Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Ni kitu cha kushangaza sana,mtu kuhoji watu wa dini, kutumia kitu ambacho kimepatikana na kodi za hao wenye dini, utahoji barabara, kwa nini zitumike na wenye dini, mahospitali, shule, madaraja, viwanja vya ndege, stend za bus, viwanja vya michezo, taa za barabarani, mwisho utahoji kupata vyeo. Mwisho unahoji mavazi, wakati wa dini zote, wamepewa nafasi kuvyaa mavazi ya shule, yanaondena na imani zao, kwa mfano wanafunzi wasiokuwa waislamu, wanaovyaa sketi fupi, blouzi na kichwa wazi wa kike, ndio mavazi yao mpaka kwenye nyumba zao za ibada.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Sikuwahi kulifuatilia hili, ila nadhani wanachofanya ni kutaka kubalance, yani siku ya ijumaa airtime kubwa inakuwa ni kwa dhehebu la kiislamu na siku ya jumapili airtine kubwa ni kwa wakristo.Kwahiyo kama wanapendelea upande mmoja zaidi hapo watakuwa wanakosea...
 
...na ukashangaa..maana ulifikiri hao waislam hawana haki ya kutumia hiyo stesheni ya Luninga..ila wakristo tu siku ya Jumapili? Nafikiri ungeyaacha kama yalivyo!

Soma vizuri. Bandiko linahoji utaratibu mzima wa TBC kutumiwa kidini bila kujali dini gani inatumia chombo hicho
 
Sikuwahi kulifuatilia hili,ila nadhani wanachofanya ni kutaka kubalance, yani siku ya ijumaa airtime kubwa inakuwa ni kwa dhehebu la kiislamu na siku ya jumapili airtine kubwa ni kwa wakristo.Kwahiyo kama wanapendelea upande mmoja zaidi hapo watakuwa wanakosea...

Nimehoji utaratibu mzima wa Ijumaa na Jumapili maana naona mambo yanakiuka dhima ya TBC ya kujenga umoja wa kitaifa kwa kutumia lugha ya Taifa na kuendesha programu za kitaifa.

Kwa vile dini tayari zina redio na TV zake nadhani umefika wakati TBC kuachana na mambo haya yanayokiuka kanuni za social justice
 
Ni kitu cha kushangaza sana,mtu kuhoji watu wa dini,kutumia kitu ambacho kimepatikana na kodi za hao wenye dini,utahoji barabara,kwa nini zitumike na wenye dini,mahospitali,shule,madaraja,viwanja vya ndege,stend za bus,viwanja vya michezo,taa za barabarani,mwisho utahoji kupata vyeo.Mwisho unahoji mavazi,wakati wa dini zote,wamepewa nafasi kuvyaa mavazi ya shule,yanaondena na imani zao,kwa mfano wanafunzi wasiokuwa waislamu,wanaovyaa sketi fupi,blouzi na kichwa wazi wa kike,ndio mavazi yao mpaka kwenye nyumba zao za ibada.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app

Hoja hapa ni fupi: ni kwa vipi taasisi za umma kama vile RTD, shule na TBC zinaweza kuwa nyenzo ya kujenga utaifa. Utaratibu wa sasa una dosari. Just my fair opinion
 
Hoja hapa ni fupi: ni kwa vipi taasisi za umma kama vile RTD, shule na TBC zinaweza kuwa nyenzo ya kujenga utaifa. Utaratibu wa sasa una dosari. Just my fair opinion
Kujenga utaifa ndio huko, watu wa dini kutumia miundombinu na vyombo vya umma, kwa vile wao hao watu wa dini, ndio walipa kodi wenyewe. Huwezi kutengenesha, watu(ambao wana dini), na kunufaika na miundombinu na Taasisi zinazotokana na kodi zao. Hivi ulitaka watumie wasio na dini?Wakati hata wasio na dini, wana vipindi vyao, kwa mfano ngoma, taarab, mziki, vipindi vya maigizo, ambavyo yapo madhehebu ya dini mengine, hawakubaliani na hayo, lakini wapo kimya.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Umeenda mbali sana, inawezekana wakawa wanatumika bila wao kujua kama wanatumika,

Japo I highly doubt that kwani TBC ipo kwa ajili ya umma wa watanzania na Waislamu na Wakristu ni moja ya makundi makubwa yaliyopo.

Mfano. Siku kama ya leo Ijumaa Waislamu (kundi mojawapo) ndio huswali na lugha kuu inayotumika kwenye dini yao ni kiarabu, this is the reality we should face it is worldwide otherwise walazimishwe kubadili lugha which is not possible, coz watakuwa tofauti na wenzao duniani.

Same kwa wakristu siku ya jumapili nao hurushwa hewani bahati nzuri kwao lugha inayotumika ni kiswahili, I think this to you is not a problem.

Hicho kimekuwa intended kuwafikia walengwa pekee, ni kweli usemavyo Tanzania/serikali haina dini, lakini pia ukumbuke watu wake wana dini zao.

Hili naona tulikubali tu halikwepeki, au kama wataka kuondolewa vipindi vya dini TBC basi viondolewe vyote bila kujali lugha inayotumika.

TV ya taifa inaendeshwa kwa mtindo wa push technology, sio kwa mtindo wa pull technology, ambako mtazamaji huchagua programu gani aangalie

Kwa hiyo, yafaa ionyesha programu za kitaifa pekee, kwa kutumia lugha ya Taifa pekee.

Taasisi za dini zina TV na REDIO zake.

Wajihudumie bila kuhujumu umoja wa kitaifa kupitia mgongo wa kodi ya umma wote
 
Kujenga utaifa ndio huko,watu wa dini kutumia miundombinu na vyombo vya umma,kwa vile wao hao watu wa dini,ndio walipa kodi wenyewe.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app

Hapana, kosa linalofanyika TBC ndio linafanyika kwa msajili wa vyama vya siasa. Kodi ya watanzania wasio na vyama inatumika kulipa ruzuku kwa vyama.

Vivyo hivyo, kodi ya mtu asiye na dini inatumika kuendesha TBC kwa faida ya muumini wa dini Y, etc

Haya mambo sio sawa hata kidogo
 
Ukimsoma vizuri jamaa hana shida na wakristo kutumia TBC, yeye shida yake ni Waislam. Hii ni kwasababu Jpili na siku nyingine amesikia Wakristo wakiendesha Ibada hakushtuka, ila leo ameshituka baada ya kuona swala na ibada za Waislam, ikamtuma

Soma tena hapa ili ujielekeze kwenye hoja ya mwandishi bila kufanya spinning:

Nakumbusha kuwa, kwa sehemu kubwa, sala nyingi za madhehebu ya KiIslamu zinatumia lugha ya Kiarabu, jambo ambalo linakiuka sera ya kujenga umoja wa kitaifa kwa kutumia lugha ya Taifa.

Hata litania nyingi za Kikristo zinasomwa kwa lugha ya Kilatini ambayo sio lugha ya Taifa.

Na hapo sijaongelea jinsi sare moja ya wanafunzi wote shuleni ilivyo nyenzo muhimu kwa ajili ya kutekeleza sera ya umoja wa kitaifa.

Kama hivi ndivyo, kwa nini TBC inatumika kidini namna hii?

Ni muhimu swali hili lijibiwe ili tujichunguze kama vyombo vya habari vya kitaifa vinakweza maslahi ya vikundi kama vile taasisi za dini au vinatweza maslahi ya pamoja kama vile umoja wa kitaifa.

Napendekeza kwamba ni kosa kutumia kodi ya raia asiye na dini kuhudumia taasisi za kidini.

Ni kama ambavyo ni kosa kutumia kodi ya mtu asiye na chama cha siasa kutoa ruzuku kwa chama cha siasa.
 
Mleta mada ana chuki kubwa dhidi ya uislam Ila Kwa unafiki anajaribu kutaja taja na ukristo ili kuficha chuki yake.

Sijaona mtu mwenye akili timamu Kama anaweza akakaa na kuanzisha mada Kama hii labda sana sana awe anasumbuliwa na chuki dhidi ya Imani fulani Kama huyu fala

Hujaelewa hoja, soma tena, kisha ujielekeze ktk hoja
 
...na ukashangaa..maana ulifikiri hao waislam hawana haki ya kutumia hiyo stesheni ya Luninga..ila wakristo tu siku ya Jumapili? Nafikiri ungeyaacha kama yalivyo!

Hujasoma wala kuelewa hoja. Siongelei uislamu. Tuliza kichwa chako, vaa miwani kama macho yana tatizo
 
MPUMBAF MJINGA MDINI
Kawaida yenu tunaijua mkisha ona Nchi inaongozwa na WAISLAM mtaanza kuhoji kila aina ya ujinga Madhebu za Kikristo kila siku zitatoa MATAMKO mkitawa na Wagalatia wenzenu hata wakivuruga Nchi namna gani mnaufyata kimyaaa
Tumesha wazioe Waatoliki mnataka Nchi iwe ktk mikono yenu tu pumbaf zenu!

Mimi sina dini, kwa hiyo sitaki kodi ninayolipa itumike kuendesha shughuli za kidini kama wanavyofanya TBC. Hapo sibanduki.
 
Mods threads kama hizi hazina tija sana sana zitakaribisha malumbano yasiyo na afya kwa jamii. Tafadhalini futeni hii takataka

Maneno haya hayana uhalisi: Threads hizi hazina tija, malumbano hata hayana afya, etc.

Mjadala unaohusu ulinzi wa katiba ya nchi sio jambo la kubeza.

Twende kwa mtindo wa point counter point. Tutafika.

Wenye jaziba watashangaa wakijibiwa kwa hoja na upole.

Hili sio jambo la kufunikwa funikwa.
 
Back
Top Bottom