Swali kwa Tundu Lissu: Kama Corona ipo Tanzania, kwanini toka alipoingia Tanzania na kipindi chote cha kampeni miezi mitatu hakuvaa Barakoa?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,160
2,000
Tundu Lissu amekuwa akidai kuwa Corona Tanzania ipo akiwa Ubelgiji ukimbizini. Akiwa Tanzania hakusema toka siku ya kwanza alipotua tu uwanja wa ndege alivua barakoa na hakuivaa tena kipindi chote cha miezi mitatu aliyokaa Tanzania akifanya kampeni akizungukwa na umati wa watu wasiovaa barakoa.

Alipokuwa akiondoka nchini kurudi ubelgiji akiwa Airport ndio akavaa barakoa ya kuondoka nayo kwenda Ubelgiji.

Swali kwake, Kama Corona ipo Tanzania kwa nini toka alipoingia Tanzania na kipindi Chote cha kampeni miezi mitatu hakuvaa Barakoa na hakuugua Corona yeye na umati wote ule uliokuwa unafurika mikutano yake?

Nadhani hata wazungu sasa watamuona hayuko sawa na kuwa taarifa zake si za kuaminika na yeye si wa kuaminika, akiwa Tanzania anakuwa kivingine akiwa kwao kivingine.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,160
2,000
Kwani YEHODAYA . Corona (Covid 19) haipo Tanzania ?!. Kwani aibu ya nini na Corona haijaanzia Tanzania...
Nauliza yeye kwa nini hakuwa akivaa barakoa kama Corona ipo? viongozi walikuwa hawavai barakoa sababu wanajua haipo yeye anayesema ipo na wakati hakuwa akivaa barakoa yeye na familia yake ndie nataka ajibu.

Viongozi hawavai barakoa na walikuwa hawavai na hata sasa hawavai .Yeye ndiye ajibu anasemaje ipo wakati barakoa alikuwa havai?
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
3,728
2,000
Nauliza yeye kwa nini hakuwa akivaa barakoa kama Corona ipo? viongozi walikuwa hawavai barakoa sababu wanajua haipo yeye anayesema ipo na wakati hakuwa akivaa barakoa yeye na familia yake ndie nataka ajibu.Viongozi hawavai barakoa na walikuwa hawavai na hata sasa hawavai .Yeye ndiye ajibu anasemaje ipo wakati barakoa alikuwa havai?
Kujizuia na corona ni kuvaa barakoa tu? Alikuwa anatumia njia zingine kujikinga
 

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
14,108
2,000
Nauliza yeye kwa nini hakuwa akivaa barakoa kama Corona ipo? viongozi walikuwa hawavai barakoa sababu wanajua haipo yeye anayesema ipo na wakati hakuwa akivaa barakoa yeye na familia yake ndie nataka ajibu.Viongozi hawavai barakoa na walikuwa hawavai na hata sasa hawavai .Yeye ndiye ajibu anasemaje ipo wakati barakoa alikuwa havai?
Corona ipo na tarajia itakupigia hodi nyumbani kwenu ili upunguze dhihaka.

Kwanza sijui uongozi wetu una nini na Corona? Hawataki hata itamkwe au kujadiliwa!
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,160
2,000
Corona Ipo, tena ipo nyingi
Shule nyingi za boarding wamecancel graduation za form six kwa ajili ya corona

Acha kujidanganya corona ipo tena nyingi tu
Uongo wako haulipi wanafunzi wa bweni na day wanapiga masomo kawa kawaida kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu

Daladala kujazana kama kawa bila barakoa wala nini

Maisha yanaendelea mitaani masokoni kama kawaida
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,160
2,000
Upinzani mbaya sana
Mtu anatamani ata nusu ya watanzania wafe ili apate la kuongea, kwann watanzania tusiwe wamoja
Sio tu mbaya umejaa unafiki angali mkutano wa upimnzani Tunduma Lisu na mkutano wote hauna barakoa akiwemo Lisu na hauna distancing wako wanacheza kufurahia Tanzania isiyo na Corona lakini baada ya Lisu kuondoka anaimba ohh Tanzania Corona iko kibao liangalie linafiki hilo likicheza bila barakoa kwenye mkutano usio na barakoa hata moja.

 

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
10,408
2,000
Swali la kijinga sana hili

Bwana Yehodaya naona unafanya kazi yako vizuri sana,kazi ya kupayuka....
Swali sio la kijinga ni swali la msingi,achana na hao wanaomini hakuna corona tumzungumzie Lissu ambaye yeye anajua kuwa Tanzania sio kisiwa hivyo corona ipo na si yeye tu pamoja akina Mbowe Zitto na wengineo wote hawakuonekana kuchukua tahadhari zozote za kujikinga na corona katika kipindi chote cha kampeni,kwa mtu mwenyewe akili lazima ujiulize kwamba hao watu wanaamini katika hayo wanayopigia kelele au huyasema tu kisiasa? Hata wewe mkuu nadhani ulishangaa inakuaje Lissu afanye kitu kama kile.
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,966
2,000
Tundu Lissu amekuwa akidai kuwa Corona Tanzania ipo akiwa Ubelgiji ukimbizini. Akiwa Tanzania hakusema toka siku ya kwanza alipotua tu uwanja wa ndege alivua barakoa na hakuivaa tena kipindi chote cha miezi mitatu aliyokaa Tanzania akifanya kampeni akizungukwa na umati wa watu wasiovaa barakoa...
Swali la kitoto, mbona huko kwenye Korona inayoua watu 1,000 kwa siku baadhi ya watu hawavai barakoa.

Fikiri kabla haujaandika, usiandike kwa sababu tu unamchukia mhusika.
 

Kite Munganga

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,719
2,000
Tundu Lissu amekuwa akidai kuwa Corona Tanzania ipo akiwa Ubelgiji ukimbizini. Akiwa Tanzania hakusema toka siku ya kwanza alipotua tu uwanja wa ndege alivua barakoa na hakuivaa tena kipindi chote cha miezi mitatu aliyokaa Tanzania akifanya kampeni akizungukwa na umati wa watu wasiovaa barakoa...

Swali lako ni la kijinga ktk karne hii sijapata sikia kwani ni sawa na mtu aulize kuwa inawezekana vipi mwanamke apate mimba bila kunyanduliwa
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
3,728
2,000
Uongo wako haulipi wanafunzi wa bweni na day wanapiga masomo kawa kawaida kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu

Daladala kujazana kama kawa bila barakoa wala nini

Maisha yanaendelea mitaani masokoni kama kawaida
Maandishi yako yanaonesha akili yako na elimu yako,

Graduations ya form six ilitakiwa kuwa tarehe 13 na zimekuwa canceled zote,

Nenda hospitali za bungeni ukaone watu na barakoa, ww endelea kuamini wanasiasa kuwa hakuna corona
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom