Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,019
- 580
Mh! Kweli tunachezewa akili zetu. Vila ngozi wetu!!!
kuna kazi tena hapo
mama kasifia mitambo ya Dowans kwamba ipo safi na ni ya kisasa,kwa maana hiyo hatuwezi kuruka chochote kile kitakachotokea kiwe kizuri ama kibaya
natoka nitarudi baadae
Kama ni hivyo basi TANESCO inunue hiyo mitambo,( tule matapishi tuishi) sheria ya manunuzi si ilibadilishwa bungeni!!!!!! Ili at least tubebe mzigo kwa mara moja kuliko kurudia rudia, maana hili ndugu yangu tumeisha livaa hatuna jinsi, njia ya kutokea ni kununua mitambo period!!!!!!Bongo tambarare! Mitambo hii iliyosifiwa na Clinton ni ile mitambo ya Dowans/Richmond iliyopigiwa kelele sana na wabunge wengi na baadhi ya mashabiki wa kisiasa Tanzania. Kinachotumaliza Tanzania ni ushabiki wa kisiasa hata katika vitu vyenye kuleta tija kwa taifia. Sasa ngoja tusikie yule atakayepiga kelele tena kama hajaambiwa wewe America, UK, Canada, etc hapana kanyaga.
Nadhani chuki za wanasiasa wa CCM ya wao kwa wao imetupelekea tuwe hapa tulipo leo. Hii pia inachangiwa na vyombo vyetu vya habari ambao nao wanaandika taarifa za kinafiki bila kufanya utafiti yakinifu na kutoa majibu ya utafiti hadharani. Nyingi utasoma tu kwa habari toka chanzo chetu, wakati mwingine unakuta mwandishi anatoa maono yake tu lakini ili ionekane habari anaandika as if kuna source.
Naunga mkono kuwashwa kwa mitambo hiyo ya Dowans kupitia Symbion na nasihi Tanesco wanunue umeme watuwekee kwenye gridi ili kupunguza huu mgao ambao kwa sasa hautangazwi lakini upo kwa sana. Kwa wanaoishi Kinondoni, M/Nyamala, K/Nyama na hata Sinza ni mashahidi kuwa mgao unaendelea kinyemela bila kutangazwa.
CCM na mipasuko ya viongozi wako wa roho wa madaraka ndiyo iliyotufikisha hapo. Hamuwezi kuwa wote mawaziri wakuu kwa wakati mmoja wala huwezi kuwa spika na waziri mkuu hapo hapo haiwezekani. Haiwezekani wote mkawa "mediocres" katika performance lazima kuna wanaofanya kazi zaidi na kama Mwenyekiti hataki kufanya kazi anaogopa sana mdogo wake anayefanya kazi kwa speed.
Haiwezekani ukapendwa na kila mtu kama unafanya kazi....ukiona unapendwa na kila mfanyakazi wakati wote (all the time) ukiwa bossi basi ujue kuwa hufanyi kazi bali umewaachia wafanyakazi wako mwanya wa kuiba, kutega na kueneza umbea katika organisation.
Tunahitaji tusimamie maamuzi yetu hata kama tulikosea sehemu fulani tunajifunza na kwenda mbele. "practice makes you perfect".
I love Tanzania, Mungu utusaidie Watanzania tufungue macho na tujue tuchohitaji. Hatuhitaji watawala bora au watakatifu...tunahitaji viongozi wenye thubutu ya kusukuma gurudumu letu mbele hata kama mbele bila kujali kuna mlima kiasi gani mbele au kuna urefu gani. Hata maili elfu zilianza na hatua moja.....
Kama ni hivyo basi TANESCO inunue hiyo mitambo,( tule matapishi tuishi) sheria ya manunuzi si ilibadilishwa bungeni!!!!!! Ili at least tubebe mzigo kwa mara moja kuliko kurudia rudia, maana hili ndugu yangu tumeisha livaa hatuna jinsi, njia ya kutokea ni kununua mitambo period!!!!!!
"Ujasiri wa kifisadi" unaelekea umezidi mipaka, wasiwasi wangu ni mmoja ...how the history will document these creatures known as Tanzanian!! Miaka 100 ijayo huenda binadamu wengine wasiamini kama kulikuwa na binadamu mbali na miti na wanyama katika eneo hili la dunia!wisdom seeds nataka nikuulize swali moja,
je huyu mama clinton anajua kuhusu hiyo sinema?
wisdom seeds nataka nikuulize swali moja,
je huyu mama clinton anajua kuhusu hiyo sinema?
"Ujasiri wa kifisadi" unaelekea umezidi mipaka, wasiwasi wangu ni mmoja ...how the history will document these creatures known as Tanzanian!! Miaka 100 ijayo huenda binadamu wengine wasiamini kama kulikuwa na binadamu mbali na miti na wanyama katika eneo hili la dunia!
Na ndiyo maana mama Hilary Clinton kaahidi kuzidisha umeme mara tatu mpaka 2015 kazi iliyotushinda kwa miaka zaidi ya 30!!
mbona 2meshalia sana hawa majamaa nimakatili balaa alianza mmoja kutubaka yaani Richmond 2kalia sana lakin wap sasa wameamua kutula mande.. . .jamani 2hurumie nyie wabakaji hadi 2toe damu ndo mtarizika. . . . .Watanzania tutaendelea kubakwa hadi tutakapolia, "tunaumia!"
wewe ni muandishi mzuri "script nzuri", sasa hapo hapo kuipendezesha sinema hii Hilary anatembelea mitambo ya Symbion na kubariki hiyo, tunasubiri kifuatacho....