Symbion Power acquires DOWANS Power plant

Symbion Power acquires DOWANS Power plant

mkuu
mmhh mbona dowans iliwashwa kwa nguvu na fasta wakairukia huyu symbiona ana nini ama ni sababu mmarekani??

Dowans waliingia kichwakichwa Richmond ikiwa moto......Symbion wamejaribu ku-buy time wakati wato wako busy Samunge
 
Duh
hilisi mchezo nahisi kuona misukule ya gwajima ikizunguka zungka na kutafuta pa kutokea na kuishia kujikuta iko
viwanja vya kawe kwenye moto usiozimika

wapi ulipo sendeka
wapi ulipo xspika sita
wapi ulipo mwakyembe

wapi wale watanzania tuliokuwa tukipiga kelele ya dowans atuitaki sasa tumebadilishiwa jina na kuitwa symbiona tumekaa kimya

raha ya milele umpe ee richmond na mwanga wa amani
apumzike kwa dowans

amin

Tulikuchukia Richmond ila symbion alikupenda kushinda sisi.
 
Mwakyembe na Sita, kwa sasa wana ulaji ambao hawataki kuuharibu, ni mawaziri. Kwani kitendo cha wao kuipigia kelele Symbion, kitawakumbusha wanachama wenzao walio na masilahi (Kama yapo) na hii symbion, juu ya uhusika wao na CCJ.
 
Hiyo Symbion nao wezi tu! Sioni logic ya kuzima hiyo mitambo ya Watsila na kuwapisha Symbion.

Hili ni tatizo la kuwaachia politicians kufanya decisions kwenye technical issue wakati hawajui hata Power [p.u] = Current[p.u] X Voltage [p.u];

Inabidi tufike wakati tuwapinge waziwazi hawa viongozi wetu tena kwa nguvu zote kunapotokea inshu zisizokuwa na maslahi kwa nchi.
 
Hahaaa mkuu hapo kwenye red tunaweza kuiita "Fundamentals of Engineering for Politicians" lol.
 
Mwakyembe na Sita, kwa sasa wana ulaji ambao hawataki kuuharibu, ni mawaziri. Kwani kitendo cha wao kuipigia kelele Symbion, kitawakumbusha wanachama wenzao walio na masilahi (Kama yapo) na hii symbion, juu ya uhusika wao na CCJ.
Kweli kabisa, tusiwategemee hao kulipigia kelele suala hili..
 
Symbiom ni Dowans in disguise. Hao watu tusiwalaumu kwani hawana la kufanya. Kelele wamepiga lakini wenye nchi wamewazunguka wafanye nini?? Tusiwatwike lawama. Isitoshe ukiwa serikalini lazima ukae kimya tukumbuke Mrema alivyofukuzwa kazi na raisi wa awamu ya pili kwa kutofautiana na serikali yake iliyomuajiri!!! Ukiwa kwenye system hutakiwi kutofautiana na mkubwa wako!!!
 
mtakapogundua ni ya mkuu wanafiki wote mtakaa kimya.
moto wa chadema hauzimiki kwa maji wala mchanga.
nyie wanafiki kumbukeni wabunge wa chadema hata hamsini hawafiki ukilinganisha na serikali ya magamba ambayo kila aliyemo ndani anaiba kwa mikono na miguu.
hata polisi wanalalamika wapo wachache kulingana na idadi ya wahalifu.sasa kwa taarifa yenu kama nape amewatuma huko mje kupima joto ili aangalie ataiba wapi kamwambieni huu ni moto wa gesi hauzimwi kwa maji.
sisi kama kawa tunasubiri mwizi aingie ndani tufunge mlango ni kichapo tu.
nyie endeleeni na usingizi wa posho kiama ki usoni mwenu.
 
wana jamvi, natumai serikali yetu tayari imekwisha amua kuhalalisha deal zote za Richmond, Dowans na sasa Symbion Power. Na kwa kuwa wakuu wa hii kampuni mpya wamepiga hodi magogoni, na waziri wa mambo ya nje wa USA kakagua ile mitambo tuliyoita haramu na kuisifiwa kuwa ni mizuri; kwangu mimi ninaona ndo tumeambiwa kuwa mlichokuwa mnapigia kelele mtakigharimia na hivi sasa kitakuwa halali.
Kwa kuwa tumekuwa na hulka ya watendakazi wachache kuliingiza taifa ktk mikataba mibovu, ninaomba mwenye copy ya mkataba iliyoingia serikali yetu na symbion power atujuze angalau kwa kifupi kama haiwezekani kuuweka hapa jamvini, ili tujue ni wapi tumeliwa. Na kama mkataba huo utakuwa kwa maslahi ya kizazi kijacho au ndo ile ile, capacity charge za kufa mtu.
Ninaomba kuwakilisha
 
nimepokea uwasilishaji wako,natia sana shaka kwan iyo simba pawa imekuja,afu na wazr kaja mmmh afu kasema anakuja kuendeleza lishe
 
nimepokea uwasilishaji wako,natia sana shaka kwan iyo simba pawa imekuja,afu na wazr kaja mmmh afu kasema anakuja kuendeleza lishe
Ndo mambo ya mataifa yenye malengo ya miaka 100 ijayo, wanabadilisha chandarua kwa gold bars au msaada wa ujenzi wa choo cha shule kwa mgodi wa uranium. Hapa ndipo ninapotamani kujuwa wawakilishi wetu wamesaini nini ktk hili la Symbion, je lina unafuu au ndo mwendo mdundo!
 
Mimi ninaona hii ni kuwa negative tu. Je tulitaka mitambo tuifanyaje. Walijaribu kuwauzia serikali tukasema wasinunue mitambo iliyotumika, walitaka kuiondoa tukasema haiwezi kuondoka bado tuna hitaji hii mitambo. Sasa kuna kampuni imeinunua bado tunalalamika je mnataka tufanye nini???. Richmond imepita lakini nchi ni lazima iendelee na uwekezaji wa umeme hatuwezi kubali kulalamikia kila kitu ndugu zangu!!. Hata rate za $4.95 CENTS siyo mbaya hapa USA tumelipa wastani wa $12 CENTS
 
hivi tumewahi kujiuliza hawa wanaoigiza majenereta ya kutumia ni kina nani? MAFUTA YANAYOTUMIKA YANAIGIWA NA KINA NANI.,je,tumewahai kutafuta kujua hawa wote wana uhusiano gani na watawala .jiulize kisha tafakakali kwa kina
 
Mimi ninaona hii ni kuwa negative tu. Je tulitaka mitambo tuifanyaje. Walijaribu kuwauzia serikali tukasema wasinunue mitambo iliyotumika, walitaka kuiondoa tukasema haiwezi kuondoka bado tuna hitaji hii mitambo. Sasa kuna kampuni imeinunua bado tunalalamika je mnataka tufanye nini???. Richmond imepita lakini nchi ni lazima iendelee na uwekezaji wa umeme hatuwezi kubali kulalamikia kila kitu ndugu zangu!!. Hata rate za $4.95 CENTS siyo mbaya hapa USA tumelipa wastani wa $12 CENTS
Ndg yangu inamaana tutakuwa tunalipia $4.95 cents kwa kiasi gani (unit au !). Ni nini kingelifanyika juu ya hii mitambo. Hakika mitambo hii tulitakiwa kuitaifisha ila tu ndo mai yalishazidi unga. Haya ni maoni yangu tu!
 
Kwa hiyo na mishahara itakuwa kama ya marekani? Kazi kweli kweli mitambo ni ya m k w e r e anapunguza damage limitations tu.
 
Ndg yangu inamaana tutakuwa tunalipia $4.95 cents kwa kiasi gani (unit au !). Ni nini kingelifanyika juu ya hii mitambo. Hakika mitambo hii tulitakiwa kuitaifisha ila tu ndo mai yalishazidi unga. Haya ni maoni yangu tu!

Kutaifisha mitambo sio wakati huu ,kwani wanaweza wakakufungia masoko ya kupata vipuri.Kinachotakiwa ni kuwa makini na mikataba siku za mbeleni,hawakulazimishi kusign mikataba,inabidi watu makini wenye elimu ya kueleweka na wazalendo.Ni kawaida ya watanzania kusign madudu na kulalamika baadae.Haya tumeyaona IPTL,Songas,Dowans,Lada,Ndege ya Raisi.Kama hakuna wataalamu wakuelewa mikataba kodi wataalamu au wakala wa kukushauri na kukusaidia.Na kama elimu yetu inayotolewa nchini ina walakini boresha elimu achana na kutoe elimu mbovu,ili tutayalishe kizazi kipya kwa soko uria.Elimu bora ndio mtaji sio ngonjera za majukwaa ya kisiasa.
 
Mimi ninaona hii ni kuwa negative tu. Je tulitaka mitambo tuifanyaje. Walijaribu kuwauzia serikali tukasema wasinunue mitambo iliyotumika, walitaka kuiondoa tukasema haiwezi kuondoka bado tuna hitaji hii mitambo. Sasa kuna kampuni imeinunua bado tunalalamika je mnataka tufanye nini???. Richmond imepita lakini nchi ni lazima iendelee na uwekezaji wa umeme hatuwezi kubali kulalamikia kila kitu ndugu zangu!!. Hata rate za $4.95 CENTS siyo mbaya hapa USA tumelipa wastani wa $12 CENTS
Duh mkuu wangu mbona unanipa za Mkullo. hii $4.95 CENTS na $12 CENTS ndio unamaanisha nini haswa!
 
Kinachonitakiza mimi zaidi ni kwamba mkataba huu wameingia serikali lakini itakjapo tokea jambo lolote Utasikia Tanesco ndio wamefanya hivi ama vile na madhambi yote hurushiwa Tanesco.

Kwa nini Tanesco wenyewe wasipewe uwezo wa mwisho wa kuchagua mwekezaji badala ya serikali kuingia mikataba kisha likivunda lawama kwa Tanesco...
 
Wana-JF,
Wakati suala la posho ya wabunge linaendelea kushika na kutengeneza vichwa vya habari, binafsi naanza kupata wasiwasi wa masuala mengine ya msingi kuwekwa kapuni (kama hili la DOWANS na SYMBION). Ni kweli suala la posho kubwa kwa wabunge wetu ni la mates makubwa kwetu na lina umuhimu wake, pamoja na hilo, suala la ujio wa SYMBION na ununuzi wake wa DOWANS naona lina umuhimu sana kwa taifa letu na wananchi wangependa kujua wawakilishi wetu (CHADEMA) wana msimamo gani katika hili. Kimya cha wanasiasa wetu na woga wa ghafla wa kushindwa hata kuizungumzia SYMBION unanitia mashaka, kimya chao kinanitia wasiwasi kwa sababu kama suala hili likiachiwa basi natumaini mafisadi watakuwa wametufunga bao la kisigino, na binafsi nisingependa hilo litokee katika kipindi hiki tunachoelekea kusherehekea miaka 50 ya Uhuru katika nchi ambayo haiwezi kuwachukulia hatua wezi na wabadhifu wa mali ya umma.

Katika hali kama hii, kama CHADEMA na vyama vingine mtaamua kukaa kimya, basi hatutakumbuka kelele za CCM lakini tutakumbuka daima kimya cha CHADEMA na vyama vingine vinavyotaka tuvione kuwa ni mbadala wa CCM.
 
Back
Top Bottom