Tabora – Uyui: Wananchi waliotakiwa kupisha Mradi wa SGR waomba Serikali isaidie walipwe fidia zao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,985
12,312
Wananchi wa Tambukareli, Kata ya Nsololo, Wilaya ya Uyui wanaiomba Serikali kutoa ufafanuzi juu ya malipo yao ya fidia kupisha ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, wakidai awali tathimini ilifanyika Machi 2023 na mpaka Mei 2024 hawajui hatima ya malipo yao.

Wameyasema hayo wakati wakidai Sheria inaelekeza baada ya tathimini malipo yafanyike ndani ya Miezi 6 lakini wanadai hawajalipwa, hivyo wanashindwa kuendeleza makazi yao.
photo_2024-05-25_00-55-49.jpg

photo_2024-05-25_00-55-42.jpg

photo_2024-05-25_00-55-58.jpg

photo_2024-05-25_00-55-53.jpg
Wanadai kuwa baadhi ya nyumba zimeshindwa kujenga vyoo na wengine wakiwa wamepewa zuio la kutakiwa kutofanya maendeleo yoyote ya ujenzi baada ya kupewa barua za tathimini.

Majibu ya Serikali soma hapa

~ Mkuu wa Wilaya: Wananchi wa Uyui wanaodai malipo ya kupisha Mradi wa SGR wafike ofisini
~ Mbunge ahoji ukimya wa Serikali kuhusu fidia ya waliopisha Reli ya SGR Tabora
 
Back
Top Bottom