Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,899
944
(1) BARABARA
1a. Musoma-Makojo-Busekera
TANROADS wako kwenye utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami kwenye barabara hili ambalo Serikali imeamua kulijenga kwa awali mbili.

Nimewasisitizia (Mbunge wa Jimbo) kwamba ujenzi unaotafutiwa Mkandarasi uwe wa kuendeleza ujenzi wa Lot 2 (Kusenyi-Makojo-Busekera) ambapo kilomita 5 za lami zilijengwa kwa miaka minne (4)!

1b. Utengenezaji wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera
TANROADS Mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango

(2) KILIMO CHA UMWAGILIAJI
2a. BONDE LA BUGWEMA
*"Consultant" ameanza kufanya "feasibility study" (tarehe 17.9.2023 - 16.10.2023). Nimempa taarifa kwamba nitawatembelea wakiwa kazini Bugwema.

*Mazao makuu yatakayoliwa kwa umwagiliaji ni: mahindi, mpunga, alizeti, dengu, pamba na mboga mboga

2b. BONDE LA SUGUTI
*"Consultant" atafanya "feasibility study" baada ya kukamilisha kazi kwenye Bonde la Bugwema

3. ELIMU
3a. ELIMU YA SEKONDARI - MAABARA
*Tunaendelea na ujenzi wa maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari. Tuendelee kuchangia ujenzi huu na tunashukuru kila mara Serikali inapotuunga mkono kwa michango yake mikubwa

*Halmashauri yetu (Musoma DC) iendelee kukumbushwa kuchangia ujenzi wa maabara 3 kwenye kila Sekondari yetu ya Kata (kwa saa tunazo 25 na tunajenga mpya 5. Sekondari za Binafsi ni 2)

3b. SCIENCE HIGH SCHOOLS
*Tunaendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu muhimu inayotakiwa kwenye uanzishwaji wa science high schools.

*Vinavyohitajika kwa uanzishwaji wa "science high school" ni: maji ya bomba, maabara 3, bweni, na bwalo la chakula.

*Lengo letu ni mwakani, 2024, Jimbo letu liwe na angalau HIGH SCHOOLS 2-3 za masomo ya sayansi. Ile ya Kasoma ni ya masomo ya "arts."

3c. ELIMU YA MSINGI - MRADI WA BOOST
*Shule za Msingi tisa (9) zimepewa jumla Tsh bilioni 1.35 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule hizo.

Wananchi, Mbunge wa Jimbo na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya waendelee kufuatilia mradi huu kwa ukaribu sana.

Shule za Msingi zilizopewa fedha ni: Bugoji, Buira, Bulinga B, Kanyega, Kataryo B, Kigera B, Mabuimerafuru B, Masinono na Nyambono B

4. MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA
4a. Maji ya MUWASA kupelekwa kwenye Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu.

MUWASA inaendelea kukusanya baadhi ya vifaa hitajika kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha.

Vilevile, MUWASA imewasilisha Serikalini Bajeti ya kutekeleza mradi huu

MUWASA imeishaanza kusambaza maji ya bomba kwa baadhi ya maeneo ya kata hizi

Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu kimeanza kupata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la zamani la Mugango-Kiabakari-Butiama

4b. Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Ujenzi umekamilika kwa asilimia 92 (92%) na ifikapo Disemba 2023 kazi zote muhimu zitakuwa zimekamilishwa

4c. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA TEGERUKA
Maji ya bomba kwenye Kata hii yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

Mabomba yametandazwa ndani ya vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kataryo, Mayani na Tegeruka

Tenki la ujazo wa LITA 135,000 tayari linakamilishwa ujenzi kijijini Mayani

4d. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA MUGANGO
Kata hii nayo itapata maji ya bomba kutoka kwenye Bomba la Mugango- Kiabakari-Butiama

Mabomba yamesambazwa kwenye vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kwibara, Kurwaki na Nyang'oma.

*Tenki la ujazo wa LITA 500,000 limejengwa kwenye Mlima Kong'u kijijini Nyang'oma

4e. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA ZA BUSAMBARA NA KIRIBA
Maji ya bomba ya Kata hizi mbili yatatoka kwenye Tenki ya LITA 500,000 liliojengwa Mkimani Kong'u. Maji yake yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

RUWASA imepata vibali vyote hitajika kutoka Serikalini, na ndani ya miezi miwili miundombinu ya usambazaji maji ya bomba ndani ya Kata hizi itaanza kujengwa.

4f. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA BWASI
Vijiji vyote vitatu vya Kiti hii, yaani Bwasi, Bugunda na Kome vinatandaziwa mabomba ya maji

Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 150,000 tayari limekamilishwa Kijijini Bwasi

4g. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VYA CHUMWI & MABUIMERAFURU
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 300,OOO umekamilika kijijini Mabuimerafuru

Mabomba yanaelendelea kutandazwa

Maji kutoka kwenye Tenki hili yatasambazwa kwenye vijiji vya Masinono na Bugwema (Kata jirani ya Bugwema)

4h: MAJI YA KISIMA CHA RUSOLI SEKONDARI
*Tunaendelea kuwashukuru baadhi ya WAZALIWA wa RUSOLI kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hiki.

*RUWASA imekamilisha ujenzi wa Tenki la LITA 75,000 kwa ajili ya usambazaji wa maji kijijini hapo.

5. AFYA
5a. HOSPITALI ya Halmashauri yetu yenye hadhi ya Hospital ya Wilaya imeanza kutoa HUDUMA za AFYA hapo ilipojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.

*Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa sana, ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, Vifaa vya Upasauji, Mitambo ya kutengeneza Oxygen.

5b. VITUO VYA AFYA
*Kwa sasa tuna jumla ya Vituo vya Afya sita (6) ambavyo ni: (i) Murangi, (ii) Makojo (mpya), (iii) Kiriba (mpya), (iv) Kisiwa cha Rukuba (Zahanati yake imepanuliwa), (v) Mugango (Zahanati yake imepanuliwa), na (vi) Bugwema (ilikuwa Zahanati ya Masinono, imepanuliwa)

5c. ZAHANATI
*Tuna jumla ya Zahanati 42
*Zahanati 24 zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu
*Zahanati 14 zinaendelea kujengwa na baadhi karibu zitakamilishwa ujenzi.
*Zahanati 4 za Binafsi zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu.

*Tunaendelea kufuatilia miradi ya usambazaji UMEME vijijini mwetu (REA & TANESCO). Miradi ya REA itaanza hivi karibuni

*Tunaendelea kufuatilia miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara zetu vijijini (TARURA & TANROADS)

*Tunaendelea kufuatilia uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwetu (RUWASA & MUWASA)

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

SHUKRANI
Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na WADAU wengine wa uchangiaji wa Maendeleo na Ustawi wa Jimbo letu wanapewa shukrani nyingi sana - tafadhali endeleeni kutuunga mkono.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 19.9.2023

Prof-Muhongo3-300x300.png
GARI NNE .JPG
picha+tatu.JPG
kkk.png
MUHONGO.jpg
IMG-20180124-WA0003.jpg
 
Huko itakuwa mapicha picha tu, hilo tofali mlilopiga nalo picha sijui mmejengea tope 😎 huko mpaka aende Kassim,
 
Back
Top Bottom