Wizara ya Fedha: Tunafuatilia wanaofanya utapeli kwa Wastaafu wanaofuatilia mafao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika katika Ukumbi wa 88 Mkoani Morogoro, linaendelea katika siku ya pili na ya mwisho Jumanne Oktoba 24, 2023.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha, Benny Mwaipaja amefungua majadiliano kwa kushukuru jinsi Mitandao ya Kijamii inavyoendelea kutumika kufikisha taarifa mbalimbali kuhusu utendaji wa Wizara ya Fedha ikiwemo elimu kwa mlipa kodi.

Utapeli wa mafao ya wastaafu
Akizungumzia mazingira ya uwepo wa utapeli unaofanywa kwa njia ya simu na nyinginezo kwa wastaafu wanaofuatilia mafao yao, Benny Mwaipaja amesema huduma zote za kufuatilia katika mamlaka na mifuko mbalimbali zote zinafanwa bila malipo na katika ofisi rasmi za mamlaka.

Mwaipaja amesema Wizara ya Fedha inafanyia kazi changamoto hiyo kwa kufuatilia namba mbalimbali zinazotumika kufanya utapeli au kujaribu kufuata utapeli.

Amesema “Namba zinazotumika kufanya uhalifu huo tunazifuatilia, wanapateje taarifa sahihi za Wastaafu? Hilo ni swali ambalo tunalifanyia kazi kwa ukaribu kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, mfano mmoja ni kuwa kuna mhalifu ambaye yupo Dar es Salaam amekuwa akibadilisha namba mara kwa mara, tunamfuatilia kwa kuwa amekuwa akitusumbua sana.

Benny 2.JPG

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha, Benny Mwaipaja

“Imekuwa ikitokea mara nyingi tapeli anapiga simu kwa mstaafu akiwa anajua taarifa zote zake nyingi muhimu, akikutana na mtu ambaye hana utulivu wala umakini katika kung’amua mambo anatapeliwa.

“Hivyo, jamii ifahamu kuwa ikiona kuna mtu anakwambia kuhusu habari za tuma hela au pelekea hela sehemu fulani, tambua kuwa huo ni utapeli.”

Elimu kwa Wastaafu
Kuhusu changamoto ya Wastaafu kutokuwa na uelewa wa jinsi ya kufuatilia maslahi yao baada ya kustaafu, Mwaipaja amesema Wizara imekuwa ikitoa elimu ya masuala ya kifedha ikiwemo kufuatilia stahiki zao miezi sita kabla ya kustaafu kwao.

Amesema “Tunawafundisha jinsi mafao yao yanavyopatikana na jinsi ya kuwekeza kwenye masuaa mbalimbali ikiwemo kwenye mifumo ya Serikali badala ya kuingia kwenye biashara ambazo baadaye zinaanza kumpa msongo wa Mawazo.”
Wasikilizaji.JPG

Moja.JPG

Wadau wakifuatilia mijadala katika Kongamano.
Vijana wengi wanafikiri hawatastaafu
Awali, Mhasibu Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, CPA Jenipha Josephat Ntangeki akifafanua kuhusu mchakato wa Wastaafu naye aliwasisitiza wanufaika hao kutumia njia sahihi kwa kwenda kwenye Ofisi za Hazina zilizopo ndogo zilizopo mikoani.

Amesema “Tumekuwa tunatoa mafunzo ya maelekezo kwa Wastaafu na Wastaafu watarajiwa kuhusu wafanye nini wanapokuwa katika mchakato.

Jenipha ameeleza kuwa “Vijana wengi wakiingia kazini hawafikirii kama kuna kustaafu, kila inapotokea nafasi ya wao kupewa elimu kuhusu mafao ya kustaafu wamekuwa hawazingatii.
Jenipha.JPG

Wizara ya Fedha, CPA Jenipha Josephat Ntangeki
“Mara nyingi ikifika mwishoni wanapoelekea kustaafu au wanapostaafu kabisa ndipo wanaanza kutaka kujua wanapataje stahiki zao.

“Hawataki kufuatilia kuanzia hatua ya mwanzo nini kinatakiwa kufanyika, hata inapotakiwa kuwa kufuatilia wao wanauliza jinsi gani ya kupata fedha bila kujua taratibu zinazotakiwa kufuatwa, ndio maana ikitokea wamepigiwa simu kushawishiwa kutuma hela ili wapatiwe huduma inakuwa rahisi kutapeliwa.

“Vijana wengi tunaona mambo ya kustaafu ni ya Wazee wakati kiuhalisia tunatakiwa kujua mapema, tunatakiwa kujifunza ni vizuri ukalifanyia kazi hilo.”
 
Vijana watastaafu vipi wakati hawana hata ajira ? Au mafao ni kwa kila mtu hata ambaye hana ajira ?
 
Kazi ya TCRA hii kwenye simu kila kukicha matangazo ya kitapeli tu mpaka hayo Makampuni ya Simu nao utaona mara vodabima sijui na takataka zingine je wana vibali vya Bima na mmefanya uhakiki kuwa Wanatakiwa watoe hiyo Huduma au Ujambazi tu kama kawaida yao...
 
Back
Top Bottom