Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,092
- 43,265
Mchambuzi,
Pole sana ndugu yangu kwa masahibu haya. Naomba nikupe moyo tu kuwa haya hayaishi na hayatakoma. Tawala mbili zinapogombania mioyo ya watu basi mara zote tawala ambayo inaelekea kushindwa hutumia nguvu zaidi kujipa nafasi. Gaddafi alijaribu sana kuzuia mapinduzi, Assad naye hivyo hivyo na hata Milosevic naye alijaribu sana. Lakini watu wakishaukataa utawala moyoni hakuna risasi wala visu vinavyoweza kulazimisha kinyume chake.
Kama umeamua kuwa huru kifikra na kimtazamo ujue kuwa kuna gharama yake. Gharama hiyo si ndogo na wakati mwingine hulazmisha gharama kubwa zaidi (ultimate price) mtu kulipa. Wapo wengi kabla yetu ambao kutokana na kuamua kuwa huru walijikuta wakilazimishwa kukimbia nchi zao, kuhama familia zao na hata wakati mwingine kuishi maisha ya kujificha ficha ili kupata nafasi ya kupigana tena.
Jambo kubwa na la maana ni kuwa usiwape maadui wako nafasi ya kukunyamazisha; jipange, na hakikisha unakuwa mbele yao maili mia moja! Mwenzako naendelea kusimama si kwa sababu hawakujaribu au kunijaribu; ni kwa sababu nimejitahidi mara zote kuwa mbele yao 1000 miles! So, keep on fighting, reorganize, but never surrender.
NIamini nikisema hivi; watawala waliojeruhiwa hawana msamaha. Kama kuna mtu yeyote anayepigania mabadiliko akidhania kuwa ati akigeuka watamseheme anajidanganya. Hawa watu hawana msamaha so, live free or die trying!