Taasisi ya Moyo wa Mwanamke Shujaa Yafanya Kongamano na Kuiasa Jamii Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

TAASISI YA "MOYO WA MWANAMKE SHUJAA" YAFANYA KONGAMANO NA KUIASA JAMII KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

TAASISI ya Moyo wa Mwanamke Shujaa yenye Makao yake Makuu Manispaa ya Morogoro chini ya Mkurugenzi wake, Dkt. Magreth Kongera, imefanya Kongamano la maombi na uzinduzi wa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na changizo la ununuzi wa gari la kusaidia Taasisi hiyo kutoa huduma.

Kongamano hilo la Kihistoria lililohudhuriwa na jamii mbalimbali ikiwemo viongozi wa Serikali , Chama, wanafunzi wa vyuo na Sekondari limefanyika katika Ukumbi wa Tanzanite Manispaa ya Morogoro Septemba 24/2023.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt. Kongera, amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na changizo la ununuzi wa gari la kusaidia Taasisi hiyo kutoa huduma.

Dkt. Kongera, amesema kuwa kongamano hilo lilienda sambamba na kukabidhi kutoa elimu mbalimbali ikiwemo miongozo ya malezi ya Watoto pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto za kikatili katika maeneo yao wanayoishi.

Aidha, Dkt. Kongera, amesema suala la ukatili wa kijinsia ni mtambuka kwani hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amelipa kipambele katika kulisimamia kwa kutaka mamlaka husika kuunda sheria kali dhidi ya wanaobainika kufanya ukatili katika jamii.

Mwisho, Dkt. Kongera ameishukuru Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa kuonesha nia ya kusaidia Taasisi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Wabunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Mzeru pamoja na Mhe. Dkt. Christine Ishengoma,Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero kwa kuwapatia Taasisi hiyo eneo kwa ajili ya kujenga Kituo cha kutolea huduma katika Wilaya ya Mvomero.

Naye, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Christine Ishengoma, amesema kuwa Mkoa wa Morogoro unakabiliwa na changamoto kadha wa kadha zinazopelekea watu kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili, utoro shuleni, ndoa za utotoni, mimba kwa wanafunzi, n.k.

“Changamoto ni nyingi ila tushirikiane kuzitatua. Watoto wasipopata elimu kizazi kinaharibika, mtu anayefanyiwa ukatili hawezi kuwa na amani wala furaha,sote tuchukue hatua, Serikali ichukue hatua, taasisi za dini zichukue hatua na kila kundi katika jamii lichukue hatua kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii” Amesema Mhe. Dkt. Ishengoma.

Kongamano hilo lilitanguliwa na mjadala kutoka kwa wataalamu wa masuala mbalimbali ya elimu wakijadili namna matukio mbalimbali ya kikatili yanavyotokea kwenye jamii zetu na kuona kuwa wazazi wakisimama imara kwenye familia zao, suala la ukatili litakwisha.

Wataalam hao wameongeza kuwa wote wanaume na wanamke wakisimama, tunaweza kupinga ukatili wa kijinsia.

Taasisi ya Moyo wa Mwanamke Shujaa imekua ikishirikiana na Serikali kwenye mambo mengi ya kutoa huduma kwa jamii ikiwemo huduma za kiroho kupitia mafundisho ya Neno la Mungu inayotolewa kwenye makanisa , shule, hospitali na kuandaa makongamano kama haya yenye dhumuni la kuisaidia Serikali kupambana na matukio mbalimbali yanayojitokeza katika jamii zetu.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-10-06 at 12.00.44.mp4
    15 MB
  • WhatsApp Image 2023-10-06 at 12.00.45.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-06 at 12.00.45.jpeg
    107.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-06 at 12.00.47.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-06 at 12.00.47.jpeg
    105.3 KB · Views: 1
  • D39.jpg
    D39.jpg
    17.5 KB · Views: 1
  • d23.jpg
    d23.jpg
    12 KB · Views: 1
  • D32.jpg
    D32.jpg
    17.8 KB · Views: 1
  • d22.jpg
    d22.jpg
    17.1 KB · Views: 1
Back
Top Bottom