Symbion Power acquires DOWANS Power plant

Symbion Power acquires DOWANS Power plant

Kuna ukweli hapa.

Balozi wa Marekani Tanzania baada ya kuona tatizo la umeme limekuwa kubwa na ni muhimu kwa Tanzania aliongea na serikali yake ya Obama kuhusu hili jambo. Serikali ya Obama na Marekani hawaiamini serikali ya Tanzania kwenye swala la pesa na ndiyo maana zile pesa za milenium haijapewa serikali bali wanafanya uwekezaji wenyewe. Serikali ya Obama ilikubali kusaidia Tanzania kwa kupitia pesa za jeshi za maendeleo. Hii kampuni inafanya shughuli za kusambaza umeme huko Afighanistan na hivyo wakatengewa pesa ili waweze kufanya shughuli Tanzania. Serikali ya Marekani ilitoa pesa hizo na pesa nyingine ikawapa kampuni ya GE ambayo ilikataa kuuza vifaa moja kwa moja kwa Tanzania kwa kuhofia rushwa. Hivyo GE na hii kampuni wameambia pesa itakuwa ya msaada na haitaenda serikalini bali itakuwa kwenye fungu la millenium fund. Obama alikubali kwa kushawishiwa na mama clinton na kumuagiza aende kuangalia hizo project na kumrudishia majibu ili kuona ni jinsi gani wanaweza kumaliza tatizo la umeme. Kupewa pesa huko kwa hizi kampuni zinasaidia kutoza kiwango kidogo cha uendeshaji wa hii mitambo na kuwafundisha Watanzania jinsi ya kuendeleza hii mitambo. Obama anataka Watanzania wafundishwe jinsi ya kuendesha hii mitambo badala ya kutegemea watu wa nje. Tanzania kama tunavyojua ni chaguo la marekani kuweka base yao na balozi wao wa Tanzania ni mwanajeshi mstaafu. Hivyo wanayosema hapo jamaa ni ya kweli kabisa.lakini si kitu kibaya ni kama ujenzi wa barabara wa millenium.
 
hahaaa kama kawaida ya US,ngoma yao ya symbion bado watanzania hawajacheza vizuri so lazima waongeze vibwakizo vya ngoma...hahaaa
 
wakuu naomba kuuliza swali hapa,pamoja ni hio Symbion kununua mitambo ya Dowans,bado ile kesi yao wanayodai serikali yetu inaendelea!!!!!!
 
wakuu naomba kuuliza swali hapa,pamoja ni hio Symbion kununua mitambo ya Dowans,bado ile kesi yao wanayodai serikali yetu inaendelea!!!!!!

hizi ni issue mbili tofauti symbion wamenunua mitambo ya DOWANS maana ilikuwa inauzwa
wanaojaribu kuunganisha symbion na DOWANS ni wakosa huruma kwa watanzania wanaoteseka na kesi ya umeme
kwa kifupi tuwape break hawa watu wafanye shughuli zao
mambo ya DOWANS tuwapelekee wao tuache unafiki na ushabi kila siku tunalia umeme leo wamarekani wamekuja watu mnapiga
kelele.
serikali ya marekani inaweka kupa nini kutoka hako kamradi ka symbion!!!!!!!!!!!!!!!
labda mtu aseme wanataka umeme uwe wa uhakika ili mambo yao ya kigamboni yaende vizuri nitaelewa lakini sio
hiyo pesa mbuzi ya umeme wa generator hii ni infrastructure kifuatacho nini hapo ndio tuwekane sawa
 
wakuu naomba kuuliza swali hapa,pamoja ni hio Symbion kununua mitambo ya Dowans,bado ile kesi yao wanayodai serikali yetu inaendelea!!!!!!

Mkuu unadhani kuna atakayesema lolote kuhusu kesi ile? Serikali hii ya kisanii imewaziba mdomo Board of directors na Management ya TANESCO si ajabu na yule hakimu wa ile kesi wasiongee lolote kuhusu kesi ile. Soma kwenye hiyo link hapo chini.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...aji-mkuu-chande-anahusika-23.html#post2062250
 
kuna taarifa zilizopatika kutoka symbion power..taarifa zaidi zinasema symion imekuja kwa msaada mkubwa wa serikali ya marekani kuisaidia tanzania.
Symbion imekuja kufanya biashara(kuvuna shamba la bibi) au kusaidia?

Au neno kusaidia limepata maana mpya?

Kwa kawaida kila anayekuja Tanzania huwa na lengo la kukamua tu au kumegeana mapesa tu na kutuongezea matatizo.

Sawa tu kama tunahitaji kusaidiwa!
 
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton jana alitembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Symbion iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuipongeza kwa kuwekeza Tanzania.

Clinton alisema ana imani kampuni hiyo inatekeleza majukumu yake vizuri ili kupunguza tatizo la nishati hiyo hapa nchini.

Alisema hayo mara baada ya kutembelea mitambo hiyo na kupokelewa na Ofisa Mtendaji wa Kampuni hiyo, Paul Hinks.

"Kutokana na tatizo la umeme linalowakabili Wananchi wa Tanzania, juhudi zaidi za ushirikiano zinahitajika ili kuwekeza zaidi kwenye sekta hiyo, nawapongeza Symbion kwa kuchagua kuwekeza Tanzania," alisema Clinton.

Alisema hakuna maendeleo bila kuwa na umeme kwani viwanda vinavyozalisha bidhaa havitafanya kazi na hivyo nchi kukosa maendeleo.

Alisema Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala ya umeme ili iweze kufikia upatikanaji wa megawati 3,000 ifikapo mwaka 2015.

" Umeme ni muhimu katika upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile hospitali, usipokuwepo huduma hizi na zinakuwa tabu kuzipata, serikali iendelee kuwekeza kwenye sekta ya umeme,"alisema Clinton.

Naye Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali ili kukabiliana na tatizo la umeme.

Alisema juhudi hizo ni pamoja Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kuagiza mitambo ya ufuaji umeme ya dharura.

Ofisa Mtendaji wa Symbion, Hinks alisema mtambo huo una uwezo wa kuzalisha megawati 120 na kuiuzia Tanesco.

Waziri Clinton leo anatarajia kukutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu na kufanya naye mazungumzo kabla hajaondoka nchini.

Marekani yasaidia Tanzania Sh 12 bilioni.

Serikali ya Marekani na Ireland zitaipatia Tanzania msaada wa dola 8.7 milioni za Marekani sawa na Sh12.8 bilioni ili kusaidia mpango wa kuboresha lishe kwa watoto.

Kati ya fedha hizo, Marekani itatoa dola 6.7 milioni sawa na Sh9.3 bilioni katika mwaka wa fedha 2012/13 wakati Ireland itatoa mwaka huu dola2 milioni za Marekani sawa na Sh2.8 bilioni.

Kiasi hicho cha fedha kilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton na Naibu Waziri Mkuu wa Ireland, Eamon Gilmore.

Walitangaza hayo kwenye mkutano wa majadiliano ya namna ya kuboresha lishe uliokuwa chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Akizungumza, Waziri Clinton ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku tatu, alisema serikali ya Marekani imeamua kutoa fedha hizo ili kusaidia juhudi zinazofanywa na Tanzania katika sekta ya afya.

"Tumefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Tanzania katika suala la lishe kwa watoto, ndiyo maana tumeamua katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha, tutatoa zaidi ya mara nne ya kiasi ambacho tumekuwa tukichangia katika lishe,"alisema Clinton.

Alisema fedha hizo zitasaidia kujenga uelewa miongoni mwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe katika mpango maalumu wa siku 1,000 za kupunguza vifo vinavyotokana na ukosefu wa lishe.

Clinton ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton, alisema watoto wanaokosa lishe bora hupata magonjwa ambayo yatasababisha madhara maishani mwao.

" Kama watoto hawapati lishe bora, hawataweza kupata elimu bora, hivyo taifa litakuwa na watu goigoi ambao watakuwa maskini,"alisema Clinton.

Waziri Mkuu, Pinda alisema kwa kuthamini umuhimu wa lishe kwa wanawake na watoto, Serikali kuanzia 2012/13 itakuwa ikitenga fedha kwa ajili kuimarisha lishe.

Aidha, Pinda alisema Serikali itaunda mpango wa kitaifa kuhusu lishe pamoja na kuunda kamati ya utendaji itakayosimamia.

"Pia tunataka kuandaa utaratibu wa kuweka virutubisho kwenye vyakula ili viweze kusaidia kutoa lishe bora kwa watoto na wanawake,"alisema Pinda.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu wa Ireland, Gilmore alisema serikali yake itaendelea kushirikiana na Marekani katika kuisadia Tanzania ili iweze kufikia malengo yake ya kupambana na magonjwa yatokanayo na lishe duni.

Alisema ili kupata lishe bora, serikali haina budi kuwekeza zaidi katika kilimo na hivyo kuwa na chakula cha kutosha.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton jana alitembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Symbion iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuipongeza kwa kuwekeza Tanzania.Clinton alisema ana imani kampuni hiyo inatekeleza majukumu yake vizuri ili kupunguza tatizo la nishati hiyo hapa nchini.
Alisema hayo mara baada ya kutembelea mitambo hiyo na kupokelewa na Ofisa Mtendaji wa Kampuni hiyo, Paul Hinks. "Kutokana na tatizo la umeme linalowakabili Wananchi wa Tanzania, juhudi zaidi za ushirikiano zinahitajika ili kuwekeza zaidi kwenye sekta hiyo, nawapongeza Symbion kwa kuchagua kuwekeza Tanzania," alisema Clinton.
Alisema hakuna maendeleo bila kuwa na umeme kwani viwanda vinavyozalisha bidhaa havitafanya kazi na hivyo nchi kukosa maendeleo.
Alisema Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala ya umeme ili iweze kufikia upatikanaji wa megawati 3,000 ifikapo mwaka 2015.
" Umeme ni muhimu katika upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile hospitali, usipokuwepo huduma hizi na zinakuwa tabu kuzipata, serikali iendelee kuwekeza kwenye sekta ya umeme,"alisema Clinton.
Naye Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali ili kukabiliana na tatizo la umeme.
Alisema juhudi hizo ni pamoja Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kuagiza mitambo ya ufuaji umeme ya dharura.
Ofisa Mtendaji wa Symbion, Hinks alisema mtambo huo una uwezo wa kuzalisha megawati 120 na kuiuzia Tanesco.
Waziri Clinton leo anatarajia kukutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu na kufanya naye mazungumzo kabla hajaondoka nchini.
Marekani yasaidia Tanzania Sh 12 bilioni
Serikali ya Marekani na Ireland zitaipatia Tanzania msaada wa dola 8.7 milioni za Marekani sawa na Sh12.8 bilioni ili kusaidia mpango wa kuboresha lishe kwa watoto.Kati ya fedha hizo, Marekani itatoa dola 6.7 milioni sawa na Sh9.3 bilioni katika mwaka wa fedha 2012/13 wakati Ireland itatoa mwaka huu dola2 milioni za Marekani sawa na Sh2.8 bilioni.
Kiasi hicho cha fedha kilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton na Naibu Waziri Mkuu wa Ireland, Eamon Gilmore.Walitangaza hayo kwenye mkutano wa majadiliano ya namna ya kuboresha lishe uliokuwa chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Akizungumza, Waziri Clinton ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku tatu, alisema serikali ya Marekani imeamua kutoa fedha hizo ili kusaidia juhudi zinazofanywa na Tanzania katika sekta ya afya." Tumefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Tanzania katika suala la lishe kwa watoto, ndiyo maana tumeamua katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha, tutatoa zaidi ya mara nne ya kiasi ambacho tumekuwa tukichangia katika lishe,"alisema Clinton.
Alisema fedha hizo zitasaidia kujenga uelewa miongoni mwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe katika mpango maalumu wa siku 1,000 za kupunguza vifo vinavyotokana na ukosefu wa lishe.Clinton ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton, alisema watoto wanaokosa lishe bora hupata magonjwa ambayo yatasababisha madhara maishani mwao.
" Kama watoto hawapati lishe bora, hawataweza kupata elimu bora, hivyo taifa litakuwa na watu goigoi ambao watakuwa maskini,"alisema Clinton.Waziri Mkuu, Pinda alisema kwa kuthamini umuhimu wa lishe kwa wanawake na watoto, Serikali kuanzia 2012/13 itakuwa ikitenga fedha kwa ajili kuimarisha lishe.
Aidha, Pinda alisema Serikali itaunda mpango wa kitaifa kuhusu lishe pamoja na kuunda kamati ya utendaji itakayosimamia." Pia tunataka kuandaa utaratibu wa kuweka virutubisho kwenye vyakula ili viweze kusaidia kutoa lishe bora kwa watoto na wanawake,"alisema Pinda.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu wa Ireland, Gilmore alisema serikali yake itaendelea kushirikiana na Marekani katika kuisadia Tanzania ili iweze kufikia malengo yake ya kupambana na magonjwa yatokanayo na lishe duni.Alisema ili kupata lishe bora, serikali haina budi kuwekeza zaidi katika kilimo na hivyo kuwa na chakula cha kutosha.

source -Gazeti mwananchi

kuna kazi tena hapo

mama kasifia mitambo ya Dowans kwamba ipo safi na ni ya kisasa,kwa maana hiyo hatuwezi kuruka chochote kile kitakachotokea kiwe kizuri ama kibaya

natoka nitarudi baadae
 
Ilikuwa Richmond, ikaandamwa na makashfa, wakaibadili jina na kudai kuwa imeuzwa, wakaiita Dowans. Makashfa yakaendelea kuwa makubwa. Mara wakataka tuwalipe mabilioni ya pesa. Tukawajia juu, wakaendelea kusisitiza tuwalipe. Wakati tukiendelea kuhamaki kwa hasira kwa kutaka kuibiwa mihela yetu akaja Al Adawi na kudai yeye ndiye mmiliki wa Dowans, akatutishia kuwa tumemchafua sana na tungeendelea angetuchukulia hatua kali. Tukafyata! Kufumba na kufumbua tukasikia sasa si Dowans tena bali ni Symbion. Tukapiga vigelegele vya furaha na pongezi.

Bosi wa kampuni ya ugavi umeme naye akatuthibitishia kuwa ndoa kati yao na Symbion ingefungwa ndani ya wiki mbili kuanzia pale tulipoitambua hiyo Symbion. Tukaendelea kukaa kimya. Hatukuwa na hatuna haja tena ya kuhoji imekuwaje kuwaje. Hatuna haja ya kuhoji tena kama yale mabilioni ya Dowans yamelipwa, nani amelipa na nani amelipwa.

Wakati tukiendelea kuishangilia Symbion, mara akaja mwakilishi wa mabosi wa dunia, akatembelea Symbion na kutupatia ahadi kedekede hasa kuhusu matatizo yetu ya umeme. Vigelegele vinaendelea.

Kukamilisha sinema, mitambo ya kuzalisha umeme ya Ubungo Gas Plant ambayo inamilikiwa na Tanesco imezimwa ili kuipisha Symbion iwashwe na kuingiza umeme kwenye gridi. Ni gharama nafuu kutembeza mitambo ya Ubungo Gas Plant kwani inamilikiwa na Tanesco hivyo haihitaji capacity charge wala gharama ya kununua umeme kwani Tanesco yenyewe ndiyo inamiliki, Symbion ni kinyume chake. Tunaambiwa kuwa gesi iliyopo haitoshi kutembeza mitambo yote kwa wakati mmoja. Na tayari Ubungo Gas Plant ziiiiii.....Symbion Power ripu ripu hureeeeee.........kwa maslahi ya nani?
 
hivi richmond nayo si ilitokea marekani??..................... yaani watz hatujakoa tu na hawa richmond wanaojigeuzageuza rangi??................
 
Bongo tambarare! Mitambo hii iliyosifiwa na Clinton ni ile mitambo ya Dowans/Richmond iliyopigiwa kelele sana na wabunge wengi na baadhi ya mashabiki wa kisiasa Tanzania. Kinachotumaliza Tanzania ni ushabiki wa kisiasa hata katika vitu vyenye kuleta tija kwa taifia. Sasa ngoja tusikie yule atakayepiga kelele tena kama hajaambiwa wewe America, UK, Canada, etc hapana kanyaga.
Nadhani chuki za wanasiasa wa CCM ya wao kwa wao imetupelekea tuwe hapa tulipo leo. Hii pia inachangiwa na vyombo vyetu vya habari ambao nao wanaandika taarifa za kinafiki bila kufanya utafiti yakinifu na kutoa majibu ya utafiti hadharani. Nyingi utasoma tu kwa habari toka chanzo chetu, wakati mwingine unakuta mwandishi anatoa maono yake tu lakini ili ionekane habari anaandika as if kuna source.
Naunga mkono kuwashwa kwa mitambo hiyo ya Dowans kupitia Symbion na nasihi Tanesco wanunue umeme watuwekee kwenye gridi ili kupunguza huu mgao ambao kwa sasa hautangazwi lakini upo kwa sana. Kwa wanaoishi Kinondoni, M/Nyamala, K/Nyama na hata Sinza ni mashahidi kuwa mgao unaendelea kinyemela bila kutangazwa.
CCM na mipasuko ya viongozi wako wa roho wa madaraka ndiyo iliyotufikisha hapo. Hamuwezi kuwa wote mawaziri wakuu kwa wakati mmoja wala huwezi kuwa spika na waziri mkuu hapo hapo haiwezekani. Haiwezekani wote mkawa "mediocres" katika performance lazima kuna wanaofanya kazi zaidi na kama Mwenyekiti hataki kufanya kazi anaogopa sana mdogo wake anayefanya kazi kwa speed.
Haiwezekani ukapendwa na kila mtu kama unafanya kazi....ukiona unapendwa na kila mfanyakazi wakati wote (all the time) ukiwa bossi basi ujue kuwa hufanyi kazi bali umewaachia wafanyakazi wako mwanya wa kuiba, kutega na kueneza umbea katika organisation.
Tunahitaji tusimamie maamuzi yetu hata kama tulikosea sehemu fulani tunajifunza na kwenda mbele. "practice makes you perfect".
I love Tanzania, Mungu utusaidie Watanzania tufungue macho na tujue tuchohitaji. Hatuhitaji watawala bora au watakatifu...tunahitaji viongozi wenye thubutu ya kusukuma gurudumu letu mbele hata kama mbele bila kujali kuna mlima kiasi gani mbele au kuna urefu gani. Hata maili elfu zilianza na hatua moja.....
 
Kweli Tanzania kichwa cha Mwendawazimu....... ukija na jembe unanyoa...jambia ....panga... shoka... Tusifurahie sana ujio wa Wamarekani Tz kwa fujo...kuna kitu wameshakiona...tukija kushtuka itakuwa too late...Hapa ni Mungu tu atunusuru..
 
wale wengine walikuwa waislamu na symbion ya wakristo.

hutawasikia akina mwanakijiji wakiandika barua ndefu ndefu kupinga bungeni na seneti usa maana wanaweza kutupwa nje ya mipaka yao.

kwa symbion tutapiga makofi kumi. hata kesi mahakamani tuifunge tu.

nini tofauti kati ya dowans na symbion mimi siioni. wote wezi wale wale ila ngozi tofauti.

amri ya mahakama iko wapi. mwanahalisi wako wapi. daktari wa wakatoliki yuko wapi.
 
kwa sasa tupate umeme kwanza......halafu hayo mengine tutayaangalia badae.

tatizo la richmond na dowans, sio ufisadi wake, wala sio hayo mabilioni wanayodai...tatizo ni kwamba huo ufisadi na hayo mabilioni yanadaiwa wakati hakuna umeme.....inakuwa haileti mantiki.

so, hiyo symbian ilete umeme kweli, sio longolongo...mara ooh, gesi haitoshi, mara sijui nani ameenda kwenye harusi....hatutaki.
 
Namkumbuka sana Mwalimu Nyerere (RIP). Uzumbukuku na viroja vya uongozi wa Tanzania yako vinaendelea kupasua anga. Nakumbuka furaha ile ya kuimba:

Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana....

Mengi ya yale yote tuliyoyakataa enzi zile sasa ndio sera. Mbaya zaidi, chama tawala kinatumia jina lilelile la chama chetu. Bado uyatima wetu unatutesa mno.
 
wale wengine walikuwa waislamu na symbion ya wakristo.

hutawasikia akina mwanakijiji wakiandika barua ndefu ndefu kupinga bungeni na seneti usa maana wanaweza kutupwa nje ya mipaka yao.

kwa symbion tutapiga makofi kumi. hata kesi mahakamani tuifunge tu.

nini tofauti kati ya dowans na symbion mimi siioni. wote wezi wale wale ila ngozi tofauti.

amri ya mahakama iko wapi. mwanahalisi wako wapi. daktari wa wakatoliki yuko wapi.

Kwani Richmond ilikuwa ya Baniani?
 
Back
Top Bottom