Symbion Power acquires DOWANS Power plant

Hii ndo kusema kuwa mali haramu iko kwenye mchakato wa kutakatishwa na kufanywa kuwa mali halali! Kazi kweli kweli!
 
sioni tofauti kati ya symbion na makampuni mengine yaliyoitapeli TANESCO. Kwanini mkataba huu unakwenda haraka kiasi hiki na kwanini serikali isitafakari mbinu nzuri ya kutatua swala la umeme, kila kukicha utasikia hiki na mwisho utasikia mkataba feki. Hili ni balaa lingine linainyemelea TANESCO
 
Kuna tofauti kubwa kama mwanga ulivyo na tofauti na giza. Maswali yaliyopo yanahitaji kujibiwa katika majadiliano. Hadi hivi sasa hili ni suala la Symbion na Dowans.. nasubiri litakapokuwa Symbion na Tanesco..

Unasubiri ili iweje? uanze ufataani?
 

:sick:
 

Sijui ujuha wa Watanzania utaisha lini? Huyo Mkurugenzi anajua kazi anayoifanya hapo TANESCO? Kwanini TANESCO isiwe mali ya Songas kama asilimia 70% ya mapato yake yanakwenda Songas? Hata hao wajumbe wa Kamati ya Madini ni wasanii kwasababu mikataba ya aina hiyo ya TANESCO wanaijua vizuri na hayo ni matokeo. Kama hawakuwa na muda wa kukabiliana na hali hiyo katika hatua za kuingia mkataba, leo wanapiga kelele za nini?
 
Hii ni sawa na kuwa na mke Chuma kisha njemba ikaopoa na kupiga mkeo kiulaini. Ukitaka kufungua mdomo unapigwa kiCorola na mshiko wa 10M Keshi. Baada ya hapo jamaa anaanza kupiga mkeo kama vile wake huku wewe umevunja kisambusa na kukenua kwa sana kwenye kikolola chako kikuukuu.
Serikali ya CCM inapigwa kiulaini mbele yakadamnasi ya wana CCM wote na Vidume wa Dowans. Viongozi wote wa CCM wameinama huku wameshika Mabampa ya VX na GX huku wakikenua.

Sijui Symbiosys sijui Dowans MMMH! Chama namba 1 kimeinamishwa.
 
Rais ana gundu period!
kama hatujalielewa hilo tutaendelea kumtafuta mchawi hatutampata.

Suluhisho liko mikononi mwa nguvu ya umma period
 
From Richmond to DOWANS TO Symbion...what next?
 

Of course kwenye biashara kuna kila mbinu, kila mtaji unapokuwa mkiubwa na ndio mbinu za kibiashara zinakuwa kubwa. Wafanya biashara wakubwa na waliofaulu vyema kwenye biashara zao, hutegemea sana intelijensia za kibiashara, mahusiano na watu aina na kada mbalimbali, kunusa harufu ya faida na hasara mapema, uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka.

Hivi katika vigezo hivyo vyote, ni mfanya biashara yupi atatumbukiza kiwango kikubwa cha fedha bila kuwa na intelijensia zilizomfanya aamue kutumbukiza fedha yake? Leo hii hata ukitaka kwenda machungwa toka muheza, kama hujatazama bei ya soko, kama hujatazama usafiri wa uhakika, kama hujatazama ni nani au wapi ukiyafikisha yatanunuliwa kwa haraka na kwa faida nzuri, basi utakuwa unacheza mchezo wa pata potea na hufanyi biashara.

Kwa mantiki hiyo, Symbion, wameyafanya yote kabla na ndio maana wanaingia katika hii biashara. Na kama hawajafanya hivyo watakuwa si wafanya biashara.
 
Duh!!!,nilifikiri hili muvu lilishamalizika kumbe bado kinaendelea!!!?wakubwa endeleeni na kamchezo kenu wananchi wa Tanzania bado ni wajinga huwa wanaishia kupiga kelele weeeeeee!!!!bila vitendo na kiukweli ni wapole na shida ni sehemu ya maisha Yao ya kila siku hivyo wawekezaji karibuni na muendelee kuwateka viongozi wao akili na kujichukulia madini bila kelele.Hamuoni Serikali inavyowatetea nyie wawekezaji embu ona huko Nyamongo mmeshawaua wananchi wao na wao Serikali nao wameongeza idadi baada ya kuwaua watano,,,wawekezaji karibuni katika SHAMBA LA BIBI sababu WATANZANIA BADO WAMELALA USINGIZI MZITO.
 
Kuna tofauti kubwa kama mwanga ulivyo na tofauti na giza. Maswali yaliyopo yanahitaji kujibiwa katika majadiliano. Hadi hivi sasa hili ni suala la Symbion na Dowans.. nasubiri litakapokuwa Symbion na Tanesco..

Mkuu heshima mbele,
Itakapofikia suala hilo kuwa la Symbion na Tanesco na hapo ndo tutakuwa tayari tumeshaliwa.
Ashakum, ni sawa na kumuona binti yako anarukaruka mitaani unasema hiyo haina tatizo nasubiri atakapopata mimba ndo ntathibitisha kuwa ni kweli.
Kwa taarifa tu ni kuwa tayari Tanesco imesema mkataba kati yake na Symbion utasainiwa muda wowote ndani ya wiki mbili kuanzia jana.
 
Ndio wametambua kuwa serikali ya CCM ina mijitu mipuuzi,yenye mizaha, miroho ya pesa na isyo na chembe za uzalendo. Wakafanya simple logical analysis kwamba kama kikampuni uchwara hewa cha mfukoni kama Richmond kiliwahi kupata nafasi kuvuna pesa za watanzania kikachomoka, kikaja kingine nacho cha mfukoni na kitapeli, DOwans kikavuna weee,kikaingia mpaka chumbani ikulu; Logical table ikaonesha faida ni TAUTOLOGY. Kwanini wasije?
Mbaya zaidi ni kuwa kuna vijitu miongoni mwa hao wanaoliwa fedha zao, kwa kudanganywa na vipesa,na tuvyeo...wanayashangilia hawa majizi na kuyaita MAJASIRIAMALI!
 
Asante sana Mwanakijiji ingawa hatujasikia kipengele cha Tarime
 
RICHOMD=<DOWANS=<SYMBION THE SHOW GOES ON -LUPE FIASCO
The Show Goes On"

[Chorus x2:]
Alright, already the show goes on
all night, till the morning we dream so long
anybody ever wonder, when they would see the sun up
just remember when you come up
the show goes on!
 

hapo kwenye red ndo kwenye shughuli nzima......uhakika wa soko, faida, usalama wa biashara, insurance, mikopo ya fasta N.K
ila naomba kuuliza, hii mitambo si ilikuwa imewekwa collateral benki ya stanbic na barclays ambako dowans walivuta hela??? sasa Symbion wameingia kwa style gani hapo??? kwakweli maswali ni mengi na majibu ndo yanachanganya kabisa!
 
Tanesco wizi mtupu, au huyajui mashirika ya umma? kwani yote yamekufa kwa nini? si ufisadi wa wafanyakazi wa hayo mashirika.
Mashirika ya uma yako chini ya nani Fauzia??? sio serikali?? serikali ni mwajiriwa wa nani Fauzia??? sio wa wananchi???? wananchi ni akina nani sasa?? sio mimi na wewe na yule?? sasa lawama abebe nani kama sio sisi wenyewe tunaokaa kimya pamoja na kuona maovu yote haya?
 

Mkuu,
Vua hilo shati, vaa gwanda la khaki halafu tafuta kadi yenye rangi tatu na alama ya vidole viwili vinavyojenga alama ya Vee shinani.
 
Mzee Mwanakijiji,
Shukran sana mkuu wangu na shukran zaidi zimfikie Dr.Slaa ambaye kaniacha najiuliza maswali mengi sana kuhusu Uongozi wa CCM..
Hivi kwa nini ni rahisi sana kuwapata viongozi wa juu wa Chadema ktk mahojiano kuliko viongozi wa CCM na hata kama wakijitokeza huongea kwa jazba na vitisho badala ya kuwaelimisha wananchi?..

Halafu ningewaomba sana kina Mnyika na Zitto ambao ni wachama wa JF toka miaka, warudi kijiweni maana toka dogo amekamata madaraka haonekaniki ila tu kwa matakwa ya kurusha habari zake. Na Uongozi wa Jf ujaribu kuwafikia zaidi viongozi wa ngazi za juu wa CCM wapate kushiriki kikamilifu kama wanachama ili nasi tujenge maandamano na mikutano ya kuelimishana/kufahamishana hapa JF..Nadhani Jf inaweza kupeleka mialiko kwa wabunge wote wa Jamhuri kupitia e-mail, Tweet au facebook..

Ningependa sana kuwasikia viongozi ngazi zote wakijumuika nasi hasa ktk maswala magumu ya Katiba, Muungano, Kilimo kwanza, Ajira, Miundombinu na hadi zote ambazo naweza ziweka ktk fungu la Uchumi na jinsi gani tunaweza kupambana na UFISADI..Na ningekomba sana swala la Ufisadi litangaziwe vita ya kitaifa.

Maadam JK amewapa nafasi CCM kuwataja Mafisadi wazi na kuahidi wanachama kulishughulikia basi inabidi Kitaifa nako wabunge wetu walifikishe bungeni na kudai sheria ya kupambana na adui huyu kitu kama - PATROIT ACT.. Uzalendo unatakiwa kupiga vita Ufisadi na sheria itungwe kama ile ya Bush kupambana na Magaidi (Terrorist).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…