Taarifa muhimu kwa Umma, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro atakutana na mwenzake wa Msumbiji leo Mkoani Mtwara

Hao ni wanasiasa tu hawana lolote
Waliwahi kuwa na kikao Kama hicho miaka miwili iliyopita na hakuna walichofanya
 
Kamanda Sirro & Amiri Jeshi Mkuu wa sasa (Raisi Magufuli) wajitahidi wawatokomeza hao magaidi, wasipowamaliza huko mbeleni (future) watarudi/au kusogea/au kuingia Tanzania

Boko Haram walianzaga hivyo hivyo, walikuwa Nigeria pekee, lakini leo hii wame-expand na kuwa katika nchi kama 3 (Nigeria, Chad, & Cameroon)

Wanaweza wakwaitwa Mtwara then waka expand kuelekea wilaya za Tunduru & Namtumbo, pia wakawa wana expand kuelekea mkoa wa Lindi, then mkoa wa Pwani (wilaya za Rufiji, Kibiti, & Mkuranga)
Vikundi vyote vya kigaidi ni attention seekers, hao dawa yao ni kuwakamata mmoja mmoja bila kuwapiga mkwara. Ukipiga mkwara tu wanapata Air time kwenye media, lengo lao linatimia.
 
katika hili niko pamoja na sirro

ukweli ni kwamba hili janga la msumbiji ni tishio pia kwa tanzania.Msumbiji waruhusu vikosi vya Tanzania to operate ndani ya msumbiji ili kuwaondoa hao magaidi kama ilivyokuwa KIBITI.....
Hata kwa kuchangishana hela tuwe tayari kuhakikisha vikosi vyetu vinakuwa well equipped
Pia Military intelligence ni muhimu sana ikiwa usalama wa Taifa umeshindwa kutoa data za uhakika na sisi wanainchi yatupasa kutoa taarifa ya kila mwenendo tunaoutilia shaka.

Ni kweli tuna vikosi vizuri ila bila sisi wanainchi tunayoyapita hayo mapori kila wakati kusaidia kutoa taarifa kazi itakuwa ngumu sana
msumbiji wamekodisha mpaka askari kutoka ufaransa lakini imeshindikana
 
Sirro embu waingize wale jamaa ambao hua wanaingiaga uwanja wa taifa kwa kurukaruka na mibegi mgongoni na mitutu wakati wa sherehe za kitaifa wafanye shuhuli hapo chap wamalize hao wapuuzi vigaidi
 
Back
Top Bottom