Tabia za Kitanzania zinazonikera...

Tabia za Kitanzania zinazonikera...

Yaani..unaona kama unakumbatiwa hivi..na kwapa sasa ndo uuuuwi!!!!

Mkwapa una ramaniiiiiii...halafu analalamika duuunh leo jooootoooo!!!!!!!

Mwanaume ana nuka kama beberu, mwanamke na shoga wananukia.
 
Kiranga ,sijakuuliza kuhusu watu wa nchi zingine kama wana tabia hizo
'
Pia sijakuuliza ni nchi gani ina watu wengi wenye tabia hizo,wala sijashandanisha nchi na nchi ili kujua nani ni kidedea
'
Wala halikua lengo langu kujua hayo,so you can keep all that by yourself,nilichokuuliza kama watanzania wana tabia hizo ama la,nashukuru kwa kunijibu
'
Sasa nakuuliza,hao wenye tabia hizo ambao umekubali ni watanzania,sasa kuna ubaya gani kwa mtoa mada kuwaita Watanzania?
 
Last edited by a moderator:
Kuamshwa na adhana za misikiti kila siku 5am. Kupigiwa kengele kila jumapili asubuhi 6am
Nataka nifaidi usingizi wangu hadi 7am
 
Mwanaume ana nuka kama beberu, mwanamke na shoga wananukia.

Kwani ukiwa mliberali ni lazima kila.mada uhusianishe na hobby yako???

Unachokoza watu halafu muandamane kuwa mnanyimwa haki zenuuu!!!!!!!
 
Yaani siipendi hii tabia, Bodaboda anatakiwa kupanda mtu mmoja lakina unakuta watu8 wamepanda huku inakoroma weee, kelele mtindo mmoja!
 
Mtu kavaa vizuri, yupo kwenye dala dala iliyojaza mbaya, kasiama halafu ana tooth pick mdomoni. Huwa natamani daladala liharibike ili safari iishie hapo hapo.
 
Kiranga ,sijakuuliza kuhusu watu wa nchi zingine kama wana tabia hizo

Lakini imedaiwa tabia hizi ni za Kitanzania, kitu ambacho kimenifanya nichunguze kama kweli hizi tabia ni za kitanzania? Nakuta zipo dunia nzima, kwa nini zinaitwa za Kitanzania?
'
Pia sijakuuliza ni nchi gani ina watu wengi wenye tabia hizo,wala sijashandanisha nchi na nchi ili kujua nani ni kidedea

Ungekuwa na justification kidoogo kudai tabia hizi ni za Kitanzania kama kungekuwa na utafiti wa kuonesha kwamba Watanzania ndio wanaoongoza katika tabia hizi, ingawa hata hapo napo kama wangekosa monopoly kusema hizi tabia ni za Kitanzania kutakuwa ni kukosea kama vile kusema mchezo wa Marathon ni wa Wakenya. Kwa hiyo hata pale ambapo ungekuwa na a dubious justification, umeikosa.
'
Wala halikua lengo langu kujua hayo,so you can keep all that by yourself,

Hapana, usipotaka kuelezewa kwa mapana usiniulize swali. Kiranga si mtu wa kuelezea vitu juu juu.

nilichokuuliza kama watanzania wana tabia hizo ama la,nashukuru kwa kunijibu

Hilo by the way ndilo lilikuwa jibu la summary, sasa ungepata jibu refu linalokwenda kwenye academic research zinazo debunk the entire notion of the centrality of tribes and the tangibility of nation states sijui ungesemaje.

Sasa nakuuliza,hao wenye tabia hizo ambao umekubali ni watanzania,sasa kuna ubaya gani kwa mtoa mada kuwaita Watanzania?

Kwa sababu hawafanyi mambo hayo kutokana na utanzania wao, wanafanya mambo hayo kwa uchafu, ujinga, upumbavu wao. Kwa hiyo, tusems "Tabia za kipumbavu zinazonikera" etc. Kusema "Tabia za kitanzania zinazonikera" halafu kulist hizi tabia ambazo Watanzania wengine hatuna, kunatutukanisha Watanzania wote, wenye tabia hizo na wasio na tabia hizo, na vivyo hivyo kunawaacha wasio Watanzania wenye tabia hizo.

Ukiongelea kukerwa na "tabia ya Kitanzania" ya kukojoa ovyo, akija M-Nepal ambaye ndiye mara yake ya kwanza kufika Tanzania na hana contact na Watanzania akikojoa ovyo, utaona sawa? Tabia ya Kitanzania kaipata wapi huyu?

Kusema tabia za uchafu, ujinga na upumbavu kwa jina la "tabia za Kitanzania" ni kukosa kuelewa kwamba hizi tabia hazitokani na utanzania, kwani zingetokana na utanzania zisingekuwepo kwa wasio Watanzania na Watanzania wote wangekuwa nazo.
 
hahahahaaaaaa!
Skiza nkwambie . . . Bla blah blah. . . .Skiza nkwambie . . . Blah. . . Blah. . . Blah . . . Skiza nkwambie. . .

Yani huwa nakasirika......lakin ndo hivyo bhana si unajua tena ni ngumu pia kujua mapungufu yako yanayowakera wengine.
Pia kuna wale wakujichokonoa pua......teh teh teh
 
tabia ya traffic police akikusimamnisha kukuuliza unafanya kazi gani inanikera.
 
Afu kuna tabia unakuta mtu anafanya afu hajistukii kabisa. Kuna siku nilikuwa na rafiki yangu kwenye ji-international airport. Kuna que ya maana, nikampa chewing gum. Yaani nilitaka kuzimia alipoifungua na kutupa kikaratasi hapo chini! Niliinama tu kukiokota bila kuongeza neno! Na alivyo mrembo na msomi!
 
Back
Top Bottom