Hivi Tundu Lissu alikubalije Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula awe mshauri wake kipindi cha kampeni?

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,352
2,000
Jana nimeisikia kauli ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akisema wanamshikilia mtu anayejiita Askofu wa kanisa la Moravian la uamsho Tanzania Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula kwa tuhuma za uchochezi.

Lengo langu siyo kum discredit huyu Askofu Ila mwanasheria msomi Kama Tundu Lissu hakuwa wa kukubali kuwa na mshauri Kama Mwamakula, tusiangalie umaarufu wake na kujulikana au uanaharakati wake bali mshauri anapaswa kuwa mtu wa haiba njema na mwenye uelewa wa mambo na mwenye busara

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula hana busara wala Sifa njema katika jamii. Historia yake inaonesha alifukuzwa ndani ya kanisa la Moravian Tanzania baada ya kuasi na kusababisha vurugu. Mwanzo alikuwa mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania na alikuwa kinara na muanzilishi wa migogoro ndani ya kanisa hasa Jimbo la mashariki. Kutokana na tabia yake hio ya kuchochea migogoro alifanya kanisa lisitawalike, ilifika wakati ikawa ni vita juu ya vita waumini wakawa wanapigana makanisani.

Ni mpaka pale kanisa lilipoamua kumvua uchungaji ndipo hali ilipotulia na sasa kanisa la Moravian Tanzania lipo shwari na imara.

Baada ya kufukuzwa uchungaji Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula bado amekuwa akijitambulisha Kama Askofu wa Kanisa la Moravian la uamsho, amekuwa akiongeza neno uamsho kujitofautisha na kanisa halisi la Moravian Tanzania.

Kiufupi Mwamakula anatumia jina la Kanisa la Moravian Tanzania ambalo limesajiliwa kwa manufaa yake, sijajua hata Kama limesajiliwa, hata Kama limesajiliwa je wizara ya mambo ya ndani inawezaje kuruhusu mtu asajili jina linaloendana kiasi hicho na kanisa lingine, na Kama halijasajiliwa inakuwaje wizara ya mambo ya ndani ikalie kimya uvunjifu huu wa sheria.

Nadhani sasa mtaona jinsi huyu Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula alivyo ni mtu wa aina gani? Je mtu mwenye sifa hiyo ya kufukuzwa ndani ya kanisa kwa kuasi anafaa kuwa mshauri wa mtu anayetaka kuwa mgombea urais?. Mtu anayetumia jina la kanisa kinyume na sheria na kulichafua kanisa la Moravian Tanzania je anafaa kuwa mshauri wa Rais Mtarajiwa? Lisu aliwaza nini?

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula amelichafua na anaendelea kulichafua kanisa la Moravian Tanzania kwa kujitambulisha Kama Askofu mkuu na huku kanisa la Moravian halinaga cheo cha Askofu mkuu, maaskofu wa kanisa la Moravian Tanzania wapo watano tu nchi nzima na Mwamakula si mmoja wao. Na wala hakuna Askofu mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania kwani kanisa lina uongozi wa majimbo na kila Askofu ana mamlaka kamili katika Jimbo na ngazi ya Taifa kanisa linaongozwa na sinodi.

Kwa mfano katika mkutano mkuu wa ACT Wazalendo Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula alijitambulisha Kama Askofu mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania na kushangiliwa kwa nderemo na vifijo huku akiwa ameongozana na wachungaji wake. Hali hiyo ameendelea nayo kipindi chote cha kampeni za Tundu Lissu.

Ombi langu kwa Serikali Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula adhibitiwe atahatarisha usalama wa nchi akiachwa Kama alivyohatarisha amani ndani ya kanisa.

Ushauri kwa Lissu awe makini siku nyingine anapoteua watu wa kumshauri.

Sikiliza kanisa la Moravian Tanzania likitolea ufafanuzi.

2206070_Mwamakula-484x450.jpg
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,233
2,000
Moravian Mbeya ndilo kanisa kubwa la pili kwa ukubwa Lisu akaenda na Askofu mwasi Mwamakula eti awahubirie wana mbeya jibu walilipata sanduku la kura yeye Lisu na wenzie watu walichukia kweli kuwa Lisu ANAWALETEA MUASI WALIYEMFUKUZA KANISANI NI DHARAU KUBWA MNO
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
102,251

Pumbaf,yaani kuwa na watu wenye akili kama zako hii nchi tusitegemee maendeleo kamwe
 
Meela

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,473
2,000
Moravian Mbeya ndilo kanisa kubwa la pili kwa ukubwa Lisu akaenda na Askofu mwasi Mwamakula eti awahubirie wana mbeya jibu walilipata sanduku la kura yeye Lisu na wenzie watu walichukia kweli kuwa Lisu ANAWALETEA MUASI WALIYEMFUKUZA KANISANI NI DHARAU KUBWA MNO

Usisahau mshauri mwingine wa Tundu Lissu alikuwa Shehe Ponda Issa Ponda. Jamani hao ndio watu desaini ya Lissu anayepigiwa upatu na mabeberu awe rais ya JMT. Lakini Mungu wa Mbinguni yuko na TZ, tusiwe na wasiwasi hayo hayatatokea kamwe. Mabeberu na Lissu wao na Issa Ponda na Mwamakula wataendelea kuisoma namba.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,233
2,000
Usisahau mshauri mwingine wa Tundu Lissu alikuwa Shehe Ponda Issa Ponda. Jamani hao ndio watu desaini ya Lissu anayepigiwa upatu na mabeberu awe rais ya JMT. Lakini Mungu wa Mbinguni yuko na TZ, tusiwe na wasiwasi hayo hayatatokea kamwe. Mabeberu na Lissu wao na Issa Ponda na Mwamakula wataendelea kuisoma namba.
Ni kweli ponda alitimuliwa BAKWATA ni mwasi wa BAKWATA Lisu ndie alimfanya mshauri wake.

Waislamu wengi wa Tanzania wako chini ya BAKWATA lakini Tundu LISU badala ya kumchukua shehe kutoka BAKWATA kwenye waislamu walio wengi akaenda kumchukua mwasi SHehe PONDA ambaye ni adui mkubwa wa waislamu walio wengi kama ambavyo Mwamakula ni adui mkubwa wa wamoraviani walio wengi

Hawa watu wawili tu Shehe Ponda na Mwamakula walichangia pakubwa sana anguko La Lisu na Chadema sababu si watu wa kuheshimika kwenye walio wengi kwenye dini zao

Lisu alichofanya ni kuchukua adui wa dini zote kubwa na kuwafanya ndio timu yake!!! Angeshinda hapooo?
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
14,146
2,000
Ni kweli ponda alitimuliwa BAKWATA ni mwasi wa BAKWATA Lisu ndie alimfanya mshauri wake
Waislamu wengi wa Tanzania wako chini ya BAKWATA lakini Tundu LISU badala ya kumchukua shehe kutoka BAKWATA kwenye waislamu walio wengi akaenda kumchukua mwasi SHehe PONDA ambaye ni adui mkubwa wa waislamu walio wengi kama ambavyo Mwamakula ni adui mkubwa wa wamoraviani walio wengi

Hawa watu wawili tu Shehe Ponda na Mwamakula walichangia pakubwa sana anguko La Lisu na Chadema sababu si watu wa kuheshimika kwenye walio wengi kwenye dini zao

Lisu alichofanya ni kuchukua adui wa dini zote kubwa na kuwafanya ndio timu yake!!! Angeshinda hapooo?
Lissu angekuwa wa kuangushwa basi serikali na NEC wasingetumia nguvu kupita kiasi kupora kura za wananchi. YEHODAYA .

Lissu, Mwamakula, Ponda etc ni aina ya watu wasiopenda kuburuzwa na wenye kusifu na kuabu.
 
IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
3,636
2,000
Mwanzoni mimi nlikuwa nasema waliomharibia na kumkosesha ushindi Lisu ni Asmterdam na Shehe Ponda, kumbe hata huyu Mwamakula nae yumo.

Hivi kina Baregu walijitoa chadema kabisa? Mbona kinaonekana kama hakina washauri wenye akili?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom