Ruvuma: Polisi Kata wanolewa juu ya uandaaji na utumaji wa Taarifa za Wahalifu na uhalifu kwa njia ya Mtandao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Kamisheni ya Polisi Jamii, Novemba 15, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Saccos uliopo Kata ya Majengo, Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma limeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo Polisi Kata namna ya uandaaji na utumaji wa taarifa za wahalifu na uhalifu Kwa kutumia Mfumo wa Kielektroniki (DIGITALIZED EARY WARNING SYSTEM).

Mafunzo hayo yameendeshwa na timu ya Wataalamu kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kupitia Kamisheni ya Polisi Jamii wakiongozwa na Mrakibu wa Polisi (SP) Dkt. Ezekiel Kyogo akiambatana na Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Robert Knox na Mkaguzi wa Polisi (INSP) Danis Mnyambwa kutoka Tehama Kuu Dodoma.

Akifungua mafunzo hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Marco Chilya amewataka Polisi Kata kuhakikisha wanasikiliza kwa makini yale yote watakayofundishwa juu ya uandaaji na utumaji wa taarifa za wahalifu na Uhalifu kwa njia ya mtandao na kuyatumia mafunzo hayo katika utendaji wao wa kazi za kila siku ili kutimiza lengo la Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP, Camillus Wambura na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
55.JPG

5.JPG

3.JPG
Aidha, Mrakibu wa Polisi (SP) Dkt. Ezekiel Kyogo amesema kuwa mafunzo hayo ni endelevu hivyo Jeshi la Polisi kupitia Kamisheni ya Polisi Jamii litaendesha mafunzo hayo kwa Mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara na Zanzibar na kuwataka askari waliobahatika kuhudhuria mafunzo hayo wawe mabarozi Kwa kuwafundisha wenginge ili kufikia lengo lililokusudiwa.

Kamanda Chilya kupitia kwa wawezeshaji wa mafunzo hayo alimshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji Polisi Kata katika utoaji wa huduma na kurahisisha utendaji kazi, Pia alishukuru Kwa kupatiwa vifaa ambayo ni kompyuta mpakato na simu janja ambazo zitaenda kusaidia katika mfumo wa utumaji wa taarifa wa kielektroniki waliofundishwa na wataalamu hao.
 
Back
Top Bottom