Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Navyozidi kukusoma naona unaongeza vitu vinavyoujaza vizuri uzi wako, suala la kila dini iwe na TV station yake linawezekana, mfano Catholic wana Radio Maria, na Waislam wana TV Iman kama sijasokea.

Unachojaribu kusema hapa ni kwamba inapotokea waumini wa hizo dini/dhehebu wakataka kusikiliza/tazama mafundisho ya dini yao wanatakiwa ku- tune specific tv station/radio yao.

Lakini sio hayo mafundisho kuyapeleka kwenye public TV station na kuwalazimisha hata wasiotaka kuyatazama (regardless wanalipa kodi coz bado wapo wanaolipa kodi na hawaoneshwi eg. ATR) hapa nimekuelewa una hoja ya msingi, wanatakiwa wote wapigwe chini.
 
Wakati kabla Rais hajahutubia kwenye shughuli za kitaifa wanasimama viongozi wa dini na kuliombea taifa na miongoni kwao yupo yule anaswali kihindu..bongo wahindu ni wachache lakini yule yupo siku zote.

Taifa letu halina dini ila mimi na wewe tuna dini zetu.

Kama huwezi kuvumilia kusikiliza masuala ya dini nyingine basi badilisha channel ili wenye kuelewa waendelee na ibada inayowahusu.

Hawezi kufurahishwa kila mtu tena kila wakati.
Hili unalolitaja ni mfano mwingine wenye kuonyesha jinsi mazoea yetu yanavyokiuka Katiba ya nchi hata katika matukio ambako mtu aliyeahidi kulinda katiba hiyo yupo pale.

Uhalali wa kazi za serikali hautokani na sala za dini yoyote.

Uhalali wa kazi za Bunge hautokani na sala za dini yoyote.

Uhalali wa kapo cha uaminifu kabla mteule hajaanza kazi katika ofisi ya umma hautokani na msahafu wa dini yoyote.

Katiba ya nchi ndio msahafu pekee inaotosha.
 
Tatizo hili hapa:

1. Serikali ya TZ haina dini japo watu wake wana dini, ambapo falsafa hii inaweza kutekelezwa kwa njia ya America-style policy or German-style policy

2. Dini za TZ ni Ukristo, Uislamu, u-ATR, ambapo waumini wa ATR ni wengi kuliko waumini wa Ukristo na Uislamu kwa pamoja

3. Kwa sababu ya utitiri wa dini zilizosajiliwa MOHA (500+) German-style policy haitekelezeki

4. Kwa hiyo, twende America-style, yaani, kufuta vipindi vya dini kwenye luninga ya Taifa.

Zingatia:

5. Tayari taasisi za dini zina vyombo vyake vya habari kwa ajili ya kuendesha mambo yao kwa jinsi wanavyoona inafaa.
OK sawa.
vipindi vya dini vimeanza kurusha Leo? Au Kwakua Leo kilirushwa kipindi cha Wasiotumia lugha ya kiswahili
 
Rejea jawabu hili hapa:

Hoja yako: Dada mi ni Mkristo lkn niseme ukweli kwamba kimtazamo wangu naona kama hoja yako haijakaa kitaifa bali imekaa kidini. Na ndo maana hoja hii imekosa wachangiaji wengi, hii ni kwa sababu watu wengi humu wameshachoka na hoja zenye kuleta malumbano ya kidini baina yetu kama Taifa.

Jibu: Haya sio malumbano ya kidini. Ni malumbano juu ya sera ya Taifa kuhusu namna bora ya kutenganisha dini na dola. Kuna sera za aina mbili duniani. Sera ya KImarekani na Sera ya KIjerumani. Wamarekani hawana hii habari ya kila dini kupewa airtime kwenye luninga ya Taifa. KIla dini ina luninga yake. Wajerumani wanweza kuruhusu baadhi ya dini kwenye luninga ya Taifa kama wanavyofanya wanapotumia TRA yao kukusanya sadaka kwa niaba ya makanisa. Lakini utitiri wa makanisa yaliyosajiliwa na serikali huwalazimisha kujikuta wanabagua baadhi ya madhehebu.

Hoja yako: Wengi humu tumeoleana na kuzaliana ktk imani tofauti. Unakuta baba muislam mama mkristo, au baba mkristo mama muisilam, watoto wanaozaliwa wanapokuwa wakubwa wanaamua wenyewe imani ya kufuata nk, hapo sijaongelea mtaani, mashuleni, maofisini na sehem mbali mbali za miji na nchi kwa ujumla.

JIbu: Kuoleana na mambo kama hayo sio hoja iliyo mezani. Mkristo akioana na Mwislamu wanaishi ktk nyumba yao wawili. Hilo sio suala la umma mpana wa kitaifa. Hoja yetu hapa ni jinsi gani bora ya kutofautisha maisha ya umma wa kitaifa na maisha binafsi. Maisha ya umma mpana wa kitaifa uko shuleni, ktk ofisi za serikali, ktk vyombo vya habari vya kitaifa, ktk vyombo vya usafiri wa umma, masoko, nk.

Hoja yako: Umekiri mwenyewe kwamba unafahamu kitambo kuhusu vipindi vya dini vinavyorushwa kila siku asubuh na usiku wakati wa kulala, yaani muda wa kufungua siku na muda wa kufunga siku, pia umekiri kuwa kuna vipindi vya kikristo huwa vinapitishwa kila jumapili kwa ajili yetu sisi wakristo lkn haukuwahi kuja kuhoji chochote kuhusu vipindi hivyo vya jumapili, lkn leo umeona na ndugu zetu na wao wameanza kupewa muda wa kuangalia au kufuatilia vipindi vyao TBC siku ya Ijumaa umekuja haraka haraka kuzungumzia habari za kodi, ila wakati walipokuwa wanarusha vya kwetu kila ijumapili bila kupitisha hiki cha ijumaa swala la kodi haukulihoji.

Jibu: Kila jambo lina sababu za karibu na sababu za mbali. Kabla ya leo Rioba alikuwa anaongoza kongamano Morogoro wakiwepo viongozi wa TEF. Pale alieleza vema dhima ya vyombo vya habari na nafasi ya lugha ya Taifa katika kujenga umoja wa kitaifa. Siku moja baadaye nikaona chombo anachokiongoza kinapingana na kauli zake za siku moja kabla. Nikafanya udadavuzi na kuibuka na hoja hii. Ni hoja ambayo haiwalengi Waislamu pekee wala Wakristo pekee. Ni hoja pana zaidi. Inawahusu Wakristo, Waislamu, Wabuda, Wahindu, Wabahai, na Wa-ATR. Pia KIlatini ni lugha ya Taifa ya Italia wakati Kiarabu ni lugha ya Taifa ya Saudia. Lugha ya Taifa ya Tanzania ni Kiswahili. TBC wanawajibika kukuza lugha ya Taifa la Tanzania na sio vinginevyo. Tujadili hoja niliyoweka mezani.

Hoja yako: Tupendane jamani sisi wote ni taifa moja hao waliotuletea hizi imani kwa sasa wapo mbali baada ya kupuuza mawazo ya aina hii.

Jibu: Njia bora zaidi ya kupendana ni kukubaliana kuhusu njia bora ya kisera katika kutekeleza matakwa ya kikatiba yanayosaema kuwa serikali ya Tanzania haina dini hata kama watu wake wana dini. TBC ni chombo cha umma kinachosimamiwa na serikali hiyo. Mjadala uendelee.
 
MPUMBAF MJINGA MDINI
Kawaida yenu tunaijua mkisha ona Nchi inaongozwa na WAISLAM mtaanza kuhoji kila aina ya ujinga Madhebu za Kikristo kila siku zitatoa MATAMKO mkitawa na Wagalatia wenzenu hata wakivuruga Nchi namna gani mnaufyata kimyaaa
Tumesha wazioe Waatoliki mnataka Nchi iwe ktk mikono yenu tu pumbaf zenu!
Sijajua unamtukana mtoa mada au wakatoliki! Likini mbona unatukana!

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
View attachment 1792731
Dk. Ayub Chacha Rioba, Mkrugenzi Mtendaji wa TBC

Leo nimeona matukio mawili yasiyo ya kawaida kwenye luninga ya Taifa TBC1, inayoongozwa chini ya Ukurugenzi wa Dk. Ayub Rioba.

1. Asubuhi kabla ya kipindi cha Bunge cha mswali na majibu TBC1 walirusha kipindi cha "Madrasa" kilichokuwa na ujumbe unaotembea kwa upande wa chini ukisomeka "Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Tukufu kwa Waislamu Wanawake Yameandaliwa na Taasisi ya Kiislam ya African Relief Foundation."

2. Mchana, mara tu baada ya matangazo ya Maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa SADC, ambako Ayub Rioba alikuwa mwongozaji, kilifuata kipindi ncha swala ya Kiislamu.

Nafahamu pia kwamba, TBC1 imekuwa na kawaida ifuatayo:

1. Kila alfajiri madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma sala ya asububi.

2. Kila usiku wa kati, kabla ya saa sita, madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma sala ya kufunga siku.

3. Kila Jumapili pia, madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma ibada za Jumapili.

Lakini, TBC ni mali inayoendeshwa kwa kodi ya umma chini ya usimamizi wa serikali isiyofungamana na dini yoyote, kama tunavyosoma kwenye katiba ya nchi.

Pia, dini nyingi tayari zinavyo vyombo vyake vya habari kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za kidini, kwa lugha wanazozitaka wao, hata kama sio lugha ya Taifa.

Nakumbusha kuwa, kwa sehemu kubwa, sala nyingi za madhehebu ya KiIslamu zinatumia lugha ya Kiarabu, jambo ambalo linakiuka sera ya kujenga umoja wa kitaifa kwa kutumia lugha ya Taifa.

Hata litania nyingi za Kikristo zinasomwa kwa lugha ya Kilatini ambayo sio lugha ya Taifa.

Kama hivi ndivyo, kwa nini TBC inatumika namna hii?

Ni muhimu swali hili lijibiwe ili tujichunguze kama vyombo vya habari vya kitaifa vinakweza maslahi ya vikundi kama vile taasisi za dini au vinatweza maslahi ya pamoja kama vile umoja wa kitaifa.

Napendekeza kwamba ni kosa kutumia kodi ya raia asiye na dini kuhudumia taasisi za kidini.

Ni kama ambavyo ni kosa kutumia kodi ya mtu asiye na chama cha siasa kutoa ruzuku kwa chama cha siasa.

Kuna tatizo hapo.
Chuki itakuua mb*wa wewe
 
Kwa mtazamo wangu tatizo hapo ni chuki ya dini fulani. Huwezi kumlazimisha mtu atumie lugha fulani katika imani yake.
Wengine imani zao haziruhusu tarumbeta lakini zinapigwa mara nyingi hasa brass band. Hapo inakuaje
Wengine imani zao haziruhisu misalaba,wengine wanaingia nayo TBC

Tofauti katika imani zetu ninyingi mno,hatuziangalii hizo tunaagalia mamboyatakayo tufikisha kwenye kufikia malengo ya nchi
Tusizipalilie tofauti zetu
 
Kwanini haudai Siku za Weekend Iwe Jumatatu na Jumanne?.
Maana J'mosi na J'pili ni Siku za Dini Fulani au hili haliihitaji tochi au sababu upo ndani ya Sikh hizi za ibada
 
View attachment 1792731
Dk. Ayub Chacha Rioba, Mkrugenzi Mtendaji wa TBC

Leo nimeona matukio mawili yasiyo ya kawaida kwenye luninga ya Taifa TBC1, inayoongozwa chini ya Ukurugenzi wa Dk. Ayub Rioba.

1. Asubuhi kabla ya kipindi cha Bunge cha mswali na majibu TBC1 walirusha kipindi cha "Madrasa" kilichokuwa na ujumbe unaotembea kwa upande wa chini ukisomeka "Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Tukufu kwa Waislamu Wanawake Yameandaliwa na Taasisi ya Kiislam ya African Relief Foundation."

2. Mchana, mara tu baada ya matangazo ya Maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa SADC, ambako Ayub Rioba alikuwa mwongozaji, kilifuata kipindi ncha swala ya Kiislamu.

Nafahamu pia kwamba, TBC1 imekuwa na kawaida ifuatayo:

1. Kila alfajiri madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma sala ya asububi.

2. Kila usiku wa kati, kabla ya saa sita, madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma sala ya kufunga siku.

3. Kila Jumapili pia, madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma ibada za Jumapili.

Lakini, TBC ni mali inayoendeshwa kwa kodi ya umma chini ya usimamizi wa serikali isiyofungamana na dini yoyote, kama tunavyosoma kwenye katiba ya nchi.

Pia, dini nyingi tayari zinavyo vyombo vyake vya habari kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za kidini, kwa lugha wanazozitaka wao, hata kama sio lugha ya Taifa.

Nakumbusha kuwa, kwa sehemu kubwa, sala nyingi za madhehebu ya KiIslamu zinatumia lugha ya Kiarabu, jambo ambalo linakiuka sera ya kujenga umoja wa kitaifa kwa kutumia lugha ya Taifa.

Hata litania nyingi za Kikristo zinasomwa kwa lugha ya Kilatini ambayo sio lugha ya Taifa.

Kama hivi ndivyo, kwa nini TBC inatumika namna hii?

Ni muhimu swali hili lijibiwe ili tujichunguze kama vyombo vya habari vya kitaifa vinakweza maslahi ya vikundi kama vile taasisi za dini au vinatweza maslahi ya pamoja kama vile umoja wa kitaifa.

Napendekeza kwamba ni kosa kutumia kodi ya raia asiye na dini kuhudumia taasisi za kidini.

Ni kama ambavyo ni kosa kutumia kodi ya mtu asiye na chama cha siasa kutoa ruzuku kwa chama cha siasa.

Kuna tatizo hapo.

Kwanini hikuhoji hayo wakati wa JPM na hata tulipokuwa na vipindi maalum kwa ajili ya msiba wa mzee MOI?
 
Hili unalolitaja ni mfano mwingine wenye kuonyesha jinsi mazoea yetu yanavyokiuka Katiba ya nchi hata katika matukio ambako mtu aliyeahidi kulinda katiba hiyo yupo pale.

Uhalali wa kazi za serikali hautokani na sala za dini yoyote.

Uhalali wa kazi za Bunge hautokani na sala za dini yoyote.

Uhalali wa kapo cha uaminifu kabla mteule hajaanza kazi katika ofisi ya umma hautokani na msahafu wa dini yoyote.

Katiba ya nchi ndio msahafu pekee inaotosha.
Waliamua kuwepo utamaduni wa kuapq ukiwa umeshika kitabu cha dini sio wajinga.

Walioamua Mungu ahusishwe katika kiapo cha kisiasa walijua wanafanya nyinyi.

Huwezi kumkwepa Mungu ukafanikiwa.
 
Bila kupepesa macho mleta mada ana element za kidini.
Hili suala la dini kila siku limekuwa likikemewa, maana ukibagua dini A utamaliza.

Ukishamaliza unabaki wewe na dini B, utaanza kusema huyu dhehebu fulani.
Ubaguzi wa aina yoyote/dini haukubaliki. Maana dhambi yake huwa ni daima
 
View attachment 1792731
Dk. Ayub Chacha Rioba, Mkrugenzi Mtendaji wa TBC

Leo nimeona matukio mawili yasiyo ya kawaida kwenye luninga ya Taifa TBC1, inayoongozwa chini ya Ukurugenzi wa Dk. Ayub Rioba.

1. Asubuhi kabla ya kipindi cha Bunge cha mswali na majibu TBC1 walirusha kipindi cha "Madrasa" kilichokuwa na ujumbe unaotembea kwa upande wa chini ukisomeka "Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Tukufu kwa Waislamu Wanawake Yameandaliwa na Taasisi ya Kiislam ya African Relief Foundation."

2. Mchana, mara tu baada ya matangazo ya Maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa SADC, ambako Ayub Rioba alikuwa mwongozaji, kilifuata kipindi ncha swala ya Kiislamu.

Nafahamu pia kwamba, TBC1 imekuwa na kawaida ifuatayo:

1. Kila alfajiri madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma sala ya asububi.

2. Kila usiku wa kati, kabla ya saa sita, madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma sala ya kufunga siku.

3. Kila Jumapili pia, madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma ibada za Jumapili.

Lakini, TBC ni mali inayoendeshwa kwa kodi ya umma chini ya usimamizi wa serikali isiyofungamana na dini yoyote, kama tunavyosoma kwenye katiba ya nchi.

Pia, dini nyingi tayari zinavyo vyombo vyake vya habari kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za kidini, kwa lugha wanazozitaka wao, hata kama sio lugha ya Taifa.

Nakumbusha kuwa, kwa sehemu kubwa, sala nyingi za madhehebu ya KiIslamu zinatumia lugha ya Kiarabu, jambo ambalo linakiuka sera ya kujenga umoja wa kitaifa kwa kutumia lugha ya Taifa.

Hata litania nyingi za Kikristo zinasomwa kwa lugha ya Kilatini ambayo sio lugha ya Taifa.

Kama hivi ndivyo, kwa nini TBC inatumika namna hii?

Ni muhimu swali hili lijibiwe ili tujichunguze kama vyombo vya habari vya kitaifa vinakweza maslahi ya vikundi kama vile taasisi za dini au vinatweza maslahi ya pamoja kama vile umoja wa kitaifa.

Napendekeza kwamba ni kosa kutumia kodi ya raia asiye na dini kuhudumia taasisi za kidini.

Ni kama ambavyo ni kosa kutumia kodi ya mtu asiye na chama cha siasa kutoa ruzuku kwa chama cha siasa.

Kuna tatizo hapo.
Unapaswa kuhoji vingi aisee, kiapo, Sala ya kikatoriki ya kufungua bunge, wimbo wa Taifa n. k japo sikuelewa ulipohusisha lugha ya kiarabu na kutoeleweka kwa wakristo na wengine wasio kuwa waislam, bahati mbaya sana hukuyasema haya zilipotumika billion za pesa kwenye mazishi ya kikristo ya baba wa Taifa, mazishi ya kikristo ya Benjamin mkapa na hata yale ya juzi ya JPM ambapo television zote zilipambwa na maombolezo ya kikristo na wakalipwa wasanii kuimba kwaya za kikristo kwa mamilioni
 
MPUMBAF MJINGA MDINI
Kawaida yenu tunaijua mkisha ona Nchi inaongozwa na WAISLAM mtaanza kuhoji kila aina ya ujinga Madhebu za Kikristo kila siku zitatoa MATAMKO mkitawa na Wagalatia wenzenu hata wakivuruga Nchi namna gani mnaufyata kimyaaa
Tumesha wazioe Waatoliki mnataka Nchi iwe ktk mikono yenu tu pumbaf zenu!
Tuliza mshono wewe..jibu hoja?acha mihemuko mtoto wa muamedi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi hivyo vipindi vya dini vitolewe kwenye taasisi zote za umma..sio TBC tu hata mashuleni..kuleta inshu za udini kwenye taasisi za umma ni kugawa taifa..kwanza taasisi za dini hazilipi kodi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom