PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,202
- 8,781
Wakuu,
Nimetaarifiwa sasa hivi kwamba mke wa member mwenzetu Freetown ameaga dunia mchana huu saa7.30 kwenye hospitali ya KCMC-Moshi.
Freetown ni member 'legend' hapa majukwaani, na kwa wale waliofika Arusha mwaka jana (27/12/2010) tulipoenda safari ya Tarangire wanapata hisia zaidi juu ya kuondokewa na mkewe kwa huyu member mwenzetu, maana tulikuwa pamoja nae bega kwa bega, na alisafiri na wanae, mabinti wawili.
Mipango ya Mazishi bado haijawekwa wazi, na zaidi inasubiri kuwasili kwa Freetown mwenyewe toka Ughaibuni anakomtumikia mkoloni, na kwa taarifa nilizopewa ni kwamba anatarajiwa kuondoka huko leo usiku, na atawasili kesho alasiri, Mungu akipenda.
Tutajuzana zaidi kinachoendelea, kwa sasa tunachoweza kusema ni kwamba Mungu ailaze pema roho ya Marehemu mke wa Freetown.
Amen.
UPDATE 1:
FreeTown ameondoka usiku wa saa 7.30 mahala anapoishi kuelekea DOHA-QATAR,ambako likuwa aondoke saa 10.00usiku waleo(11/2/2011), lakini bahati mbaya flight aliyoondoka nayo anakoishi imechelewa kwa masaa mawili, hivyo hakuweza kuunganisha connection ya QATAR-AIRWAYS usiku wa leo, NA HIVYO ATALAZIMIKA KULALA HAPO QATAR na leo usiku ndipo atasafiri kwa shirika hilohilo na atafika Dar-JNIA kesho(Ijumaa) saa 7.mchana, na atakuwepo uwanjani hadi saa 12.00jioni, ambapo ndio atapanda Precision Air kuja KIA.
UPDATE 2:
Mulioko Dar mna nafasi kubwa ya kuonana na FT hapo JNIA kesho, maana atakuwepo hapo kwa more than 4 hrs kabla ya kuja Arusha, hivyo kwa watakaopenda kumtafuta tutawapa contact yake mumpate kirahisi.
UPDATE 3:
Marehemu Mrs FT atasafirishwa siku kati ya Jmosi au J'pili kutoka Arusha kuelekea Njombe Iringa, ambako ndiko Domicile Place ya couple hii...
UPDATE 4:
Kesho JUMAMOSI kuanzia saa 3.oo asubuhi IBADA RASMI ya kumwaga marehemu mrs FT itaanza pale nyumbani kwake UsaRiver....NA BAADA ya IBADA hiyo, safari rasmi itaanza saa 7.00 kuelekea IRINGA kwaajili ya kumpumzisha marehemu...na msafafara utawasili huko Jumapili Alfajiri.
Mazishi yatafanyika JUMAPILI,(hakuna kizuizi kwa mujibu wa madhehebu ya Kiluther),na gari iliyopeleka mwili wa marehemu itageuza siku hiyohiyo ya Jumapili jioni!
UPDATE 5🙁12/2/2011...d-day)
Kwa kiasi kikubwa ratiba imezingatiwa.
Mwili uliletwa jana toka KCMC, na ukalala nyumbani kwa FT.
Leo kazi kubwa ilikuwa ni organization tu ya taratibu na jinsi ya kukamilisha heshima kwa shemeji yetu.
Katika ratiba iliyoandaliwa hapo nyumbani, kulikuwa na nafasi ya mwakilishi wa JF kutoa neno, ambapo tumemteua member mmoja aliyetoa SALAMU na hisia zetu kama JF-(Globally).
UPDATE 6:
muda wa saa 12:41 asubuhi hii nimewasiliana na S'Voice akanambia wako junction ya Makambako, na wanapata chai kabisa ili wakifika huko kijijini iwe nishughuli moja tu ya mazishi...
Msafara mwingine wa wanajf ukiongozwa na Maty na FirsLady umeshatangulia mbele, na anakaribia kufika eneo la tukio sasa!
Mikitaboloki Engai Engoitoi(muende salama na Mungu awatangulie)
UPDATE 7 AND FINAL:
Jeneza limeshushwa kaburini mnamo saa 6.30 za mchana, na hivyo kuhitimisha rasmi shughuli na machungu yaliyoandamana na tukio hili lisilo na huruma.
JINA LA BWANA LIBARIKIWE

Katika hali ya kushangaza kidogo,waombolezaji wameomba mwakilishi huyo arudi tena kwenye microphone ili awaeleze kwa ufasaha,
Msafara umeondoka saa 5.20 asubuhi nyumbani kwa FT, kuelekea pande za Iringa...na ka mujibu wa mawasiliano tight tunayoestablish nao, ni kwamba mambo yanaenda vizuri, na wameshafika Moro.JF ni nini,na inafanya nini...hahahaaa!...ilikuwa ishu kidogo!..lakini kiu yao ilikatwa kutokana na maelezo!