Ndugu wana JF, hasa wadau wenzangu jukwaa la siasa,nimeona kuna umuhimu wa kuwapa tu taarifa kwamba nimepotea kidogo humu ili kujipanga kutokana na vitisho navyokumbana navyo kutokana na michango yangu mbalimbali humu,hasa kuhusiana na misimamo yangu dhidi ya madhaifu ya chama changu cha CCM kuelekea 2015;
kwa wengi,naamini watakubaliana nami kwamba lengo langu limekuwa ni kujenga,sasa hawa wachache kwa mtazamo wao ni kwamba nabomoa chama (CCM) kuelekea 2015;
vitisho hivi havijaanza leo lakini hivi karibuni,kasi imekuwa kubwa zaidi; mbali ya kupokea vitisho,pia nimedokezwa na vyanzo vyangu vya kuaminika sana kuhusu mpango uliopo wa kunidhuru,hivyo niwe makini hasa in the public arena na nimetajiwa wahusika kwa "majina" na "kitaasisi"!
Ni wale walee!.. Wanaowaueni na kuwatesa nyie wanyakyusa!.. Kumbuka waliomtesa ULIMBOKA!.. Waliomtesa KIBANDA,... Waliomtilia sumu MWAKYEMBE!... Waliomuua MWANGOSI!... waliomtenda Prof MARK MWANDOSYA!... Waliomuua prof JUAN MWAIKUSA!... waliomuua MWAIKAMBO!... na sasa kazi inaendelea!!!!!!!!... Hivyo si vitisho JIHADHARI!... Lisemwalo lipo kama halipo LAJA!...
Watuhumiwa mpaka leo hawajakamatwa!.. Aliyemuua MWANGOSI anapelekwa mahakamani na gari la kifahari kama mfalme (SI KARANDINGA LA MAGEREZA) na kulindwa na polisi si maafisa magereza!... Hii ndiyo Tanzania yetu NCHI YA AMANI!