Maji ya Bomba Yaendelea Kusambazwa Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MAJI YA BOMBA YAENDELEA KUSAMBAZWA MUSOMA VIJIJINI

Serikali kwa kupitia RUWASA na MUWASA inaendelea kusambaza maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria kwenda vijijini mwetu.

MUWASA imepewe jukumu la kusambaza maji ya bomba kwenye Kata zilizo jirani na Mji wa Musoma. Kata hizo ni: Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu.

RUWASA inaendelea kusambaza maji kwenye vijiji vyote 68 vya Jimboni mwetu, vikiwemo vijiji vya Kata 4 zilizotajwa hapo juu (ushirikiano wa RUWASA & MUWASA kwa baadhi ya vijiji vya Jimboni mwetu).

Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru Serikali yetu kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwa manufaa ya ustawi wa Jimbo letu na wakazi wake.

CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa inaelezea kazi za MUWASA za usambazaji wa maji ya bomba vijijini mwetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 21.2.2024
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-02-20 at 23.09.10.mp4
    29 MB
Back
Top Bottom