Ni muda sasa umefika makanisani kuwe na bar ndogo za kunywa pombe, waumini wanywe pombe kusuuza nafsi,

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Exception ni wakristo wachache sana kama wasabato wanaoamini bado Mungu huchukizwa na Pombe.

Hata ma askofu wakati wa misa hunywa mvinyo takatifu mbele ya macho yetu, sioni ubaya wowote kuwe na min bar makanisani kwajili ya waumini

1696709646147.png


Makanisani kuwe na bar ndogo ila kuwe na sheria mtu apige chupa mbili ama tatu ili awe katika kundi la mywaji (kulewa kidogo) na si mlevi.

Alafu kitu kizuri zaidi ni kwamba makanisa huwa yana misamaha ya kodi na tozo, si hivyo tu lakini pia wanaweza kuuza bila faida, hii itafanya bei iwe rahisi kuliko hata kwenye kambi za jeshi.


Agano la kale lilishapitwa na wakati kwa dini zinazoamini Mungu hachukizwi na Pombe, si pombe tu hata sheria za wanyama wa kula zilishapitwa na wakati watu wanagonga kitimoto, Hata sheria za agano la kale kuhusu mavazi zilishapitwa na wakati sikuhizi makanisani kawaida kukuta mwanamke kavaa suruali ama gauni linamchoresha hips, mapaja na makalio.


Mithali 31:6 -7

Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.

Ukiona maada hii imekuchukiza kwa kuona labda nadhihaki imani yako, jiulize mwenyewe "ni kwanini namuona mtoa post kanidhihaki wakati kashauri pombe iliyoruhusiwa na kanisa iwepo kanisani ?" ikiwezekana jipigie makofi kwa kupata akili ya kutambua kwamba Pombe ni chukizo kwa Mungu,
 
Makanisani kuwe na bar ndogo ila kuwe na sheria mtu apige chupa mbili ama tatu ili kukidhi kigezo cha kuwa mnywaji na sio mlevi.

Kanisa liwe sehemu ambayo waumini wawe na amani na wafurahi, Pia kwa wale wenye shida waweze kupunguza mawazo maana biblia agano jipya imeruhusu hata maskini kunywa pombe kupunguza mawazo,

Agano la kale lilishapitwa na wakati, Mungu alichukizwa na unywaji wa pombe lakini agano jipya limetupa uhuru,
Naunga mkono hoja, pamoja na nyama choma kitimoto na huku mziki laini, Bwana asifiwe🤣🤣🤣
 
Makanisani kuwe na bar ndogo ila kuwe na sheria mtu apige chupa mbili ama tatu ili kukidhi kigezo cha kuwa mnywaji na sio mlevi.

Kama mtu ni mnywaji ni bora aruhusiwe kustua mbili ama tatu kwenye bar ya kanisa kisha aingie kanisani akiwa mwepesi

Agano la kale lilishapitwa na wakati, Mungu alichukizwa na unywaji wa pombe lakini agano jipya limetupa uhuru hata masikini kahamasishwa anywe pombe kupunguza mawazo.
Labda wakatoliki ndio wataweza
 
Back
Top Bottom