Mnoko
Duh! hii kali...
Suzy pole sana kwa mitusi unayopewa japo hatujuwani. Mgosi Tido nawe pole sana kwa tuhuma hizo. Yamesemwa mengi.. kutekelekeza familia kule London (najua wako TIC, London)..japo kupanga ni kuchaguwa.
Hili la udini linatia kinyaa...mi najaribu kuhakiki ila napata tabu mno wamejaa watu wa dini moja sana kwenye habari pale TUT. Ni ndugu zangu kutoka bonde kina Kihampa, Neema Mhando, nk. Jaribu ku sort out maana tulizoea kusikia lafudhi za kiswahili faswaha za kina Hemed Jongo, Mikidad Mahmoud, Mohammed Ahman, Abdallah Mlawa, Halima Mchuka, Ahmed Kipozi,nk.
Hoja si udini, lakini nani hajui kama wenyeji na waswahili wa pwani ni wazuri kwa lafudhi na kiswahili kitamu. Sitaki kuwasema watani wangu wasukuma kule MWANZA AU Tabora halafu uwape taarifa ya habari wakusomee ile ladha ya kusikiliza itakuwepo?
Tido TUT technically unafaya vitus na mabadiliko tunayaona.. napenda presentations za Aisha Dachi na yule binti mwenye jina kama la Kikenya (samahani nimemsahau). Marina Hassan naye anajitahidi lakini aache kiswahili kirefu na maelezo mengi.