Sura ni mwanajeshi ila mawazo ni ya Polepole

Sura ni mwanajeshi ila mawazo ni ya Polepole

Dogo ni mkufunzi wa ndege za kivita - captain wa ndege za kivita (mkufunzi) si mtu mwepesi kama tunavyodhani.
Tunaomba Kanali ( Mkuu wa kambi ya Airwing) ajitokeze akanushe kwamba yule kijana si wa kambi yake.
Akanushe akiwa kajifungia wapi kwa mfano?
20251004_201233.jpg
 
Dogo ni mkufunzi wa ndege za kivita - captain wa ndege za kivita (mkufunzi) si mtu mwepesi kama tunavyodhani.
Tunaomba Kanali ( Mkuu wa kambi ya Airwing) ajitokeze akanushe kwamba yule kijana si wa kambi yake.
Akanushe ili iweje? Kwa nini mnapenda sana kuishi kwa ulaghai na uongo?

CCM wamezinajisi sana akili zenu.
 
Kwasasa nchi imefika pabaya
Rais anapaswa kujua ccm mtandao wanamhujumu asipokuwa makini atakuwa na mwisho mbaya sana
 
Tujifunze kwa tapeli na fisadi la IPTL bw. SETH
Kwa sasa tukikamata fisadi tusiishie kuliweka lock up mafisadi hufanikiwa kutoana baadae.

Kwa sasa Fisadi anapaswa kutolewa riport ya kwamba aliruka kwenye gari la polisii wakati tunaenda kufanya uchunguzi nyumbani kwake😃
 
This is nothing more than a transient political tide brought about by the general elections, one that shall eventually subside, leaving CCM to persist in plundering the nation with their customary ruthlessness and utter lack of compassion.
Church!
 
Nchi ilipofikia kazi kweli kweli kuongea lugha moja
 
Polepole alisema wakikaza shingo watashusha maboya kama kwenye ndege inapotokea hali ya hatari🐼
 
Sura kweli ni mwanajeshi,

Sare kweli ni za kijeshi,

Ila mawazo (Talking Points) ni ya ndugu Humphrey Polepole.

Wale wana-CCM ambao walidhani kwamba Polepole ana ushawishi mdogo hapa nchini, kwamba ni mtu wa kupuuzwa walifanya mahesabu yao vibaya mno. Malalmiko yote ya kuharibika kwa Tanzania yanawalenga watu wakubwa wafuatao, Jakaya Kikwete, Edward Lowassa, Benard Membe na Rostam Aziz. Malalamiko ya ndugu H.Polepole yamegeuka kuwa The Official Narrative Against CCM's Rulling Elites, na hamuwezi kufanya lolote lile.

Mwanadamu anaweza kuficha mambo mengi, lakini hana uwezo kuficha JUA, MWEZI na UKWELI.
==========================================================
CCM na Watanzania huwa tuna kumbukumbu ndogo mno kwamba Tanzania hayawezi kutokea machafuko, lakini tunasahau kwamba yaliwahi kutokea huko nyuma zaidi ya mara nne kwa nyakati tofauti. Miaka ya 60 yalitokea, miaka ya 70 yakatokea na miaka ya 80 yakatokea, yakiongozwa na maafisa wa jeshi ambao hawakuridhika na sera za TANU/ASP/CCM.

Utofauti kipindi kile na kipindi hiki ni mmoja tu: UHALALI WA SERIKALI (Legitimacy). Serikali ilikuwa inaungwa mkono na wananchi wengi, hivyo jeshi lingepata shida kutawala hata kama wangefanikiwa. Mzee Nyerere alichokwa na sera zake, lakini watanzania walimuheshimu mno na wengi ndani ya vyombo vya usalama walikuwa na maswali kama:
​
  • Akishaondoka Mzee Nyerere nani atakuwa mbadala wake ?​
  • Huo mbadala wa Mzee Nyerere anaweza kuwa na hulka za kizalendo ? ​
  • Nyerere alikuwa na wafuasi kote Africa, ambao wamepita Tanzania na kuwa hadi maraisi wa nchi mbalimbali, unadhani tukimtoa Mzee Nyerere kinguvu hawataihujumu Tanzania na hata kuvamia nchi kijeshi ?​
  • Vipi kuhusu watanzania wa kawaida, mtawaambia nini kuhusu Nyerere wao ambaye kwao ni kama BABA na MUNGU MTU ?​
Madam Samia na Al-Hajj Kikwete hawana hii HOME FIELD ADVANTAGE, kwasababu wanabadilishika (They're Not Indispensable). Hawana kitu cha ziada ambacho kitafanya watanzania wawalilie zaidi zaidi ya sababu za UDINI na MASLAHI BINAFSI tu.

CCM + TISS, mlionywa sana, miaka na miaka. Haya mnayoyafanya yatakuja kuwatokea puani. Acheni matumizi mabaya ya vyombo vya dola na kuviingiza kwenye siasa za moja kwa moja na kuhujumu watu. Leo hii vyombo hivi vinaanza kufanya siasa dhidi yenu mnalalamika. Tulipofika hapa, sipo pazuri na sidhani kama kuna MWAFAKA WA KISIASA unaweza ukaleta SULUHISHO kwasababu kila upande uko kwenye vita ya uhai wake.

Wale wanaojiita kwamba ni WAZALENDO wanaamini kwamba CCM MTANDAO wakivuka 2025 basi Tanzania imekwisha. Huku CCM MTANDAO wanaamini kwamba wakitolewa MADARAKANI watashughulikiwa ipasavyo kuliko hata ambavyo JPM aliwashughulikia. Mara ya mwisho waliponea chupu-chupu, kipindi hiki watauwawa kabisa au kufungwa.

MWANADAMU HUVUNA ALICHOKIPANDA.......
MIAKA 30 TOKEA 1995, sasa CCM wanavuma walichokipanda miaka yote......
​
Na waombe Mungu atakayechukua nchi asiwe na hulka za Kitundu Lisu tundu Lisu, hapo ndio wataimba na kusaga meno

Mimi nilianza kuona dalili za "wakubwa" kuwachoka "wakubwa wao" hasa hasa kufuatia kauli za hivi karibuni za Mwanasheria mkuu wa serikali kwenda kwa wanataaluma wenzake

Zile kauli zinaonekana kama za "masononeko" kwamba kuna vitu wanafanya nje ya taaluma zao kukidhi matakwa ya wengine bila wao kupenda lakini wanaobena zigo la dhambi ni wao
 
Back
Top Bottom