Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Regumalile ni fisadi mbaya sana. Sasa kaamua kumchafua Rais na Zitto huku akijua kabisa huyu Rais ndio anaembeba hata ktk mikataba yake.
 
Nimeshangazwa Sana na kauli aloitoa zzk kukanusha madai ya Dr Mengi, kauli hii inanipa utata Sana maana nachokumbuka Raisi JK ni kweli alikuwa Ughaibuni wakati sakata la escrow linaendelea but mweshimiwa aliludi wakati bado bunge laendelea, tena hakuna siku nlokuwa boadi Kama siku hiyo maana local channel zilianza rusha matangazo ya mweshimiwa akitoa historia ya ugonjwa wake na vipindi vya bunge kuhamishiwa TBC 2 ambako sisi makabwela hatukuwa na access nayo. Watanzania tubadilike tusiwe watu wa kubuluzwa mda wote.
Nawasilisha.
 
Alirudi wakati bunge ndo linaelekea mwisho.kwahiyo kusema zito alipomaliza kuwasilisha escrow akaenda kumwona jk ambaye hakuwepo kwa mwezi wote ni urongo wa wazi
 
Zitto anacheza na akili za watanzania. Ameshambulia sana gazeti la Mawio, lakini hajajibu hoja hata moja. Mawio kwa wiki kadhaa limekuwa linafunua uongo wa Zitto. Ajibu hizo hoja ili tumwelewe. Vinginevyo asubiri tu historia itamhukumu
 
Nimeshangazwa Sana na kauli aloitoa zzk kukanusha madai ya Dr Mengi, kauli hii inanipa utata Sana maana nachokumbuka Raisi JK ni kweli alikuwa Ughaibuni wakati sakata la escrow linaendelea but mweshimiwa aliludi wakati bado bunge laendelea, tena hakuna siku nlokuwa boadi Kama siku hiyo maana local channel zilianza rusha matangazo ya mweshimiwa akitoa historia ya ugonjwa wake na vipindi vya bunge kuhamishiwa TBC 2 ambako sisi makabwela hatukuwa na access nayo. Watanzania tubadilike tusiwe watu wa kubuluzwa mda wote.
Nawasilisha.
Vijana wa Chadema mna akili Timamu,Nauliza...???
 
Inabidi nianze kununua MAWIO sasa kumbe huwa linafunua maovu ndo nmegundua sasa
 
Nitafurahi katika mikutano yake hiyo ataje majina ya watu walioficha mabilion Uswiss. Hilo hatutalisahau
 
Zitto na mengi wote wezi tu mafisadi wa kuogopa sana hawafai kuwepo kwenye jamii ya watu wastarabu.
 
Zitto amedisappoint mageuzi nchini. Kweli njaa mbaya sana!

Lakini ni kawaida kwenye harakati, watu dizaini hiyo hawakosekani.

Ni vema waliosalia katika mapambano wakaze uzi, mana mapambano si lelemama.
 
Huu ushirikiano Mpya kati ya Rugemarila (Mtuhumiwa wa Escrow)na Mmiliki wa Mwana Halisi Forum na Mwandishi wa gazeti la Mawio si Salama kwa Rasilimali za nchi.

Katika kuhangaika Mzee Mengi,amemtuhumu Zitto Kabwe kuwa ndiye kampelekea Rais Kikwete taarifa juu ya Mengi Kumshighulikia pindi atakapo staafu.Lengo la habari hii ni mwendelezo wa visasi na vita ya kuhakikisha Zitto anapotea hatimae kufifiza harakati za ACT-wazalendo.

Kwamujibu wa Mengi, Chanzo cha habari hizo ni Gazeti Jipya la 'Taifa Imara' lililoanzishwa Kimkakati.

Gazeti la Taifa Imara lenyewe mnajua linamilikiwa na nani?

Gazeti la Taifa Imara ni Mali ya Rugemalila ambae ni Miongoni mwa watuhumiwa wa Ufisadi wa Escrow waliowaponza Tibaijuka na Werema .

Sasa mtu huyu huyu alianikwa tena hivi karibuni kwenye ziara ya ACT-Wazalendo kuwa kapewa tenda ya Tril 54 kujenga Bandari ya Mwambani corridor kinyemela bila Zabuni hiyo kufuata taratibu za manunuzi.

Rugemalila na genge lake la mafisadi wanaofukarisha taifa hili kila kukicha wanaendelea kutafuta target ya kumsambaratisha Zitto ili waendelee kuliibia taifa bila kukemewa.

Halafu habari yenyewe,Chanzo chake eti ni Mwana Halisi forums.

Yaani Mwana Halisi inayomilikiwa na viongozi wa Chadema (Kubenea) wanaweza kuwa chanzo cha habari ya kuaminika na ikawa njema kwa Zitto?

Hizi ni tuhuma za kutunga,na ndio maana mara kadhaa tumetahadharisha kuwa huu ushirikiano kati ya baadhi ya viongozi wa Chadema na watu wachafu kama Rugemalila unapaswa kutiliwa mashaka hasa na wazalendo wa mchi hii.

Haya si mahusiano yenye Afya na kamwe hatuwezi kuendelea kuwachekea na kuwaunga mkono.

Vita dhidi ya Ufisadi imemfanya Zitto kupata maadui wengi, Sasa Rugemarila na Kubenea wanashirikiana kupambana na Zitto.

Gazeti la Mawio kila wakiamka hawana habari yoyote zaidi ya Zitto na ACT-Wazalendo.

Kubenea na Anthon Komu wameona nguvu ya kumdhibiti Zitto haitoshi,wameamua kufanya Collaboration na Rugemarila kupambana na Zitto.

Wametunga habari ili kutaka msaada wa Reginald Mengi kwenye hii vita.

Na Mengi bila kufuatilia mmiliki wa Gazeti na Chanzo cha habari (Source) ameamini kichoandikwa.

Tunachoweza kufanya wanyonge wa nchi hii ni kugomea kununua Magazeti yanayoshirikiana na Mafisadi kudhoofisha vita dhidi ya Ufisadi.

Tusinunue gazeti la Mawio,na Taifa imara kutokana na kusaliti Vita dhidi ya Wizi.

Wanyonge bado tunasafari ndefu na tusipoungana aki na Rugemarila watatumaliza na wataendelea kutukejeli kuwa Mil 25 ni pesa za Chai.

Mwobho wewe akili unazo? Mbona watanzania tunakua na ufinyu wa mawazo kiasi hiki? Kila uchwao edo fisadi ukiuliza fafanua ufisadi wake mtu awezi kukwambia zaidi ya fisadi yule,na ndio hivyo hivyo kwa ruge huyu ufisadi wake ni upi? Mtu alilipa kodi na ela iliyobaki alitoa kama ajuavyo mwenyewe,sasa tatizo liko hapa kwa nini tunawaogpa wakubwa waliobeba ela kwa viroba? Tuanze na vyanzo sio hawa wa chini tuache unafiki wa tz jamani
 
simshangai ZZK kulishambulia Mawio kwani hata mwanshalisi lilipofichuwa mipango yake na kafurila kutaka kumpindua Mbatia,aliweka chuki nalo. hawa vijana wanamfahamu zzk inje ndani.
 
Nenda OFISI Yoyote ya Chadema iliyokaribu nawe....

naona unaota chadema tu, sasa mwambien zito ajibu hoja kuu ambayo mawio linatoa, mosi zito kuhus escrow hakufanya lolote kama isingekuwa mbowe kugoma na kusimama pamoja na ukawa, asijitape. pili zito alipunguza idadi ya wabunge 2010 kwa kuwaengua wabunge wa chadema jimbo la pinda na nimrod mkono swahiba wake wapite bila kupingwa. tatu uhujumu aliofanya kwa cdm zito kuanzia pm7, mpaka kwa akina mkumbo ajibu kwanza hizo hoja ajue kila kitu kiko documented, zito zuber kabwe vyanzo vyako vya hela tutaweka hewan muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom