Symbion Power acquires DOWANS Power plant

Symbion Power acquires DOWANS Power plant

mimi siioni.

Cheap politics!

1.wale wengine walikuwa waislamu na symbion ya wakristo.
Ni lini na wapi wananchi waliikataa dowans kwa sababu za kidini? Kwanza nani wamiliki wa Dowans maana hata Rais wetu hawajui?

2. nini tofauti kati ya dowans na symbion - Kwa zaidi miaka 5 na ushee, Dowans/Richmond walikuwa wanauzia wananchi giza tena kwa bei ya kuruka huku wakiwa wameahidi kuuza umeme. Symbion ndio wamenza kazi, tuwa-judge baada ya kuona utekelezaji wao.
 
wale wengine walikuwa waislamu na symbion ya wakristo.

hutawasikia akina mwanakijiji wakiandika barua ndefu ndefu kupinga bungeni na seneti usa maana wanaweza kutupwa nje ya mipaka yao.

kwa symbion tutapiga makofi kumi. hata kesi mahakamani tuifunge tu.

nini tofauti kati ya dowans na symbion mimi siioni. wote wezi wale wale ila ngozi tofauti.

amri ya mahakama iko wapi. mwanahalisi wako wapi. daktari wa wakatoliki yuko wapi.

Unayo hoja. Ungeeleweka zaidi kama ungeondoa fikra za udini kwenye comment yako.
 
Kweli Tanzania kichwa cha Mwendawazimu....... ukija na jembe unanyoa...jambia ....panga... shoka... Tusifurahie sana ujio wa Wamarekani Tz kwa fujo...kuna kitu wameshakiona...tukija kushtuka itakuwa too late...Hapa ni Mungu tu atunusuru..

Kuna raia mmoja wa kigeni mahali fulani aliwahi kujigamba hivi: "Tanzania is a fertile country, you can plant stone and harvest mangoes".
 
Kuna raia mmoja wa kigeni mahali fulani aliwahi kujigamba hivi: "Tanzania is a fertile country, you can plant stone and harvest mangoes".

Ndo faida ya ubinafsishaji ambapo tumebinafsisha hadi akili zetu. Mungu ibariki Tanzania
 
kwa sasa tupate umeme kwanza......halafu hayo mengine tutayaangalia badae.

tatizo la richmond na dowans, sio ufisadi wake, wala sio hayo mabilioni wanayodai...tatizo ni kwamba huo ufisadi na hayo mabilioni yanadaiwa wakati hakuna umeme.....inakuwa haileti mantiki.

so, hiyo symbian ilete umeme kweli, sio longolongo...mara ooh, gesi haitoshi, mara sijui nani ameenda kwenye harusi....hatutaki.

Hoja yangu ni kuwa kwa nini mitambo ya Tanesco ambayo haihitaji capacity charge wala gharama ya kununua umeme inazimwa ili kuipisha Symbion wakati tutahitaji kulipia umeme utakaozalishwa na kampuni hiyo?
 
Bongo tambarare! Mitambo hii iliyosifiwa na Clinton ni ile mitambo ya Dowans/Richmond iliyopigiwa kelele sana na wabunge wengi na baadhi ya mashabiki wa kisiasa Tanzania. Kinachotumaliza Tanzania ni ushabiki wa kisiasa hata katika vitu vyenye kuleta tija kwa taifia. Sasa ngoja tusikie yule atakayepiga kelele tena kama hajaambiwa wewe America, UK, Canada, etc hapana kanyaga.
Nadhani chuki za wanasiasa wa CCM ya wao kwa wao imetupelekea tuwe hapa tulipo leo. Hii pia inachangiwa na vyombo vyetu vya habari ambao nao wanaandika taarifa za kinafiki bila kufanya utafiti yakinifu na kutoa majibu ya utafiti hadharani. Nyingi utasoma tu kwa habari toka chanzo chetu, wakati mwingine unakuta mwandishi anatoa maono yake tu lakini ili ionekane habari anaandika as if kuna source.
Naunga mkono kuwashwa kwa mitambo hiyo ya Dowans kupitia Symbion na nasihi Tanesco wanunue umeme watuwekee kwenye gridi ili kupunguza huu mgao ambao kwa sasa hautangazwi lakini upo kwa sana. Kwa wanaoishi Kinondoni, M/Nyamala, K/Nyama na hata Sinza ni mashahidi kuwa mgao unaendelea kinyemela bila kutangazwa.
CCM na mipasuko ya viongozi wako wa roho wa madaraka ndiyo iliyotufikisha hapo. Hamuwezi kuwa wote mawaziri wakuu kwa wakati mmoja wala huwezi kuwa spika na waziri mkuu hapo hapo haiwezekani. Haiwezekani wote mkawa "mediocres" katika performance lazima kuna wanaofanya kazi zaidi na kama Mwenyekiti hataki kufanya kazi anaogopa sana mdogo wake anayefanya kazi kwa speed.
Haiwezekani ukapendwa na kila mtu kama unafanya kazi....ukiona unapendwa na kila mfanyakazi wakati wote (all the time) ukiwa bossi basi ujue kuwa hufanyi kazi bali umewaachia wafanyakazi wako mwanya wa kuiba, kutega na kueneza umbea katika organisation.
Tunahitaji tusimamie maamuzi yetu hata kama tulikosea sehemu fulani tunajifunza na kwenda mbele. "practice makes you perfect".
I love Tanzania, Mungu utusaidie Watanzania tufungue macho na tujue tuchohitaji. Hatuhitaji watawala bora au watakatifu...tunahitaji viongozi wenye thubutu ya kusukuma gurudumu letu mbele hata kama mbele bila kujali kuna mlima kiasi gani mbele au kuna urefu gani. Hata maili elfu zilianza na hatua moja.....

Nakubaliana nawe mkuu,tatizo la watawala wetu ni kwamba wapo pale ili mradi wawepo lakini hawapo pale kikazi,na akijitokeza mtu akaamuwa kuchapa kazi anapingwa kama ukoma,hebu angalia Mh magufuri alijitolea kuchapa kazi kwa kufuata misingi,taratibu na kanuni walizojiwekea lakini mwisho wa siku wakuu waka mkemea wakidhani labda anajitaftia umaarufu wa kisiasa

Lakini pia najiuliza swali hivi kweli watawala wa hii nchi hawaoni mambo yanavyokwenda mlama? inamaana ni sisi tu great thinkers ndio tunao yaona haya?
 
Mafisadi waligundua kuwa tatizo si mitambo ya Richmond/Dowans, bali ni majina hayo,
hivyo wamekuja na mbinu mpya ya kubadili jina ambalo ni Symbion. Kuna neno tena hapo?
Tutawasifia wee wakati mitambo ni ileile tuliyoikataa!

Mungu ibariki Tanzania
 
kwani yeye nani hadi akisifia kitu ndio iwe kimekubalika!??
Tatizo hatuna viongozi wenye maamuzi bali tuna viongozi wanaotekeleza mapenzi ya makundi fulani ya watu kwa faida zao wenyewe!!
Pole Tanzania
 
Cry my beloved country,

Marekani kama Nchi ambayo inajiita ni prefect wa dunia huwa kila siku inahimiza utawala bora. Dhana mojawapo ni utawala bora ni kufuata na kuheshimu sheria. Iweje leo huyu mama anapanda ndege Washington DC mpaka africa, Tanzania, Dar Es Salaam kuja kuhalalisha uvunjifu wa sheria.

Je hajui kama chombo kilichochaguliwa na wananchi ( bunge) kwa Azimio la Bunge kilisema wazi kuwa mkataba kati ya kampuni ya Richmond na Taanesco ( shirika la Umma) na baadaye kuhamishwa kwa Dowans ni batili , na moja ya sababu ni kukiukwa kwa sheria ya manunuzi? Je hajui kama kuna kesi mahakamani kuhusu mitambo hiyo na mahakama ikasema kuwa hakuna ruhusa kufanya kitu chochote wala mazungumzo juu ya mitambo hiyo bila ridhaa ya mahakama. Haoni kuwa kitendo cha Kampuni ya Symbions kununua mitambo hiyo ni uvunjaji wa sheria za nchi na kwa yeye kubariki kitendo cha kampuni yake kununua mitambo hiyo ni sawa na kusema ilikuwa sawa kwa Symbion kuvunja amri halali ya mahakama?

Je huyu Waziri anajua kuwa mara baada ya kununua mitambo symbions wakaanza mazungumzo na Tanesco kuhusu kuizia Tanesco umeme bila ya tena kufuata sheria ya manunuzi, Na anajua kuwa kabla mkataba haujafikiwa viongozi wa Symbion walikuwa Ikulu na mkuu wa nchi kabla hata mazungumzo hayajaisha, Hicho kitendo kingefanyika nyumbani kwa Hillary kweli wananchi wangeelewa? Uwazi wanaopigia debe kila siku uko wapi?

Haoni kuwa anavyofanya sasa ni sawa na alivyoingilia uhuru wa Pakistani wa kupeleka majeshi yake Ndani ya nchi huru kwenda kufanya ugaidi. Haoni kuwa anachofanya sasa ni ugaidi wa kibiashara ( commercial terrorism).

Viongozi wetu wako wapi? wawakilishi wetu wako wapi? Mbona wamekaa kimya bila kusema chochote, magazeti yako wapi, wanaharakati wako wapi? Ninapokaa na kuona kila mtu anachelea kusema inanifanya nikumbuke misamiati ya kizamani ya siasa ya maneno kama puppet na stooge na kufikia jumuisho kuwa viongozi wetu ni puppets na stooges wa nchi za magharibi na hawajali kabisa maslahi ya wananchi wao.

Nasema hivyo kwa sababu Tatizo tanzania sio Umeme, tatizo ni elimu duni, tatizo ni huduma za afya vijijini na mijini tatizo ni njaa inayotokana na kilimo duni, tatizo Tanzania ni kugawa ardhi kubwa yenye rutuba kwa wageni wachache na kuwaachia wazawa wakiwa hawana ardhi. Tatizo Tanzania ni jinsi tunavyonyonywa na kuuwawa na matajiri wanaochimba madini kama dhahabu, uranium nakadhalika, tatizo ni kugawana rasilimali zilizopo nchini, tatizo sio umeme kama Hillary alivyodanganywa.

Hillary Clinton ameishia Dar es Salaam na kupanda mboga Mlandizi, kwa nini hakusogea mbele kidogo tuu aonne jinsi wananchi walivyo na makazi duni maeneo ya Ruvu mpaka Chalinze, vituo vya afya duni, shule duni wakati makampuni toka nchini mwake ndo yanayoneemeka na rasilimali zetu?

Alimuuliza Mtanzania yoyote kuwa vipaumbele vyetu ni nini, au kaamua kudandia treni kwa mbele kama njia ya kusaidia uongozi uliopo baada ya kuona jahazi la umeme wa maruhani litaondoa utawala uliopo ifikapo 2015 na hivyo kufanya makampuni ya kimarekani kuanza upya kuongea na serikali itakayokuwa madarakani?

Hillary Please, remember we are a free country, let us decide our fate we do not need your hypocritical assistance.
 
Hapa Tanzania watu mbalimbali wamejitokeza kutengeneza sinema nyingi lakini kuna hii
iliyoanzia kwenye igizo dogo tu lenye maudhui ya vita dhidi ya rushwa na ufisadi la Richmond,
linaloonesha jinsi watawala walivyo tayari kuumiza wananchi wao ili kutibu majeraha yao wenyewe
au rafiki zao ni sinema tamu sana.


Sinema hii ndefu ilianza kama mzaha vile: wahusika wakuu wakiwa ni wale wanaojua kufisadi
Taifa hili. Jinsi sinema ilivyoanza wengi tulidhani itaishia sehemu moja tu ya Richmond, kumbe
jamaa ni wajanja sana kwani walipoona kuwa Watanzania tumepiga kelele nyingi kuhusu Richmond,
wakatubadilishia 'Angle' na kutuwekea sehemu ya pili ya filamu; Dowans.


Mwandishi wa kisa hiki: Richmond/Dowans, ni mwandishi mahiri sana mwenye kuijua vyema
kazi yake. Hubadilisha msuko wa hadithi (plot) kila anapoona ipo haja ya kufanya hivyo bila
kuharibu maudhui yake, mwanzoni tulipohoji tuliambiwa kuwa mmiliki wa Dowans hajulikani!
Wakati huohuo Waziri wa Nishati na Madini akikomalia kuilipa Dowans!


Upepo ulipobadilika ghafla baada ya kelele nyingi zilizopigwa na wananchi, mmiliki wa Dowans
akajitokeza na kukataa kupigwa Picha. Ila alitaja kuwa alitoa mamlaka kwa Mbunge Rostam Aziz
(ingawa Rostam aliwahi kuikana) kuisimamia Kampuni ya Dowans hapa Tanzania!


Watazamaji wa sinema wakaishtukia, mwandishi akabadilisha 'angle' na kutangaza kuwa
serikali ikinunua mitambo ya Dowans watafuta kesi. Watanzania wakagoma tena safari hii
kwa kelele kubwa sana. Sasa ameleta kitu kipya zaidi kinachoitwa Symbion Power!


Hapa ndipo sinema hii inaponoga zaidi, kwani alichokifanya mwandishi wa kisa hiki ni kuuhadaa
umma wa Watanzania na mgawo wa umeme ili tuingie mkenge wa nguvu, na tuikukubali
Symbion Power ambayo ni Mrithi wa Dowans.


Hii yote ni kuwafanya Watanzania majuha wasiojua kitu au kusoma alama za nyakati. Hainiingii akilini
kuwa Symbion Power na watuhumiwa wa Richmond/Dowans ni vitu viwili tofauti, watakuwa wamebuni
mkakati huu wa kuibua kampuni hii ili kufuta madoa ya Richmond/Dowans usoni kwao. Na sasa
Tanesco inaingia mkataba na kampuni hiyo ili ituuzie umeme.


'Angle' ya mwandishi katika kisa hiki imebadilika sana baada ya kuona kwamba jina la Dowans
halitakiwi kabisa na Watanzania ametuletea jina jipya, na kama tuliukataa umeme wa Dowans
basi tutasahau itakapoanza Symbion Power. Na wote tutapongeza maana tutaiona kama mkombozi
kwa kuwa tayari tumeghiribiwa kwanza kwa kuletewa mgawo wa umeme mkali ili ionekane kuna shida.


Sinema hii ndefu ya Richmond/Dowans, na sasa Symbion ina mafundisho mazuri sana kwa jamii:
mojawapo ni kuwa nchi yetu haipaswi kabisa kuwa na umeme ulio imara kwa kuwa watu watakosa
ulaji. Mgawo wa umeme ni lazima uwepo hata kama tulikwishaambiwa kuwa utabaki kuwa historia.


Bila mgawo wa umeme zile kampuni zao za kuuza majenereta zitakufa. Hivyo kwao mgao wa umeme
ni dili zuri, zuri mno. Dili litakalowahakikishia ulaji milele na kuendelea kujenga heshima ya kuwa na
vitambi vya kuvimbiwa ufisadi.


Wasiwasi wangu tu ni kuhusu mwisho wa sinema hii ndefu isiyochosha, kwani watawala wakizidisha
ulafi, wa kunywa mchuzi wote, wananchi wanaweza kuingilia kati na kuamua kumwaga ugali, kama
watawala wakimwaga mboga. Yatakayotokea baada ya hapo ni dhambi kuyaeleza.
 
Mbona sinema inaendelea ... si kuna Obama na Hillary Clinton? Si ni jana tu Mama Clinton alikuwa pale Ubungo?

Ndo maana nikaiita sinema, na huo ndio mpango waao kutuuzia umeme kwa kutumia mitambo (Dowans)
tuliyoikataa kwa kutumia jina jipya (Symbion Power)
 
The syndicate is huge!!! Hawa watu hawawezi kuacha michezo yao. Ni kama mtu anayekula nyama ya mtu, akianza haachi, hawa mpaka tuwatoe kwa nguvu!!!

Tutanyonywa mpaka basi...
 
Watanzania tutaendelea kubakwa hadi tutakapolia, "tunaumia!"
 
Hii sinema imeshaisha kama Uncle Sam(US gov.) kaingilia kati lakini na mashaka kuwa wamemwambia Mkulu tutaua hili soo nawe tufanyie abc si unajuwa mambo ya scratch my back i scratch yours.Kitendawili wanataka favour gani kwetu ??
 
Hii sinema imeshaisha kama Uncle Sam(US gov.) kaingilia kati lakini na mashaka kuwa wamemwambia Mkulu tutaua hili soo nawe tufanyie abc si unajuwa mambo ya scratch my back i scratch yours.Kitendawili wanataka favour gani kwetu ??

Itaisha kama wananchi watatulia na kukubali yaishe, vinginevyo hakitaeleweka endapo kelele za wananchi zitaanza tena,
kwani Marekani ni nani hadi asipingwe? Atatumia mabavu lakini ujumbe utamfikia kuwa wananchi wameshtuka
 
Symbion imekuja kufanya biashara(kuvuna shamba la bibi) au kusaidia?

Au neno kusaidia limepata maana mpya?

Kwa kawaida kila anayekuja Tanzania huwa na lengo la kukamua tu au kumegeana mapesa tu na kutuongezea matatizo.

Sawa tu kama tunahitaji kusaidiwa!

Taifa letu limekwishaharibika sasa hivi. Hata ikatokea umeanguka kwa kuzidiwa na maradhi karibu na mahali ambapo jamaa mwenye helicopter alikuwa ametua, akakuokota, akakuambia panda nikupeleke hospitali - kwa jinsi tulivyo Watz ni lazima tutasema, 'kwa nini aamue kuniokota na kunibeba, lazima huyu mtu anapata faida kwa kuinbeba, japo hujui faida gani!

Mtu mzima kabisa, unaweza kusema Marekani inaweza kufaidi kwa kuzalisha umeme kupitia mitambo ya Dowans!!! Wastani wa makusanyo ya bandari moja tu ya kimataifa, kati ya zaidi ya 100 walizo nazo ni zaidi ya U$400 million kwa siku. Huu ni mfano mdogo tu wa uchumi wa Marekani ulivyo mkubwa halafu aje Tz kwaajili ya kukuza uchumi wa Marekani kwa kupitia generators za umeme!! Tunawahitaji zaidi Wamarekani kuliko wanavyotuhitaji. Saudi Arabia, pamoja na utajiri wa mafuta, wameenda kuwapigia magoti Wamarekani waongeze vitega uchumi Saudi Arabia ili wapunguze tatizo la ajira, halafu eti maskini wa kutupwa Tanzania wanajifanya hawahitaji uwekezaji wa Wamarekani.
 
kwani yeye nani hadi akisifia kitu ndio iwe kimekubalika!??
Tatizo hatuna viongozi wenye maamuzi bali tuna viongozi wanaotekeleza mapenzi ya makundi fulani ya watu kwa faida zao wenyewe!!
Pole Tanzania
Hapo mama D tumefungwa bao la kisigino, tulikataa waarabu, tukakataa wahuni fulani vile sasa tumetumbukia jumla kwa USA.
Lakini kama ni staili ya kutubail out hakuna shida. If raping is inevitable,let the one raped relax and enjoy it.
 
hivi richmond nayo si ilitokea marekani??..................... yaani watz hatujakoa tu na hawa richmond wanaojigeuzageuza rangi??................
Nadhani huyu mama kachomekewa hii dili wala hajui nini ni nini?????? Nani atamsutua huyu na team yake???????? Madudu ni yale yale, watu wana bidii kuyauza kwa wajinga fulani WaTZ. CDM vipi penyeza news hizo kwa hawa jamaa, si wanachulia ufisadi?????? MWAKA HUU TWAFA kila kona tumebanwa, tufanyeje kujikwamua??????
 
Back
Top Bottom