TRC: Suala la Nauli za Treni ya SGR tumekabidhi mapendekezo kwa LATRA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,991
12,343
large-1711552010-IMG-20240327-WA0002.jpg

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imefanya ziara ya kukagua Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kujionea majaribio ya treni hiyo ambayo yalianza hivi karibuni.

Ziara hiyo imeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vuma Augustine (Mbunge wa Kasuru vijijini), ambapo aliambatana na wajumbe wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa na wadau wengine kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro kwa kutumia treni hiyo Machi 27, 2024.

Makamu huyo amesema Kamati hiyo imeridhishwa na mradi huo na kudai unatekelezwa katika kiwango kinachostaili na kufanya kuwavutia wananchi huku akiipongeza TRC kwa usimamizi mzuri.

Kamati ya PIC imefanya ziara kwanza ya kukagua Mradi wa SGR na kuangalia majaribio ambayo TRC wanayafanya kama maandalizi ya kuanza kwa safari zao rasmi

Ameongeza "Kama Kamati tumeridhishwa na pasipo na shaka kwa huu mradi umetekelezwa katika viwango ambavyo vinastaili, viwango vizuri kwa kweli ni mradi unaovutia kwa Watanzania."

Aidha, amesema kuwa mpaka sasa mradi huo unaotumia zaidi Tirioni 23 tayari Serikali imetoa zaidi ya asilimia 40 ya fedha hizo huku ikiendelea kutoa nyingine kulingana na ujenzi unavyoendelea.

"Nichukue nafasi hii kwa niaba ya Kamati kwanza kuipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo imefanyika kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya mradi huo, kwa sababu mradi huu wote wa ujenzi wa mtandao wa reli Tanzania," amesema Vuma Augustine.

Ameongeza kuwa "Pia niipongeze TRC kwa usimamizi mzuri na makini, lakini rai yangu kwa TRC, moja waendelee kutunza miundombinu hii lakini waendelee kuwasimia wakandarasi kwenye miradi kukamilisha kazi ndogondogo zilizobaki kwenye kipande hiki kinachokaribia kukamilika"

Aidha, kwa upande wa Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa akizungumzia ziara ya Kamati ya PIC, ameleza umuhimu wa Kamati hiyo ambayo amesema ina jukumu la kuangalia tija ya pesa ambazo zimekuwa zikipitishwa kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo SGR, lakini amesisitiza kuwa ni jambo muhimu kusikia Kamati hiyo imeridhishwa na hatua zinazoendelea TRC ikiwemo usimamizi mzuri wa mradi.

"Tuishukuru sana Kamati yetu ya PIC ndiyo inahusiana na uwekezaji wa mitaji ya Serikali kwenye mashirika yetu mbalimbali, kwahiyo ni Kamati muhimu kwetu tunaenda kuomba Bajeti tunapewa mapesa lakini Kamati inakuja kuangalia tija ya hizo pesa zilizoletwa.

“Ni Kamati muhimu sana katika taasisi, na ujue kama TRC tunachukua mapesa mengi sana ndani ya Bajeti, nafikiri mjue ndio taasisi inayochukua pesa nyingi kwenye bajeti, kwahiyo ujio wao hapa ni muhimu sana na hasa hasa tunaposikia wameridhishwa kwa kile wachokiona," amesema Kadogosa

Ameongeza kuwa suala la nauli zitakazotumika kwenye maeneo ambayo yanatarajiwa kuanza kazi Mwezi Julai 2024 kwa upande wao wameshakamilisha utaratibu na kuwasilisha kwenye mamlaka husika ambao ni LATRA ambao wataweka nauli wazi mara baada ya michakato yao ikiwemo kuwashirikisha wadau wengine.
 
NAULI ZIAKISI HALI HALISI SIO KUKOMOANA
 
Back
Top Bottom