Swala la TUGHE kunikata 3% ya mshahara wangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swala la TUGHE kunikata 3% ya mshahara wangu.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mupirocin, Jan 5, 2012.

 1. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Habari za sasa wanaJf.
  Mimi ni mwajiliwa mpya kwenye sekta ya afya katika salary slip yangu nakatwa PAYE 30% mshahara wangu ni above 720,000/= TUGHE nakatwa 2% NHIF 3% na NSSF 10%: Hoja yangu ni hivi TUGHE wananikata kiasi hicho kwa kazi ipi wanayonifanyia, nikiwa intern wanakosa posho hatuoni kama wako concerned nakatwa 30% kama kodi ya kichwa sioni mtu akitoa tamko hata kuionya serikali . Nimeajiriwa sioni hata kiongozi kuja kunikaribisha kama mpya na faida nitakazo zipata kama mwanachama wa TUGHE, kwa kweli nimeamua kumwagiza katibu wa kituo aache mara moja kunikata mshahara wangu kuwapa wezi hawa wa watumishi wa afya. Naomba wafanyakazi wote tuungane tutor ufisadi wa hawa watu wa TUGHE, SWALA la PAYE nitalizungumzia siku nyingine.
   
 2. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,635
  Likes Received: 1,996
  Trophy Points: 280
  uliwahi ku-apply kuwa mwanachama wao? Vipi walipata idhini ya kukata pesa yako....subiri kidogo nije nikupe mfano halisi wa wizi wa hivyo vinavyojiita vyama vya wafanyakazi...WEZI WAKUBWA!
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  tena mimi sitaki kuvisikia kabisaaaaaaa

  hivi vyama bwana vinashirikiana na serikali kutuibia
  mfanyakazi anakatwa kodi ya kichwa na vat lakini anapokwenda sokoni hakuna vitu vilivyotengwa kwa ajili ya wafanyakazi kwani atavinunua na kulipia tena kodi huu ni unyonyaji kwa wafanyakazi

  chama cha walimu ndio kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa,wao wanakata pesa kwa kulazimisha lakini bado walimu kibao wanamatatizo

  bima ya afya ndio sitaki kuisikia kabisaaaaaaaaaaaaaaa,wao wanakata hata kama hujajiunga,kila mwezi zidi ya 10000,lakini ukienda hospital uakimbiwa na wametupa majina kbisa pasipo kujua kuwa tunakatwa pesa zetu,huu wizi sijui lini utakwisha

  yapo mengi sana wafanyakazi wanakatwa ktk mishahara yao
   
 4. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  mkuu mimi sijui hata maana ya TUGHE na wala sijamwona kiongozi yeyote kunikaribisha na kunipa maelekezo ya huo upuuzi wao. Binafsi nimeshamwambia katibu sitaki kukatwa hela yangu kuwagawia mafisadi.
  Mbaya zaidi nakatwa 30% ya mshahara wangu. Yaani 30% ya 720000 jumlisha na hela inayozidi kwenye hii laki 7. Mimi nilijua VAT ni 14% nikajua itakatwa hii ya salary yangu. Binafsi niliishiwa nguvu kabisa kumwuliza mhasibu eti na katwa kiasi hicho afu bado nikienda sokoni kila ninacho nunua nalipa ushuru tena. Mimi naomba wachumi wanisaidie hii system ya hapa bongo inatumika wapi duniani na nini maana yake mtu kukatwa 30% kama tax.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  ulijiunga uanachama tughe?
   
 6. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama bado hujajaza fomu au kutoa maeleze kwa maandishi wakukate hiyo ada ya uanachama ni batili hustahili kukatwa bila wewe kuridhia hayo makato, kwanza unatakiwa uwe mwanachama wa Trade Uninion yeyote ile ikiwamo TUGHE na uridhie vinginevyo hata hao wanaokata toka mshahara wako wana kiuka sheria soma Employment and Labour Relations Act , Part V, Act 61 inayoongela Deduction of trade union dues. Hapo utapata nguvu ya kisheria ya kuwaeleza wanaokata hizo 3% wasimamishe makato hayo
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Unajua sheria za Tanzania zina loophole nyingi mno. Zinaweza kusema hivi kwenye kipengele fulani halafu kipengele kingine kikaja kupinga kipengele hicho.

  Mfano kwenye Act hiyo hiyo ya Ajira ya 2004 kuna kipengele kingine ambacho kinasema mwajiri kwa kukubaliana na chama cha wafanyakazi chenye wanachama ambao ni majority wanaweza kumkata mfanyakazi Union dues hata kama si mwanachama ilimradi anafaidi matunda ya kazi zifanywazo na chama (kama vile negotiations za mshahara....n.k). Makato haya yanaitwa "Agency shop fees" ambayo hayatakiwi kuwa zaidi ya makati ambayo wanakatwa wanachama wengine.

  Maana yake ni kuwa hata kama wewe si mwanachama lakini chama kina tawi lake mahali pa kazi ambalo lipo kisheria na limepata majority ya wafanyakazi ambao ni members, basi hata wale wasio wanachama watakatwa kiwango hicho cha fedha ili kulipia huduma zitolewazo na chama, ili mradi malipo hayo yasizidi kiwango ambacho wanakatwa wanachama wengine ambacho ni 2% ya base salary.
   
Loading...