Tido Mhando fuata mfano wa Raia Mwema

Jan 16, 2007
721
176
Tido Mhando Raia mwema wamekupa nafasi kijijitetea au kijibu hoja Hii ndio demokrasi hivyo ingelikua vyema kama TBC ingelikua inafuata mfano huo wa kutoa nafasi pia kwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani au watu wenye mawazo tofauti na yale ya serikali au CCM ingelikua vyema kama ungemwalika Mzee wa Vigongo (Johnson Mbwambo),katika kipindi maalumu au kumpa nafasi kutoa maoni yake.TBC inaendeshwa kwa kodi ya wananchi na sio kwa fedha za CCM



Uchambuzi wa Mbwambo haukunitendea haki


Tido Mhando
Septemba 30, 2009

Kwako Mzee wa Vigongo (Johnson Mbwambo),

Nataraji ya kwamba baada ya uchambuzi wako wa kina wiki mbili zilizopita na kufuatiwa na uchambuzi mwingine wiki jana wa msomaji wako Selemani Rehani kuhusu mahojiano ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyafanya na Watanzania, mwanzoni mwa mwezi huu, utanipatia nami fursa angalau ndogo tu ya siyo kutaka kujitetea bali kutoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu kitendo hiki cha kihistoria kutokea nchini hapa na labda kwenye kanda hii ya Afrika ya Mashariki.

Na hasa kama mlivyonichambua wewe na mwenzako, kwa ushiriki wangu na kuhusika sana kwenye mpango huu, ikiwa ni pamoja na kumsaidia kwa karibu mheshimiwa Rais kuwasialiana na waulizaji. Pia kama mtangazaji mwandamizi na mwenye uzoefu mkubwa kwenye fani hii ya utangazaji.



Tido Mhando
Hata hivyo, napenda kueleza kuwa nitazungumzia zaidi yale mambo mliyoyajadili kuhusu mimi pekee na labda TBC kama shirika la umma lilofanya kazi ya kurusha matangazo haya kwa niaba ya vituo vingine kadhaa vya televisheni na radio hapa nchini, na hivyo kwa mara ya kwanza kuonyesha mshikamano wa hali ya juu wa vyombo hivi.

Nimesema tayari kuwa hiki kilikuwa ni kitendo cha kihistoria kutokea kwenye kanda hii, ingawa wewe kwenye makala yako umegusia kwamba Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda pia hutumia mtindo kama huu. Hii si kweli. Mfumo wa utangazaji alioutumia JK safari hii ni wa phone in, ambapo mhusika au wahusika, hutumia mawasiliano ya simu pamoja na ujumbe wa simu kujibu moja kwa moja maswali ama maoni ya waulizaji.

Utaratibu kamili hufanywa, kama ilivyofanya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, wa jinsi gani waulizaji wanavyoweza kuuliza maswali ama kutoa maoni yao hayo.

Kwa upande wake, Rais Museveni hajawahi hata siku moja kutaka aulizwe maswali kwa mfumo huu, bali kile anachokifanya na ambacho yu maarufu sana, ni kwakuwa yeye ni msikilizaji mzuri wa vituo mbalimbali vya radio vya nchini mwake, basi huwa nyakati fulani fulani huchangia na yeye kwa simu kama msikilizaji mwingine, kwenye mada zinazojadiliwa na vituo hivyo, Na kwahiyo kamwe huu siyo ule utaratibu wa phone in nilioueleza hapo juu.

Utakelezaji wa utaratibu huu wa phone in huweza kufanywa kwa mitindo kadhaa, na hasa katika kile kinachoelezwa kuwa maswali ya nyongeza baada ya swali la msingi. Hapa muuliza swali anaweza kupewa nafasi hiyo au muulizaji mwingine pia huweza akachangia ama hata mtangazaji msaidizi anaweza akatoa maswali haya ya kujazia. Ila jambo la msingi hasa ni kiini halisi cha phone in hiyo, ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda na idadi ya wachangiaji.

Wakati ikitangaza utaratibu huu, Kurugenzi ya Mawsiliano ya Ikulu, ilisema bayana kwamba, Mheshimiwa Rais, atajibu, au kupokea maoni na hata ushauri moja kwa moja kutoka kwa wananchi wake na si vinginevyo.

Ingawaje tangazo hili lilikuwa la muda mfupi sana hadi kutimia muda wa kipindi, lakini Watanzania walilipokea kwa shauku kubwa mno. Wakati tulipoanza kipindi kile, tayari e-mail zaidi ya elfu mbili mia tano zilikuwa zimepokelewa na wapiga simu zaidi ya mia tano walikuwa wamekwisha kujiandikisha kutaka kuuliza maswali yao. Ni wazi idadi kubwa ilikuwa ikitarajiwa wakati wa kwenda kwa kipindi chenyewe.

Kwa maana nyingine, ilikuwa wazi kwamba Mheshimiwa Rais alikuwa anataka kusikia kauli za wananchi kutoka pote nchini na si vinginevyo.

Haya ndiyo yaliyokuwa madhumuni halisi ya mpango huu. Na ukizingatia wingi wa watu waliojitokeza kutaka kushiriki, hata ile nafasi finyu ya kutia swali la nyongeza haikuwepo, vinginevyo ingekuwa ni kuwanyima haki walengwa halisi.

Na sasa hapa ndipo linajitokeza lile suala lililojadiliwa sana hasa na wewe Mzee wa Vigongo (Mbwambo), kwamba nilishindwa kutia maswali ya ziada. Kwanza napenda kurudia ya kuwa haya hayakuwa majadiliano yangu binafsi na JK, kwahiyo kauli za kulinganisha wakati huu na wakati nilipokuwa BBC haupo kabisa.

Kipindi kile cha enzi za BBC kilikuwa ni changu, nikiuliza maswali ninayotaka, kitu ambacho naweza kukifanya hata sasa katika kipindi changu tofauti.

Na pia nina uhakika ya kwamba endapo ningeingiza maswali mengi ya nyongeza, kibao kingenigeukia kwa kulaumiwa kuwa nilichukua nafasi kubwa ya maswali kuliko wahusika, na hasa kwa kuwa wakati mwingine maswali haya ya ziada huhitaji majibu marefu ya kina labda kupita swali la msingi.

Kwa hakika nilitaka wananchi wengi wapate nafasi ya kuuliza maswali, na ndio maana wakati mmoja nilimtaka radhi Rais atoe majibu mafupi kiasi.

Na vivyo hivyo suala lako la kutaka kuwepo jopo la kutoka Jukwaa la Wahariri ama jopo la watu wengine wasomi, kama alivyoshauri msomaji wako Rehani, halikuwepo kwa wakati huu. Kwa kweli kwa sababu ya uhaba huo wa nafasi na muda, kama ilivyokuwa, hata wale walio pata nafasi ya kuuliza maswali, kwa makusudi kabisa, hawakupewa nafasi ya kuuliza swali lolote la nyongeza nia ikiwa ni ile ile ya kuwapatia wananchi wengi nafasi ya kuuliza maswali. Ikumbukwe ya kwamba waliiobuni utaratibu huu walichukua muda wa kutosha kutafakari mambo haya yote muhimu.

Vile vile Mzee wa Vigongo (Mbwambo) hata umediriki kusema ya kwamba nilikuwa namuogopa boss wangu. Kwa kweli sikuwa, na wala sina sababu yoyote ya kumuogopa Rais Kikwete, mtu ambaye nimewahi kukutana naye na hata kumhoji mara nyingi akiwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi.

Kile ninachoweza kuthibitisha kwako na wasomaji wako, ni kwamba namheshimu sana Rais wangu ambaye bila ya shaka ni Rais wako pia. Na sijui hili suala la boss linatoka wapi. Rais Kikwete ana mamlaka kwa watu wote wa nchi hii, na wala sio kwa baadhi ya watu tu.

Kama mwandishi wa habari mwandamizi wa zaidi ya miaka arubaini sasa, (nilianza kazi ya kutangaza Januari 13, 1969), nimegundua ya kwamba heshima kwa viongozi ni jambo muhimu mno.

Ni tabia hii ndiyo iliyonifanikisha kupata nafasi ya kuwa karibu sana na viongozi wote wa juu wa nchi zetu hizi za Afrika ya Mashariki na kati. Viongozi wengi wanahitaji kukuamini na wala hawana woga na maswali. Acha nikupatie mifano michache tu ya kibinafsi.

Nakumbuka siku moja nilikuwa napiga soga huku nikicheka na Rais wa zamani wa Kenya, Daniel Arap Moi kwenye uwanja wa ndege. Alipoondoka waandishi wa Kenya waliniuliza niliwezaje kuwa karibu naye hivyo wakati wao hawathubutu kabisa.

Katika tukio jingine, nilimpigia simu wakati mmoja hayati, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere akiwa ndio tu amefika hotelini Nairobi nikamuomba nimhoji. Kwa kawaida alikuwa hapendi sana mahojiano haya ya simu, lakini alipoelezwa na wasaidizi wake kwamba ni mimi, alikuja na kuniambia kwa mzaha ya kwamba endapo chai yake aliyokuwa anakunywa itapoa, basi, nitailipa. Tuliongea kwa zaidi ya nusu saa.

Marehemu Rais Laurent Kabila alinikaribisha mwenyewe kwenda Kinshasa, DR Congo. Nilipofika huko, Balozi wa Uingereza aliniambia nimepoteza muda; maana kiongozi huyo alikuwa hana wakati wa kuonana na watu hata viongozi wengine waliokwenda kumtembelea walishindwa kumuona.

Siku ya pili yake, Rais Kabila aliniita saa tano usiku, tukaongea kwa muda wa zaidi ya saa mbili kwenye sebule ambayo wiki tatu baadaye alipigwa risasi akauwawa.

Wakati mmoja nilikuwa na mihadi na Rais Museveni wa Uganda shambani kwake Rwachitura, Mbarara, Kilomita kadhaa kutoka mjini Kampala. Kwa kawaida akiwa shambani huko huwa pia anakutana na watu wengi sana, hasa vikundi vya wananchi mbali mbali.

Alipoona muda unapita, aliniletea ujumbe mwenyewe kuniambia nisijali, hata iweje tutaongea; maana anataka nimpatie habari za Wabondei (alisema kwa utani). Aliniita saa saba usiku na tukaongea hadi saa tisa alfajiri.

Phone in nyingine iliyofana sana hapa Tanzania ni ile ya mwaka 2000 nilipowaleta pamoja Rais Amani Karume, wakati huo akiwa ndio tu kachaguliwa na CCM kuwania nafasi ya Urais, na Maalim Seif Sharif aliyekuwa amesimamishwa na CUF.

Haikuwa vyepesi hivyo, kwa wao kukubali kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wapiga simu mbalimbali, na hasa kwa kuwa hata kipindi cha kampeni kilikuwa hakijaanza. Lakini wagombea wote walikuwa wameniamini.

Halikadhalika nilifanya phone in nyingine na Rais Paul Kagame wa Rwanda pamoja na Dk. Salim Ahmed Salim wakati alipokuwa Katibu Mkuu wa OAU.

Nimetoa mifano hii kuonyesha ni kwa jinsi gani heshima kwa viongozi huweza kukupatia mwandishi wa habari ufanisi kwenye kazi yako. Kwa hiyo narejea tena kwamba ndiyo namheshimu sana Rais Kikwete na wala sina sababu ya kuwa muoga.

Kwa upande mwingine Mzee wa Vigongo (Mbwambo) sikuilewa hoja yako uliposema kwenye makala yako ya wiki jana ulipanga awali kuchapisha maoni ya wengi waliokuwa wamechangia kuhusu makala uliyoiandika, lakini baadae ukaamua kuchapisha maoni ya msomaji mmoja tu, Selemani Rehani kwa kuwa yalikuwa yamewasilisha maoni ya wengi.

Nami pia uchambuzi wangu haukubaliana na hilo, nadhani ulitaka tu kuweka maoni ya mtu aliyeunga mkono hoja zako. Uandishi wa habari weledi unataka maoni ya aina yote yapewe nafasi. Na kamwe haiwezekani kwamba wale wote waliochangia walikuwa wanakubaliana nawe, hata kama walikuwepo wachache waliotofautiana nawe, (na naamini walikuwepo) basi hao ungewapa nafasi wanayostahili ukaweza kuonyesha maoni ya pande zote mbili za shilingi, hivyo ndivyo uwandishi wa habari adilifu unavyotaka.

Kwa kumalizia napenda kusema tena ya kwamba mimi nimejaribu kuelezea tu kwa kiasi baadhi ya mambo mliyoyagusia kwenye maandishi yenu kunihusu mimi na kipindi kile cha mwanzoni mwa mwezi.

Kwa ujumla wewe na wengine kadhaa mlikuwa na haki bila ya wasi wasi ya kutoa maoni hayo, jambo lililobainisha mafanikio ya msingi yaliyopata kipindi kile.

Kwanza kabisa hakuna shaka kwamba ndiyo kipindi kilicho angaliwa na kusikilizwa na Watanzania wengi zaidi kuliko kipindi kingine chochote mwaka huu. Wakati mmoja mitambo ya shirika la simu TTCL, ilishindwa kuhimili mtiririko wa simu zilizokuwa zikiiingia kwa wingi mno.

Na pia siyo tu Watanzania walioangalia kipindi hiki, huko Kenya wananchi wa huko wamewataka viongozi wao, hasa Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga, kuiga mfano huu wa Rais Kikwete.

Halikadhalika wananchi wengi wa nchi jirani za Burundi na Rwanda pia walivutiwa sana na kipindi hiki. Kwa ujumla, kama tunavyofahamu sisi waandishi wa habari, hali hii inabainisha ya kwamba ubunifu huu umepata mafanikio makubwa kwani bila ya shaka ujumbe uliotakiwa kutolewa uliwafikia walengwa.
 
Tido, we need a level playing field in your institution. Usidhani kwavile uliletwa na wanamtandao kutoka BBC basi lazima wao peke yao uwape ujiko kwenye radio na TV zetu!! The equal treatment principle must be applied.
 
Back
Top Bottom