Nguvu ya elimu katika medani za ujasusi na ulinzi: Tanzania tuna nini cha kujifunza?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
UTANGULIZI:

Kuna uzi uliwahi kuanzishwa na Ndugu Mwanahabari Huru

Ambapo aliwasilisha mambo ambayo Bwana Evarist Chahali aliwahi kuyazungumza kuhusu hali ya Usalama hapa nchini. Japo dhumuni la huu uzi siyo kuyazungumzia hayo mambo bali kusema kile kitu ambacho Mkuu izzo alikiandika hadi kunishawishi na mimi pia nichangie. Alizungumzia kuhusu nguvu ya Elimu kwenye medani za Ujasusi, ambapo alisema kwamba nchi huwa hazitegemei pesa tu kwenye Ujasusi bali pia Elimu: Nchi zenye mifumo Imara ya Elimu kamwe hamuwezi kushindana nazo kwenye medani za Ujasusi hasahasa Ujasusi wa nje ya mipaka.

Hivyo basi kwa ufupi tu,
Ntaweka hayo mabandiko mawili yaliyochangiwa na mimi mwenyewe (MALCOM LUMUMBA)pamoja na Mkuu izzo ili tujenge msingi mzuri wa huu mjadala hivyo mnakaribishwa sana kuchangia au kukosoa chochote kile ili kufanya mjadala uwe wenye manufaa kwa wote. Tutakapo pata wasaha tutaweza kuwa tunachangia huu uzi kwa kuweka kabisa na nakala mbali mbali za Kitaalamu kama ushahidi ili kuweza kusaidiana zaidi.

SEHEMU YA I:
MAONI YA IZZO KUHUSU UMUHIMU WA ELIMU KWENYE MEDANI ZA UJASUSI


Tanganyika tumekubali kukaa uchi mbele ya mtoto mdogo wote tunajua Duniani hakuna nchi zenye mahusiano makubwa Kama ilivyo huu unaoitwa utatu wa kutukuka yani United states of America , United kingdom na Israel ambazo kwa pamoja zinatengeneza Block yenye nguvu kiuchumi, kijeshi na kimaendeleo kwani Duniani kuna block 4.

Duniani zipo nchi nne kutoka blocks 4 zinazorun dunia
1. USA (United states of America) hapa anatoka US
mwenyewe
2 USE(United states of Europe) hapa anatoka UK
3 TGC (The Great China) hapa anatoka China
4 MES (Middle East States) hapa anatoka Israel

Hizi nchi zinazotengeneza utatu uliotukuka pamoja na kuwa na historia ya ushirikiano wa miaka zaidi ya 200 kwa UK na US na miaka 70 kwa US na Israel hata siku moja hawawezi kushere intelligence information zinazohusu maslai ya nchi Kama nchi au mipango ya kijasusi ya nchi Kama nchi ukitoa maslai ya ushirikiano wao nitashangaa sana Sana na kusikitika Kama Tanganyika nchi iliyokuwa na sifa nje ya mipaka yake katika maswala ya intelligence, Security na Defence kwa kujua au kutokujua kuwa uchi kwa nchi ambayo ukubwa wake ni sawa na mkoa ndani ya Tanzania nchi ambayo tumeishinda kwa kila kitu kuanzia kiuchumi, kijamii na kimaendeleo japo kuna watu watasema kuwa wana maendeleo kuliko sisi lakini kwa tafsiri sahihi ya Development tumewazidi rabda wametuzidi usafi wa mji wao tu.

Ukiangalia wenzetu ambao mifano mingi tunachukua kutoka kwao pamoja na kufanya mambo mengi kwa pamoja lakini swala la National interest katika upande wa intelligence zinabaki kuwa siri ya taifa usika tu.

Kingine ambacho naona kinaweza kutufanya tukawa. uchi hata mbele ya vnchi vidogo ambavyo ni aibu kutokana na heshima yetu tuliojenga kwa muda mrefu kwenye sector ya intelligence, Security na Defence ni mfumo wetu wa kuchukua vijana ambao ndio mioyo ya usalama na Ulinzi wa, Watanganyika na Wazanzibar tumewakabidhi mfano wenzetu wanavyofanya ambapo hata sisi tulikuwa tunafanya hapo zamani sijui Kama tunaendelea kufanya.

Secret Service, CIA, MI5 (Military Intelligence, Section 5) na MI6 (Military Intelligence, Section 6) Mi5 na MI6 ni UK
intelligence Agency 5 ni domestic counter-intelligence and security huku 6 foreign intelligence taasisi hizi 4 zinafanya kazi kwa karibu sana na mifumo yao mingi inafanana sana recruitment zao zinafanana pia kwani wote wana recruitment za aina mbili.

1 Direct recruitment
2 Sponsor recruitment
DIRECT RECRUITMENT hii inafanyika kwenye vyuo vitatu tu duniani yani taasisi zote nne nilizozitaja hapo vyuo hvyo ni:

A University of Oxford (UK)
B Yale University (US)
C Stanford University (US)

Unaweza jiuliza kwa nini hv 3 tu na kwa nini si Harvard University, University of Cambridge au MIT(Massachusetts
Institute of Technology) nitakuja kuelezea kwanini sasa vyuo hvyo 3 ndio recruitment kubwa inafanyika kufika
vyuo hvyo unafika kwa njia mbili tu

1 Akili sana(Genius)
2 Kipato kikubwa(Rich)

Miaka ya nyuma Kabla ya hii Sponsor Recruitment walikuwa wanachukua kutoka vyuoni tu especially vyuo
hvyo vitatu kama nilivyokwambia kwanza ni vyuo ambavyo ni bora sana na mwanafunzi kusoma hapo lazima huwe na kitu kimoja kati ya hv viwili AKILI au Kwenu ni MATAJIRI kwani Ada yake imechangamka sana pia ni vyuo
vinavyochangamkiwa na wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali duniani so walikua wanapiga ndege watatu kwa jiwe moja kwan wanapata ku recruit wanafunzi wa mataifa mbalimbali kwa kazi za kispay pili wanapata best student kutoka sehemu mbalimbali duniani tatu wanapata first class family yani watoto wa matajiri na viongozi kutoka sehemu mbalimbali duniani kwani watoto wa matajiri na viongozi ni matajiri na viongozi wa baade so walikua wanaangalia future utakuja kuona baadae kwa nini nasema future?

SPONSOR RECRUITMENT hii ufanyika kwa kuapply kazi kama wanavyoapply kazi nyingine kila mwaka zinatoka
nafasi 15-45 unaweza jiuliza kwa nini ni nafasi 15-45 tu? Nitakuja kujibu so nafasi hizi zinatangazwa kwenye website za mashirika hayo na watu wanaapply na vigezo vyake ni 9 tu namba zote nitazielezea kwa nini sasa vigezo hvyo ni:

1. Pass a written examination called the (SAEE)
2. Physical Abilities Test (APAT)
3. Security interview and pass credit checks
4. Pass a polygraph exam
5. Pass a medical exam
6. Pass background investigation
7. Be interviewed by a hiring panel
8. Pass a psychological examination
9. Bachelor’s degree with superior academic achievement

Unaweza jiuliza kwenye hii sponsor recruit elimu imewekwa mwisho jibu ni kuwa Elimu kila mtu anaweza pata lakini akili zinapatikana kwa watu special pia Duniani kuna aina tatu za elimu ambazo ni

A Elimu ya dini
B Elimu ya darasani
C Elimu maalumu (elimu hii wanafundiswa watu maalumu kuja kudeal na wenye elimu hizo mbili yani dini na
darasani)

Hapa nia yao ni kukufundisha elimu maalumu ambayo huwezi fundishwa shuleni au kanisani na msikitini lakini
wanaitaji mtu mwenye uelewa kidogo ndio maana wakasema bachelor’s degree with superior academic
achievement YALE UNIVERSITY chuo hiki kipo New Haven, CT 06520 Connecticut US hapa ndipo hub ya recruitment ya spies unakumbuka nilikwambia intelligence is about FUTURE?

Chuo hiki ndio chuo ninachoongoza duniani kwa kutoa viongozi, wataalamu, watafiti yani kinafiti namba 3 katika intelligence namba 3 ina maana kubwa sana nitakuja elezea pamoja na zile namba pale juu YALE pekee kwa Marekani imetoa.

1 Marais wa Marekani 4
2 Members of Congress 530
3 Cabinet Secretaries 60
4 Supreme courts justices 19

Hapo bado atujaenda kwenye nafasi zingine kifupi YALE ndipo wanatoka watu wanaorun dunia kwenye kila sector hata ukiangalia hizi secret societies zote kama Illuminate, Skull and Bones tafiti zao zote wanaozifanya ni wanafunzi wa Yale.

Haya tuje kwenye namba nimetaja namba 15,45,9 na 3
(15) 1+5=6
(45) 4+5=9
6,9,9 na 3
3 stands for Air,Land na Sea yani Dunia
6,9 zote zinagawika kwa 3 na jibu ni 2 na 3 so 2+3=5
5 stands for milango ya fahamu yani binadamu
so kwa pamoja unapata BINADAMU NA DUNIA code 5 na 3

SEHEMU YA PILI:
MCHANGO WANGU KUHUSU NGUVU YA ELIMU KWENYE MEDANI ZA UJASUSI

Izzo good to see you again brother.
Hili la Tanzania linatuumiza akili na mioyo watu wengi sana.
Ikumbukwe kwamba hizi harakati za kuihujumu Tanzania hazijaanza leo sema tuliamua tu kufumba macho.
Kuna kipindi miaka ya 90 huyu jamaa alijaribu kuuwa wanajeshi wa Tanzania nchini Congo DRC ikashindikana.
Leo hii na dunia ya mitandao, elimu yetu hafifu na nchi kukosa mwelekeo yakitokea yale ya Kagera siyo rahisi kupona.

Yote tisa naungana na wewe kabisa kwamba Maslahi ya nchi yatabaki kuwa maslahi ya nchi.
Lakini huwezi kujenga taifa Imara lenye nguvu kiuchumi na Kijeshi kama mamluki wameharibu elimu ya nchi kwa maksudi. Tanzania ilikuwa na nguvu sana miaka ya nyuma kwasababu ya Elimu. Wanafunzi wa awamu za mwanzo wakina Mzee Warioba, Mzee Mahiga na Mzee Samatta walifundishwa na walimu kutoka vyuo vikubwa kama Oxford University, Harvard University na Yale University: Ndiyo maana hata mambo waliyoyafanya yalikuwa ni yakuogopesha sana. Mfumo wa kutengeneza wasomi wenye tija ulikuwa ni wa tofauti sana.

Nguvu kubwa ya Uingereza ni Oxford University, Mataifa yote unayoyaona kuanzia Marekani yamejengwa na Oxford University. Cecil Rhodes alikuwa ni moja kati ya watu waliotamani sana Marekani irudi kuwa Koloni la Uingereza. Ukisoma Memoirs zake alivyokuwa na miaka 23 aliandika kama mtoto wa tajiri kwamba Uingereza ivamie Marekani tena.

Lakini alipokuwa mzee akagundua kwamba utawala wa mabavu haitasaidia hata kidogo, hivyo akapendekeza kwamba Uingereza ianze kutoa Scholarship kwa wanafunzi wenye akili sana wa Marekani. Anavyokufa aliaacha pesa nyingi sana kufanikisha huu mpango wake na hadi leo hii ndiyo tunaona kitu kama "The Cecil Rhodes Foundation".

Wamarekani wengi walisoma sana Oxford University na katika kufanya hivyo wakajikuta wana mawazo sawa na yale ya Waingereza. Hapa ndipo mwanzo wa mambo kama Ango-American Coalition na Special Relationship kuzaliwa. Soma hapa kuelewa zaidi: Cecil John Rhodes facts, information, pictures | Encyclopedia.com articles about Cecil John Rhodes

NB 1:Huu uhusiano na Oxford University ndiyo umeifanya Marekani kuwa taifa lenye nguvu hapa duniani hii leo. Ikumbukwe kwamba Sera za Mwanazuoni maarufu hapa dunaini katika Karne ya Ishirini Sir Halford McKinder ambazo ndizo zimewajenga Wanasiasa nguli kwenye mambo ya Ulinzi na Mahusiano ya Kimtaifa Dr.Henry Kissinger na Dr Zibgniew Brzezinski zilianzia Chuo Kikuu cha Oxford. Sir Halford McKinder ni mfano halisi wa wanafunzi wa Oxford ambao mkuu izzo amewazungumzia.

Kuna Nadharia aliiandika kuhusu Urusi inaitwa The Heartland Theory ambayo aliwaambia Waingereza na Wamarekani kwamba ili kutawala dunia ni lazima wakamate The Heartland ambapo ni eneo la Urusi na Ulaya Mashariki. Uingereza baada ya kujua kabisa kwamba hawezi tena kupambana na Ukomunisti ilibidi aanze kujipanga kutafuta ushirikiano mkubwa sana na Marekani. Marekani na Uingereza walianzisha The Council for Foreign Relations ambapo Sir Halford McKInder ndiyo alikuwa moja ya wasomi wakubwa kushauri mataifa ya Magharibi juu ya hatari za umoja wa kisovieti. Soma hapa kuelewa zaidi:pARAMETERS, US Army War College Quarterly - Summer 2000

Ikumbukwe kwamba Marekani alikuwa hana nguvu kubwa kidiplomasia kama Uingereza,
Na kuna taarifa zilizovuja kwamba Ikulu ya Raisi F. Roosevelt ilikuwa imejaa majasusi wa Uingereza wakiongozwa na Mkubwa wao Roald Dahl ambao walikuwa wanashawishi sana maamuzi ya nchi hadi uamuzi wa kuingia vita ya Pili ya dunia. Ilifika kipindi kwamba CIA (Central Intelligence Agency) inavyoanzishwa ambayo zamani illiitwa OSS (Office of Strategic Services) sehemu kubwa ya mafunzo yao ilifanywa na The British MI6. Soma hapa:When Roald Dahl Spied on the United States

Uingereza alikuwa mbele sana kutokana na uhalisia kwamba yeye alikuwa na uzoefu mkubwa wa kupambana na mataifa makubwa duniani kuliko Marekani. Hili lilitokana na kuwekeza sana kwenye Elimu kwa mifumo ya vyuo kama Oxford na Cambridge. Pia alikuwa ameanza kampeni ya kulinda maslahi yake tokea miaka ya 1600 hata Marekani hajazaliwa. Majasusi wake wamefanya operesheni za kijasusi (Clandestine) dhidi ya falme zenye nguvu kama Tsarist Russia, Imperial Germany, Imperial France, Republican France, Habsburg Austria, Imperial China, Imperial India and The Ottoman Caliphate. Wote hawa aliwakalisha kwasababu moja tu kubwa "ELIMU, ELIMU, ELIMU, ELIMU"

Isingekuwa wasomi wa Uingereza kumshauri mfalme kwamba Uhuru wa Marekani utainufaisha sana Uingereza basi huenda Marekani asingesaini Mkataba wa Paris (Pact of Paris) wa mwaka 1782 na asingekuwa taifa kubwa kama leo. Uingereza aliona mbali sana kwamba kuna siku Marekani itakuja kuwa na manufaa kwake.

Hukukosea kabisa, mwaka 1917 na 1941 Marekani alimsaidia sana sana Uingereza asiangamie. (Hizi ndizo faida za kuwekeza sana kwenye elimu na kuwaachia mamlaka watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri) Lakini sisi huku Watawala wetu wameona ni fahari sana kupambana na Raia wao kana kwamba ni wahalifu fulani hivi, wanaleta upendeleo wa kidini, kakabila na kikanda..Halafu mwisho wa siku wanaoshika hatamu ya uongozi wa watu zaidi ya milioni 40 Mungu mwenyewe anajua.

Haya sasa,
Huu mpango wa kusomesha wasomi ulikuja hadi nchi za Afrika baada ya Uhuru, ambapo Marekani alianza kusomesha watanzania wenye akili kupitia The Rockerfeller Foundation, huku Uingereza akisomesha watanzania wenye akili kwa kupitia The Common Wealth Capacity Building Programme.

Lengo lilikuwa ni kuwaandaa watanzania kifikra ili wawe na mlengo wa kisiasa ambao utawafanya wawe huru lakini pia wawe kwenye upande wa Mataifa ya Magharibi kipindi cha vita Baridi (Shaping the intellect of African minds into Ango-American purview of the world). Hapa ndipo wanafunzi wa kitanzania wenye uwezo wa kipekee kama Marehemu Prof Justinian Rweyemamu, Dr Augustine Mahiga , Prof Mathew Luhanga, Prof Kighoma Malima, Dr Salim Ahmed Salim, Andrew Chenge na Prof Ibrahim Lipumba wakatengenezwa.

Mzee Nyerere alipoenda nchini Canada miaka ya 60's, Alitoa hotuba nzuri ambayo iliwashangaza sana wazungu. Wakamuuliza hivi huko Tanzania kuna watu wenye akili kama wewe?

Mzee Nyarere akajibu na kusema kwamba yupo "Akamtaja Mzee Augustine Mahiga". Hapa usisahau kwamba huyu Mahiga na wenzake walisahwahi kufanya vurugu ya migomo pale Mlimani kipindi hicho panaitwa University of East Africa. The Rockefeller Foundation ikamfadhili na kumpeleka University of Toronto Canada akafanya Masters na PhD, na alivyorudi nchi yote ilinufaika sana na inanufaika sana mpaka leo na alichokipata kule.

Leo hii ukikaa na Dr Mahiga, au Marehemu Prof Rweyemamu kama umesoma maandiko yake,
Utakuja kugundua kwamba walikuwa ni wajamaa haswa wanaopenda nchi yao lakini wana mawazo fulani ambayo yako kimagharibi sana kama ambavyo Mzee Nyerere alikuwepo. Hii inawatofautisha sana na wale wasomi waliosoma nchi kama Uchina na Umoja wa Kisovyeti.

NB 2: Lazima tukubali kwamba kuvunja Ushirikiano wa kielimu na mataifa ya Magharibi kisa tofauti za kifalsafa ni makosa mabaya ambayo Mzee Nyerere na chuo chake cha Kijamaa cha Mlimani walifanya. Naamini sana katika Elimu ya Ujamaa na Kujitegemea lakini ni lazima tukubali kwamba hatuwezi kujenga elimu bora bila kushirikiana na mataifa makubwa yaliyoeendela Kitaaluma kama Uingereza na Marekani.

University of Oxford, Harvard University, Stanford University na Yale University vimetutangulia sisi sana kwasababu vimefanya tafiti kubwa zilizobadili mwelekeo wa dunia kwa ziadi ya miaka 100. Pia tusisahau kwamba vyuo vya Marekani viko mbele sana duniani kwasababu vichwa wote wa dunia wako pale. Mfano takwimu za haraka zinasema kwamba asilimia 50% ya PhD zote za Marekani ni Foreign Born, hivyo ni lazima watakuwa na Reserve ya kutosha ya wasomi wenye akili sana wanaofanya biashara ya Ujasusi, Jeshini, Uchumi na Siasa.

Ukisoma "The Road to Academic Excellence: The Making of the world Class Research University" ambao ni utafiti wa Bank ya Dunia wa mwaka 2011 umesema yafuatayo: Nchi haiwezi kuendelea kitaaluma bila kufanya EXCHANGE PROGRAMMES kwa wanafunzi na walimu. Wakatoa mfano hai ambao mimi sikuupinga kabisa kwamba hadi nchi kama Uchina inapeleka wasomi wake wakubwa kutoka vyuo kama Peking University kwenda kujifunza nje. Wamegundua kwamba ili waweze kutawala dunia njia pekee siyo kufanya siasa za woga, kikimbia na kujificha (The Politics of Fear).

Leo hii takwimu zinasema kwamba baada ya Kuanguka kwa jumuiya ya Kisovieti,
Matajiri wengi wa Urusi wanapeleka watoto wao kwenda kusoma nchi za Uingerea na Ulaya hasahasa kwenye masomo ya Uchumi na Sanaa. Sayansi Warusi wamejipanga sana sana kupitia vyuo vyao kama Moscow State University, University of Saint Petersburg na vinginevyo.

NB 3: Zamani Tanzania iliweza kupeleka wasomi wenye uwezo wa kipekee sana kuiwakilisha Tanzania kwenye mambo ya msingi. Nakumbuka Mzee Salim Ahmed Salim aliwahi kuwa Raisi wa Baraza la Ulinzi na Usalam la Umoja wa Mataifa na Dr Augustine Mahiga naye akaja kushika nyazifa hiyo baadae. Dr. Salim wakati yuko Umoja wa Mataifa aliweza kuisadia Tanzania kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Southern Rhodesia chini ya Serikali ya Ian Smith, huku Dr. Salim akiwa ndiyo Raisi wa hivyo vikwazo. Tanzania ilikuwa masikini lakini ilikuwa na watu makini sana sanaa. Mwaka 1972 Dr. Salim alikuwa moja ya watu walipigia debe Uchina kurudishwa Umoja wa mataifa na kupewe kura ya VETO huku Taiwan akifukuzwa. Ulikuwa huwezi kuja nchi za Afrika Mashariki na kati bila kuonana kwanza na wasomi wa Tanzania.

Kuna miaka taifa kubwa X liliwahi kutupa taka za kinyukilia (Nuclear Waste) kwenye misitu ya Congo DRC,
Lakini kilichowashangaza wazungu ni kwamba zile taarifa zilifika Ikuli ya Mzee Nyerere na wale majamaa walipigwa bonge la Mkwara na ikabidi wawe wapole na kuacha ule mchezo. Leo yetu hii kweli sisi Watanzania ni watu wa kupigwa mikwara na kale kanchi ambako ni kijinusu mkoa, isitoshe asailimia 70% ya viongozi wake ni sisi tuliowalisha, kuwafundisha na kuwaweka madarakani? (Hii nchi yetu lazima itakuwa na laana kwasababu hiki kiwango cha upumbavu hakikubaliki)

NB 4: Ilifika kipindi ilikuwa rahisi sana kufanya kazi za Ujasusi wa kimataifa na kushawishi mashauri makubwa sana ya kidiplomasia kwasababu Watanzania wengi walifanya kazi kwenye Mashirika makubwa ya kimataifa na hata kufundisha vyuo vikubwa sana vya nchi mbali mbali (hasa zile za Jumuiya ya Madola). Tulikuwa na Wizara ya mambo ya nje ndogo sana lakini mabalozi walifanya kazi kuliko hata yale mataifa makubwa yaliyokuwa na bejeti kubwa kuliko sisi. Mzee Warioba alishawahi hadi kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Kimataifa inayosimamia mipaka ya bahari: Hii mahakama watu wanaoingia ni wenye akili iliyotengenezwa haswaa. Leo hii mimi natoa ushahidi wangu binafsi bila kuleta majungu, nimeshuhudia nafasi ya Tanzania ikichukuliwa sana na Wakenya kwasababu wamekuwa na akili ya ziada kuliko sisi katika hili. ICRC na UN wamejazana sana Wakenya. Ukienda kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa kanda yetu hii Wakenya wamejazana na sasa Ukienda kule Netherlands na Geneva utashangaa ambavyo Wakenya wanafanya kazi ambazo zinaijengea Kenya kidiplomasia na Kiuchumi kwa miaka ijayo. Nimeona baadhi ya Marafiki zangu wa Kenya wakifanya Intern Mahakama ya ICC the Hague kwa wingi.

NB 5: Mwanasheria Mkuu Dr Kilangi anasema kwamba Wanasheria wa Tanzania wanapigwa chenga sana na Sheria za Kimataifa na hili limekuwa ni tatizo la nchi kupoteza kesi nyingi. Mimi nasema tutaachaje kushindwa wakati wanasheria wetu hawafundishwi vizuri? Law Schools nyingi hapa nchini zinafundisha watoto wakariri Civil Procedure Codes, Criminal Procedure Act na kuvizia Preliminary Objectives (PO) tu. Ukiwatoa nje ya hapa wanasheria wa Tanzania hawawezi kushindana kwenye soko la kimataifa, hata PhD wanaandika Maandiko yao kwa kujivuta ova wanalazimishwa (THINGS ARE JUST UGLY, AND ARE GETTING UGLIER EVERY DAY).

Juzi naona watoto fulani wa Kenya na Uganda wameandikiwa Recommendations za Kwenda Kusoma Oxford University,Harvard University, Leiden University, Geneva Academy of International Law na London School of Economics hadi nikaona wivu nikasema hizi ofisi za UN na ICRC zingekuwa na Watanzania huenda na sisi watoto wetu wangepata hizi nafasi. Moja ameenda kusomea mambo ya Conflict Analysis, Mwingine Law of War na International Criminal Justice, Mwingine Economics Law. Hapa nchi zao zitapata manufaa makubwa kutokana na Exposure watayopata huko: Mtoto kama huyu akija kuwa kiongozi nchi kwake ni lazima atafanya mambo makubwa na mazito tu.

Huwezi kucheza na mfumo wa Elimu wa nchi halafu ukategemea utabaki salama hata siku moja.
Hivi unategemea hawa wafanya maamuzi makubwa ya kiuchumi ya nchi kwenye mambo ya Kiusalama na Kiuchumi utawaokota tu au watashushwa na malaika kama mitume? Waswahili husema usipokuwa makini utachekwa hata na mbwa. Sasa leo tunafanyiwa figisu za kijinga na kanchi kadogo kama kale, ujumbe na Precedent ambayo inatengenezwa mbele ya mataifa mengine yanoyotuzunguka ni huu:
-Tanzania ni nchi dhaifu tofauti na zamani, simba huyu kazeeka tunaweza kumshika tu sharubu na tukabaki salama na wala hawawezi kufanya lolote lile.

HITIMISHO:
Haya mambo niliyoyaleta hapa hayapo kwa dhumuni la kuruhusu kejeli dhidi ya Serikali au Taifa letu bali kukosoa ili kujenga. Hivyo tujaribu kuwa waungwana na tujaribu kukosa yale mambo ambayo kweli tunahisi yanahitaji kurekebishwa (Tuzuie mihemko). Pili haya mambo yote ambayo tumeyaweka hapa yametokana na vyanzo vya wazi kama vitabu na vijarida mbalimbali.

Natanguliza shukrani zangu,

MALCOM YOUNG, JR
 
There is need to change our education system mbaya zaid ...kwenye core watoto wanafundishwa ... In a poor Way ... Wakuu inabidi tuwe serious we are not too late but we are ...
Kwenye kampen za 2015 mgombea kupitia chadema alisema vitu tunavyohitaji ni ELIMU , ELIMU , ELIMU
 
dah iz nondo si za mchezo na ni ukweli mtupu coz nowdays serikal yetu imejikita kwenye chaguzi zaidi mambo mengine yenye manufaa kwa nchi yetu kwa miaka 100 ijayo yamewekwa kapuni, nguvu zimewekezwa zaidi kwenye kuhakikisha wanabaki nadarakani kwa njia yoyote ile!!!, ndyo maana tunashuhudia vurugu nyingi mno kipindi hiki
 
Malcom, kuna hoja inatamkwa na wanazuoni kuwa Tanzania imepatwa na udumavu wa elimu.

Nimemsikia Dr Kahangwa akizungumza redioni kuhusu elimu wiki hii akisema kuwa Watoto wetu wengi huko mashuleni sio tu kuwa hawasomi inavyotakiwa lakini akili yao (imedumaa) si kama ya kizazi cha wanafunzi miaka kadhaa nyuma.

Hapa napata idea kuwa hata hiyo indirect recruitment inavyofanyika hasa ktk vyuo vya ndani kwa wanafunzi waliosoma ktk mfumo wetu wa elimu ndo hii shida inayozungumza hapa.
Na pia nafkiri wanaohusika na recruitment hawazizingatii shule binafsi za kimataifa km IST, HOPAC, etc kule kwa kiasi fulani wanapata elimu ya kimataifa hata ktk ngazi ya primary na secondary na Mara nyingi hata preference yako ya vyuo inakuwa ni vya ulaya na marekani ( first world).
Kungekuwa na utaratibu wa kufanya early recruitment ktk hizi shule pia.
Kama umeshakutana na hawa vijana akili zao ni tofauti sana na wale wenye level sawa ktk shule za "kawaida".
 
Malcom, kuna hoja inatamkwa na wanazuoni kuwa Tanzania imepatwa na udumavu wa elimu.

Nimemsikia Dr Kahangwa akizungumza redioni kuhusu elimu wiki hii akisema kuwa Watoto wetu wengi huko mashuleni sio tu kuwa hawasomi inavyotakiwa lakini akili yao (imedumaa) si kama ya kizazi cha wanafunzi miaka kadhaa nyuma.

Hapa napata idea kuwa hata hiyo indirect recruitment inavyofanyika hasa ktk vyuo vya ndani kwa wanafunzi waliosoma ktk mfumo wetu wa elimu ndo hii shida inayozungumza hapa.
Na pia nafkiri wanaohusika na recruitment hawazizingatii shule binafsi za kimataifa km IST, HOPAC, etc kule kwa kiasi fulani wanapata elimu ya kimataifa hata ktk ngazi ya primary na secondary na Mara nyingi hata preference yako ya vyuo inakuwa ni vya ulaya na marekani ( first world).
Kungekuwa na utaratibu wa kufanya early recruitment ktk hizi shule pia.
Kama umeshakutana na hawa vijana akili zao ni tofauti sana na wale wenye level sawa ktk shule za "kawaida".

Recruitment huwa inafanyika popote pale ambapo panakuwa na uhitaji ndani ya Taasisi za kijasusi,
Wakiona mtoto wa IST atawafaa basi watamchukua, wakiona mtoto wa Shule kama Kibaha anafaa basi pia watamchukua. Muhimu ni kwamba wapate watu wanaoweza kufanya taasisi itimize majukumu yake kwa weledi wa hali ya juu..


NB: Hoja hapa ni kwamba tunahitaji Elimu inayotolewa kwenye shule kama HOPAC na IST,
Au vyuo kama Oxford na Stanford hasa kwenye mambo ya tafiti, itolewe hapa nchini kwa kiasi kikubwa ili tuweze kupata viongozi wenye mitazamo mipana ya dunia kama alivyokuwa Mzee Nyerere.
 
Back
Top Bottom