line moja moja kwa kila duka.

Mpaka hapo namiliki line 6 kwa biashara mbili tu kabla sijahesabu line ninazotumia kwenye simu zangu. Hii ni adhabu kwelikweli.

Nashauri makampuni ya simu yabuni njia nzuri ya kupunguza matumizi ya line za simu hasa kwa shughuli zinazofanana inapotokea mmiliki ni moja. Hii itanguza sana kadhia ya kukariri namba za simu maana lazima line zote ziwe active.

NB. Siku mkitekeleza jambo hili msisasau kunilipa mirahaba japo kidogo.
 
Hii ilinitokea pia Ila wakanipigia simu nikaunganishe na laini moja ya mtandao husika
 
Back
Top Bottom