Nakubali mtumishi,
Pombe inaweza kukufanya usahau kwa muda, lakini haiwezi kuondoa sababu iliyokufanya uumie. Usiku unaweza kulewa ukasahau, lakini asubuhi ukiamka, tatizo bado lipo. Kileo kinapokwisha, maumivu yanaweza kurudi. Ndiyo maana dawa ya kweli si kukimbia maumivu kwa pombe, bali kumrudia Yesu na kumkabidhi mzigo wako. Pombe inaweza kuzima hisia kwa muda Yesu ndiye anayebadilisha moyo na kukupa nguvu ya kukabiliana na maisha.
Mithali 31:6–7 haisemi kwamba pombe ndiyo dawa ya kudumu ya huzuni, inaeleza matumizi ya kileo kwa mtu mwenye uchungu ili kwa muda asikumbuke taabu yake.