Hayo utayaona kwenye Mazao yote hapa kwetu Tanzania
AISEEEE, nimekusoma sana mkuu.
Jambo la ziada kidogo: hivi inakuwaje tunao wataalam chungu nzima wizarani (kilimo na kwingineko); hivi hawa wastu wanafanya kazi gani huko?
Baada ya kuweka bandiko langu la mwanzo katika mada hii, likaniijia swali: hivi nchi kama Vietnam ambao ndio wanaoongoza katika zao hili wao wakoje? Nika-'google' "Vietnam Cashewnut Processing Industry" Nikakuta taarifa nyingi tu, na hata wao wanavyohangaikia kupata mali ghafi za kulisha viwanda vyao, na jinsi wanavyolinda 'technology' yao ili waendelee kuwa vinara. Waliwanyima Nigeria teknologia hiyo walipoiomba 2007 kwa sababu za ushindani huo.
Nimesoma dakika chache tu na kupata picha ya yanayotusumbua sisi, moja wapo likiwa hilo la kukosa teknologia sahihi. Sasa najiuliza, pamoja na kuwa na wasomi wote hawa tulionao sasa tunashindwa kabisa angalao kujua matatizo yetu yanatokana na nini, tunabaki kuwa watu wa kubahatisha tu? Juzi Rais Magufuli akadhani Jeshi litatumia vile viwanda kuuku tulivyokuwa navyo, jamaa (wataalam wetu) wanamwangalia tu, pengine wakichekelea! Nilliona picha ya wanajeshi wamepinda migongo wakibeba mashine, sijui walikuwa wanaipeleka wapi!
Magufuli angependa kuwa Dikteta wa ukweli, udikteta wake ulitakiwa ufanyike huko huko kwa watu wake huko serikalini, na sio huku uraiani. Hata mimi ningemuunga mkono. Hawa wasomi tulionao ni lazima wafanye kazi kama punda kama hawawezi kujituma wenyewe.
Kwa hiyo inawezekana sana kwa hawa wafanya biashara wetu hapa wanasita kuingia katika biashara hiyo kwa kujua ugumu huo. We have no technology needed to process the damn thing efficiently, and those who have the technology are reluctant to share!
No wonder, we hardly see any of those companies willing to set up here, even with the available incentives.
Narudi huko huko nilikoanzia. Suluhisho la matatizo yetu haya ni kuwapa wakulima uwezo. Acha waunde Ushirika wao na wawe na uwezo wa kila namna katika shughuli za mazao wanayoyalima.