Sura ni mwanajeshi ila mawazo ni ya Polepole

Sura ni mwanajeshi ila mawazo ni ya Polepole

Sura kweli ni mwanajeshi,

Sare kweli ni za kijeshi,

Ila mawazo (Talking Points) ni ya ndugu Humphrey Polepole.

Wale wana-CCM ambao walidhani kwamba Polepole ana ushawishi mdogo hapa nchini, kwamba ni mtu wa kupuuzwa walifanya mahesabu yao vibaya mno. Malalmiko yote ya kuharibika kwa Tanzania yanawalenga watu wakubwa wafuatao, Jakaya Kikwete, Edward Lowassa, Benard Membe na Rostam Aziz. Malalamiko ya ndugu H.Polepole yamegeuka kuwa The Official Narrative Against CCM's Rulling Elites, na hamuwezi kufanya lolote lile.

Mwanadamu anaweza kuficha mambo mengi, lakini hana uwezo kuficha JUA, MWEZI na UKWELI.
==========================================================
CCM na Watanzania huwa tuna kumbukumbu ndogo mno kwamba Tanzania hayawezi kutokea machafuko, lakini tunasahau kwamba yaliwahi kutokea huko nyuma zaidi ya mara nne kwa nyakati tofauti. Miaka ya 60 yalitokea, miaka ya 70 yakatokea na miaka ya 80 yakatokea, yakiongozwa na maafisa wa jeshi ambao hawakuridhika na sera za CCM.

Utofauti kipindi kile na kipindi hiki ni mmoja tu: UHALALI WA SERIKALI (Legitimacy). Serikali ilikuwa inaungwa mkono na wananchi wengi, hivyo jeshi lingepata shida kutawala hata kama wangefanikiwa. Mzee Nyerere alichokwa na sera zake, lakini watanzania walimuheshimu mno na wengi ndani ya vyombo vya usalama walikuwa na maswali kama:
​
  • Akishaondoka Mzee Nyerere nani atakuwa mbadala wake ?​
  • Huo mbadala wa Mzee Nyerere anaweza kuwa na hulka za kizalendo ​
  • Nyerere alikuwa na wafuasi kote Africa, ambao wamepita Tanzania na kuwa hadi maraisi wa nchi mbalimbali, unadhani tukimtoa Mzee Nyerere kinguvu hawataihujumu Tanzania na kuvamia nchi kijeshi ?​
  • Vipi kuhusu watanzania wa kawaida, mtawaambia nini kuhusu Nyerere wao ambaye kwao ni kama BABA na MUNGU MTU ?​
Madam Samia na Al-Hajj Kikwete hawana hii HOME FIELD ADVANTAGE, kwasababu wanabadilishika (They're Not Indispensable). Hawana kitu cha ziada ambacho kitafanya watanzania wawalilie zaidi zaidi ya sababu za UDINI na MASLAHI BINAFSI tu.

CCM + TISS, mlionywa sana, miaka na miaka. Haya mnayoyafanya yatakuja kuwatokea puani. Acheni matumizi mabaya ya vyombo vya dola na kuviingiza kwenye siasa za moja kwa moja na kuhujumu watu. Leo hii vyombo hivi vinaanza kufanya siasa dhidi yenu mnalalamika. Tulipofika hapa, sipo pazuri na sidhani kama kuna MWAFAKA WA KISIASA unaweza ukaleta SULUHISHO kwasababu kila upande uko kwenye vita ya uhai wake.

Wale wanaojiita kwamba ni WAZALENDO wanaamini kwamba CCM MTANDAO wakivuka 2025 basi Tanzania imekwisha. Huku CCM MTANDAO wanaamini kwamba wakitolewa MADARAKANI watashughulikiwa ipasavyo kuliko hata ambavyo JPM aliwashughulikia. Mara ya mwisho waliponea chupu-chupu, kipindi hiki watauwawa kabisa au kufungwa.

MWANADAMU HUVUNA ALICHOKIPANDA.......
MIAKA 30 TOKEA 1995, sasa CCM wanavuma walichokipanda miaka yote......
​
Talking points……,
 
Unajua polepole aliamua kukichafua aliponyimwa maslahi? Halafu wajeda wamemwamini sana cause haiwezekani balozi mwenye elimu yake aongee upuuzi. Na tena alivyotenguliwa tu, wajeda wakamwamini kwamba anayoongea ni ukweli! #oktoba tunakiwasha. Its now or never!
 
Mimi nimesema awe JW au sio JW but ameongea maneno ambayo yanapendwa na wananchi wengi CCM mtandao inatakiwa kuachia hii nchi kwa amani muendelee kula hizo pesa mlizochuma tofauti na hapo mtu atatoka na bikini au Boxa mbio
 
Huku CCM MTANDAO wanaamini kwamba wakitolewa MADARAKANI watashughulikiwa ipasavyo kuliko hata ambavyo JPM aliwashughulikia. Mara ya mwisho waliponea chupu-chupu, kipindi hiki watauwawa kabisa au kufungwa.
Ova
 
Kwasaea vita ya kushika dola Kia upande umeamua liwalo na liwe. Tunaelekea kwenye machafuko kama mzaha.
Kuwa na amani mkuu! Watanzania wengi hawako tayari Kwa machafuko.
Kwa Sasa watanzania bado tumelala tumejaa ujinga ujinga mwingi
 
Unajua polepole aliamua kukichafua aliponyimwa maslahi? Halafu wajeda wamemwamini sana cause haiwezekani balozi mwenye elimu yake aongee upuuzi. Na tena alivyotenguliwa tu, wajeda wakamwamini kwamba anayoongea ni ukweli! #oktoba tunakiwasha. Its now or never!
It is now or never
 
Unajua polepole aliamua kukichafua aliponyimwa maslahi? Halafu wajeda wamemwamini sana cause haiwezekani balozi mwenye elimu yake aongee upuuzi. Na tena alivyotenguliwa tu, wajeda wakamwamini kwamba anayoongea ni ukweli! #oktoba tunakiwasha. Its now or never!
Polepole alinyimwa maslahi gani wakati alikuwa Balozi.
 
Kwa mujibu wa Akashic records,walimwengu watabe kama kina hayati Sheikh Yahya,walishayasema haya Kwa sasa ishakuwa ile collective consciousness watanzania wanaipata,wanajua mambo Kwa undani kabisa.Sasa vibrational forces kama hizi huwa hazizuiliki kama walimwengu washayaona haya basi wameyaona kupitia Akashic records.
Yajayo sio poa,tuombe sana Mungu,tuvuke salama.
 
Back
Top Bottom