Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Maneno yako ya busara sana, nitajisikia vibaya sana kukupoteza kijana kama wewe, nilitegemea vijana kama wewe wengepongezwa na kuenziwa lakini, dogo CCM imekosa mwelekeo, kwa sasa chama sio salama hata kidogo kiko mikononi mwa majambazi, mijizi, milafi na watenda maovu bila wazi wazi bila aibu, kwa sababu wanajeuri ya pesa na Dora. Kijana tumia busara uko kwenye treni iendayo speed, na umeshoona mbele reli imemeng'olewa unangoja nini ...

Umenena vyema sana, ni bora pia akaweka bayana hao wanaomtishia ni akina nani ili jamii iwatambue kwani hata akitoa taarifa kwa vyombo vya usalama kama polisi hawatafanya lolote la kumsaidia zaidi ya kumbeza kama ambavyo wamewafanyia wengine.
 
Pole sana,
Chukua hatua za haraka za kujihakikishia usalama wako. Baada ya hapo wasiliana na wadau wengine wakusaidie kuwa salama na kuendeleza unayodhani ni azma yako kwa faida ya nchi yako. Karibu Tanzania: Mungu akulinde.

Naona wahanga mnafarijiana! Poleni sana kwa kuwindwa kama ndege.
 
Ndugu wana JF, hasa wadau wenzangu jukwaa la siasa,nimeona kuna umuhimu wa kuwapa tu taarifa kwamba nimepotea kidogo humu ili kujipanga kutokana na vitisho navyokumbana navyo kutokana na michango yangu mbalimbali humu,hasa kuhusiana na misimamo yangu dhidi ya madhaifu ya chama changu cha CCM kuelekea 2015;kwa wengi,naamini watakubaliana nami kwamba lengo langu limekuwa ni kujenga,sasa hawa wachache kwa mtazamo wao ni kwamba nabomoa chama (CCM) kuelekea 2015; vitisho hivi havijaanza leo lakini hivi karibuni,kasi imekuwa kubwa zaidi; mbali ya kupokea vitisho,pia nimedokezwa na vyanzo vyangu vya kuaminika sana kuhusu mpango uliopo wa kunidhuru,hivyo niwe makini hasa in the public arena na nimetajiwa wahusika kwa "majina" na "kitaasisi"!

Ndugu zangu,ningependa kuwahakikishia kwamba pamoja na vitisho hivi ambavyo vinaweza kupelekea mtu kuteswa, kuwa sodomized na hata kuuwawa kijasusi, sitaacha kukipigania chama changu cha CCM kwani nafanya hivyo kwa msukumo wa ninacho kiamini,lakini hasa mapenzi yangu kwa nchi yangu ya Tanzania,na nina amini kwa dhati kabisa matatizo ya sasa ya CCM ni matokeo ya waharibifu wachache ambao watapita tu na kwenda zao na kutuachia chama ambacho ili kirudi katika uimara wake,kitahitaji ujenzi mpya (ndani au nje ya ikulu) wa kuzungumza tena na the common man na kuelewana nae, na hivyo ndivyo tutaweza kuleta ushindani wa kweli dhidi ya chama makini cha chadema au chama chochote kingine; Lakini ni muhimu kwa wana CCM wenzangu tukubali ukweli kwamba sasa ni chama cha watu,sio chama cha viongozi;pia tuwe consistent,tusiwe watetezi wa ccm kutokana na awamu au nani yupo ikulu basi tuwe watetezi wa ccm kutokana na mapenzi yetu ya kwa taifa ambapo chama ni njia pekee ya kuboresha taiga hilo kupitia uongozi;

Vinginevyo CCM kamwe haiwezi kufa lakini pia ni dhahiri kwamba CHADEMA nayo haiwezi kufa,kwahiyo wana CCM wenzangu,hasa vijana wa sasa na wa baadae, tusipoteze muda kwa kujidanganya juu ya hilo; nadhani ni muhimu sasa tufikie level of maturity in liberal democracy na kukubali kwamba CHADEMA is here to stay,and just like sisi CCM, cHADEMA (na wapinzani wengine) wana haki ya kutafuta ridhaa ya wananchi kushika dola ili kuwaongoza kuelekea Tanzania yenye neema; CCM tukifanikiwa kutambua ukweli huu, basi uelewa huu utakuwa ni mwanzo mkubwa sana wa mageuzi makubwa sana ndani ya chama chetu kwani kwanza tunahitaji mageuzi ya fikra;tukiweza hilo, tutaanza kuwa washindani wa hoja badala ya viroja na jazba na hivyo kufanikiwa kurudisha imani ya umma kwa chama chetu ambayo inazidi kuzorota kuelekea 2015; Vijana wenzangu,tuhamie kwenye siasa za hoja mbele ya wananchi zenye outcome ya kupokezana vijiti kwa amani na utulivu kwani hiyo ndio maana ya kukubali demokrasia ya uliberali 1992;kwenye demokrasia nyingi zenye mafanikio, vyama hupokezana uongozi wa nchi kwa amani na utulivu,na anayeshindwa huchukulia hilo kama changamoto ya kujipanga upya;ChADEMA kutushinda CCM uchaguzi ngazi ya udiwani,ubunge na hata urais doesn't mean it is the end na badala yake it should mark a new beginning and an era inayotawaliwa na mapinduzi ya kifikra; Kujiita chama cha mapinduzi sasa iwe na maana ya mapinduzi ya fikra;katika hili,naamini kabisa ndani ya CCM huko Lumumba na kwingineko kwenye nafasi za maamuzi, wapo vijana wenye uwezo to set a precedent kwa wadogo zetu waliopo huko mashuleni,vyuoni n.k,hasa wale ambao bado wana imani na CCM;ni suala la uamuzi tu kwa vijana wana ccm katika nafasi husika,na pia, mshikamano miongoni mwao hasa dhidi ya divisive forces, na vile vile kuweka maslahi ya taifa mbele kabla ya maslahi ya chama; the precedent ni muhimu kwa vijana watakaotufuatia baadae kuja kuimarisha na kugeuza utamaduni wa ovyo na ubabaishaji mkubwa ndani ya CCM ya leo;

Vijana wenzangu,muwe ni wana CCM au wana, CHADEMA...naamini kabisa kwamba wengi wetu lengo ni moja - kuboresha maisha ya watanzania,na iwapo inatokea tunapishana,basi ni juu ya jinsi gani au njia bora zaidi ya kufikia lengo husika; Kama zitto alivyopata nena kwenye kipindi kimoja cha star tv mwishoni mwa mwaka jana,vijana tuna haja ya kuacha kuiga siasa za wazee zilizojaa majungu,fitina na visasi,badala yake tuungane kujenga taifa letu kwa ari mpya,na iwapo tunatofautiana basi iwe kwa hoja juu ya jinsi gani kila chama kinaamini njia ipi ni bota katika kufikia Tanzania yenye neema kwa maslahi ya walio wengi,huku tukiachia wananchi kufanya maamuzi baada ya kuchekecha hoja;

Nahitaji sana sala zenu,

Mungu ibariki Tanzania.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Tatizo la ccm pana watawala hakuna viongozi,watawala lengo lao ni kuendelea kutawala bila kubugudhiwa.Unachokifanya wewe ni chema ktk uongozi lakini ni kibaya katika watawala wa ccm.Ushauri wa bure njoo huku Chadema kwenye viongozi.
 
du!pole mchambuzi....usitishike wala kusita kuusema na kuusimamia ukweli..kwani utakuweka huru...Ni vizuri unawambia hali halisi vijana wenzako ccm...maana wengi wanaishi gizani.. I wish ccm kungekuwa na vijana wenye msimamo kama wako....maana simwoni hata mmoja...wengi wanaishi kwa illusions..wakati wakubwa zao wanaitafuna nchi....
 
Mchambuzi said:
mbali ya kupokea vitisho,pia nimedokezwa na vyanzo vyangu vya kuaminika sana kuhusu mpango uliopo wa kunidhuru,hivyo niwe makini hasa in the public arena na nimetajiwa wahusika kwa "majina" na "kitaasisi"!
Mkuu muda si mrefu wanausalama watakutafuta,wamo humu huwa wanapita naskia.
 
Pole sana Mchambuzi. kwa kweli katika medani ya siasa hakuna mahali salama aslimia mia. Umonnyesha msimamo mzuri tofauti na wengine wanaoikejeli Chadea kwamba itakufa kabla ya 2015.Watanzania wanataka uongozi bora si majina. wanataka maendeleo si propaganda na ahadi hewa.wanataka amani si ugaidi na hujuma. wanataka kuishi si kuuwawa. ifikapo2015 wananchi watakuwa na maamuzi tayari. kila atakae uongzi aanze kujipnaga vema azichange kaata zake vizuri nafasi ipo kidogo...
 
fanya haraka kuwataja kabla CDM hawajakuteka
 
Mungu akupe Nguvu, na kukulinda na Wabaya wote, wapate kushindwa, upate kulitumikia Taifa letu kwa moyo na uzalendo wote, uushinde udhalimu, uoga na majaribu yote.
Kikubwa umweke Mungu Kwanza.

Ndugu wana JF, hasa wadau wenzangu jukwaa la siasa,nimeona kuna umuhimu wa kuwapa tu taarifa kwamba nimepotea kidogo humu ili kujipanga kutokana na vitisho navyokumbana navyo kutokana na michango yangu mbalimbali humu,hasa kuhusiana na misimamo yangu dhidi ya madhaifu ya chama changu cha CCM kuelekea 2015;kwa wengi,naamini watakubaliana nami kwamba lengo langu limekuwa ni kujenga,sasa hawa wachache kwa mtazamo wao ni kwamba nabomoa chama (CCM) kuelekea 2015; vitisho hivi havijaanza leo lakini hivi karibuni,kasi imekuwa kubwa zaidi; mbali ya kupokea vitisho,pia nimedokezwa na vyanzo vyangu vya kuaminika sana kuhusu mpango uliopo wa kunidhuru,hivyo niwe makini hasa in the public arena na nimetajiwa wahusika kwa "majina" na "kitaasisi"!

Ndugu zangu,ningependa kuwahakikishia kwamba pamoja na vitisho hivi ambavyo vinaweza kupelekea mtu kuteswa, kuwa sodomized na hata kuuwawa kijasusi, sitaacha kukipigania chama changu cha CCM kwani nafanya hivyo kwa msukumo wa ninacho kiamini,lakini hasa mapenzi yangu kwa nchi yangu ya Tanzania,na nina amini kwa dhati kabisa matatizo ya sasa ya CCM ni matokeo ya waharibifu wachache ambao watapita tu na kwenda zao na kutuachia chama ambacho ili kirudi katika uimara wake,kitahitaji ujenzi mpya (ndani au nje ya ikulu) wa kuzungumza tena na the common man na kuelewana nae, na hivyo ndivyo tutaweza kuleta ushindani wa kweli dhidi ya chama makini cha chadema au chama chochote kingine; Lakini ni muhimu kwa wana CCM wenzangu tukubali ukweli kwamba sasa ni chama cha watu,sio chama cha viongozi;pia tuwe consistent,tusiwe watetezi wa ccm kutokana na awamu au nani yupo ikulu basi tuwe watetezi wa ccm kutokana na mapenzi yetu ya kwa taifa ambapo chama ni njia pekee ya kuboresha taiga hilo kupitia uongozi;

Vinginevyo CCM kamwe haiwezi kufa lakini pia ni dhahiri kwamba CHADEMA nayo haiwezi kufa,kwahiyo wana CCM wenzangu,hasa vijana wa sasa na wa baadae, tusipoteze muda kwa kujidanganya juu ya hilo; nadhani ni muhimu sasa tufikie level of maturity in liberal democracy na kukubali kwamba CHADEMA is here to stay,and just like sisi CCM, cHADEMA (na wapinzani wengine) wana haki ya kutafuta ridhaa ya wananchi kushika dola ili kuwaongoza kuelekea Tanzania yenye neema; CCM tukifanikiwa kutambua ukweli huu, basi uelewa huu utakuwa ni mwanzo mkubwa sana wa mageuzi makubwa sana ndani ya chama chetu kwani kwanza tunahitaji mageuzi ya fikra;tukiweza hilo, tutaanza kuwa washindani wa hoja badala ya viroja na jazba na hivyo kufanikiwa kurudisha imani ya umma kwa chama chetu ambayo inazidi kuzorota kuelekea 2015; Vijana wenzangu,tuhamie kwenye siasa za hoja mbele ya wananchi zenye outcome ya kupokezana vijiti kwa amani na utulivu kwani hiyo ndio maana ya kukubali demokrasia ya uliberali 1992;kwenye demokrasia nyingi zenye mafanikio, vyama hupokezana uongozi wa nchi kwa amani na utulivu,na anayeshindwa huchukulia hilo kama changamoto ya kujipanga upya;ChADEMA kutushinda CCM uchaguzi ngazi ya udiwani,ubunge na hata urais doesn't mean it is the end na badala yake it should mark a new beginning and an era inayotawaliwa na mapinduzi ya kifikra; Kujiita chama cha mapinduzi sasa iwe na maana ya mapinduzi ya fikra;katika hili,naamini kabisa ndani ya CCM huko Lumumba na kwingineko kwenye nafasi za maamuzi, wapo vijana wenye uwezo to set a precedent kwa wadogo zetu waliopo huko mashuleni,vyuoni n.k,hasa wale ambao bado wana imani na CCM;ni suala la uamuzi tu kwa vijana wana ccm katika nafasi husika,na pia, mshikamano miongoni mwao hasa dhidi ya divisive forces, na vile vile kuweka maslahi ya taifa mbele kabla ya maslahi ya chama; the precedent ni muhimu kwa vijana watakaotufuatia baadae kuja kuimarisha na kugeuza utamaduni wa ovyo na ubabaishaji mkubwa ndani ya CCM ya leo;

Vijana wenzangu,muwe ni wana CCM au wana, CHADEMA...naamini kabisa kwamba wengi wetu lengo ni moja - kuboresha maisha ya watanzania,na iwapo inatokea tunapishana,basi ni juu ya jinsi gani au njia bora zaidi ya kufikia lengo husika; Kama zitto alivyopata nena kwenye kipindi kimoja cha star tv mwishoni mwa mwaka jana,vijana tuna haja ya kuacha kuiga siasa za wazee zilizojaa majungu,fitina na visasi,badala yake tuungane kujenga taifa letu kwa ari mpya,na iwapo tunatofautiana basi iwe kwa hoja juu ya jinsi gani kila chama kinaamini njia ipi ni bota katika kufikia Tanzania yenye neema kwa maslahi ya walio wengi,huku tukiachia wananchi kufanya maamuzi baada ya kuchekecha hoja;

Nahitaji sana sala zenu,

Mungu ibariki Tanzania.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wataje hadharani, la sivyo itakuwa kama unapoteza muda. Threads zako za muungano na kundi la ujamaa CCM pamoja na kucriticize CDM na CCM ... vitisho vinaweza kutoka sehemu mbalimbali.

Cha muhimu zaidi ni kuwaangalia walio karibu na wewe ... usiangalie mbali.
Mkuu umemsoma vyema lakini?
mbali ya kupokea vitisho,pia nimedokezwa na vyanzo vyangu vya kuaminika sana kuhusu mpango uliopo wa kunidhuru,hivyo niwe makini hasa in the public arena na nimetajiwa wahusika kwa "majina" na "kitaasisi"!
 
Pole kijana, sioni kama watu wanafanya siasa ndani ya ccm zaidi ya vitisho tu, haya ndo aliyochaguliwa nayo kinana?
 
Hapa li-KOVA na mimacho yake yote JF. Kesho utasikia anasema CHADEMA.
 
Hao wanaokutishia waweke hadharani ili kuwapunguza kasi ya utekelezaji na badala yake waanze kujipanga upya. Mchawi mpe mtoto alee, peleka taarifa polisi. Peleka maelezo yako pia kwa Hellen Kijo Bisimba na mwisho ujisaimishe kwa amiri jeshi. Yawezekana ukapata rehema yake akakulinda sambamba na vijana wake wa kazi. Unaweza ukaona ninakushauri mambo ya kuchosha lakini gharama zake ni ndogo kuliko maisha yako.
 
Jamii yetu inadanganyika kirähisi sana.
Critical thinking haipo kabisa!!!
Ndio maana misururu ya wagonjwa ilijaa Loliondo...

Chifu, misisuru hiyo ilifunguliwa na kaka mkuu, alijifanya yupo mapumzikoni, lakini akaamua kwenda 'kudanganyika' na kikombe cha jero.
Kaka mkuu mjanja sana, alitumia ukaribu wa Olduvai Gorge na Samunge kutokomea kwenye kikombe bila raia wengi kujua.

Baada yake, misusuru ya mawaziri (Lukuvi, Magufuli n.k.) vigogo wa polisi, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge n.k. ilionekana.

Katika hilo chifu ZeMarcopolo nakubaliana nawe. Ni hatari kwa taifa kuongozwa na viongozi wasio critical thinkers, wanaodanganyika kwa kikombe cha jero.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu Mchambuzi kwa hivyo vitisho unavyopewa. Tunakuombea usalama. Wewe ni mmoja kati ya vijana wachache ambao ninawakubali kwa kusimamia ukweli na kuwa na mapenzi ya kweli kwa nchi yetu ya Tanzania.
 
Chifu, misisuru hiyo ilifunguliwa na kaka mkuu, alijifanya yupo mapumzikoni, lakini akaamua kwenda 'kudanganyika' na kikombe cha jero.
Kaka mkuu mjanja sana, alitumia ukaribu wa Olduvai Gorge na Samunge kutokomea kwenye kikombe bila raia wengi kujua.

Baada yake, misusuru ya mawaziri (Lukuvi, Magufuli n.k.) vigogo wa polisi, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge n.k. ilionekana.

Katika hilo chifu ZeMarcopolo nakubaliana nawe. Ni hatari kwa taifa kuongozwa na viongozi wasio critical thinkers, wanaodanganyika kwa kikombe cha jero.

Chief hii na usalama wa Mchambuzi unahusiana vipi?

Wengine maneno yenu yanauzito humu msihamanike kuandika bila kueleweka wengine tukajitafsiria tu!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Mkuu ujichunge sana na pia kuacha kabisa matembezi ya usiku ukiwa peke yako.
au ikibidi kutoka usiku awe anachukua kabisa dawa ya ganzi na wembe wa kukatia kucha!!natania
 
Back
Top Bottom